SIMBACHAWENE: Sikufumaniwa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

SIMBACHAWENE: Sikufumaniwa

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Mungi, Jun 24, 2012.

 1. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #1
  Jun 24, 2012
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,986
  Likes Received: 445
  Trophy Points: 180

  [​IMG]
  NAIBU Waziri wa Nishati na Madini, George Simbachawene, ameibuka na kukanusha vikali uvumi ulioenea jana kuwa amefumaniwa na mke wa mtu mjini Singida usiku wa kuamkia jana na kujeruhiwa mkono kwa kisu.


  Akizungumza na waandishi wa habari mjini Karatu jana jioni, Simbachawene ambaye pia ni Mbunge Kibakwe (CCM) mkoani Dodoma, alisema habari hizo ni uongo na kudai kuwa zimeenezwa na baadhi ya wabunge wa Chadema aliokutana nao mjini Singida jana wakati akiwa njiani kwenda msibani Karatu.

  Alisema kuwa katika hoteli aliyofikia, kuna mtu alifumaniwa akiwa na mke wa askari na kufafanua kuwa watu walizua jambo hilo kwa kuwa naye alilala katika hoteli hiyo.


  "Ni uzushi tu walidhani kuwa mimi nimefumaniwa, ukweli ni kwamba jambo hilo halijanitokea. Mimi nilifika hapa jana (juzi) nikitokea Dodoma kuelekea Karatu kuhudhuria msiba wa shemeji yangu," alisema Simbachawene.

  Aliwataja watu wanaodaiwa kueneza uvumi huo hizo kuwa ni wanachama wanane wa Chadema akiwemo Mbunge wa Viti Maalumu kupitia chama hicho, Christina Lissu.

  "Baada ya kufika Singida nilikwenda katika baa moja na kuwakuta wabunge wa Chadema na baadhi ya wanachama, nilipata kinywaji na kurudi hotelini kulala," alisema Simbachawene.

  Huku akivua shati kuwaonesha waandishi wa habari kwamba hakukatwa mapanga mikononi kama ilivyodaiwa, alisema kuwa alipoamka asubuhi ndipo alianza kusikia habari kuwa amefumaniwa na mke wa mtu.

  Awali taarifa kutoka Singida zilizowekwa pia kwenye mitandao ya kijamii zilidai kuwa Naibu Waziri huyo alikumbwa na mkasa huo jana alfajiri.

  Tukio hilo ambalo inaelezwa kuwa lilitoka majira ya saa kumi, baada ya taarifa hizo kumfikia mwenye mke, ilimlazimu mmiliki wa hoteli hiyo kutoa taarifa Polisi ili kuzuia maafa zaidi

  Uvumi huo ulidai kuwa baada ya taarifa hizo, iliwalazimu askari Polisi kwenda katika hoteli hiyo ili kumuokoa Simbachawene, ambaye tayari alikuwa amejeruhiwa mkono kwa sime na askari huyo mwenye mke.

  Mara baada ya purukushani hizo katika eneo hilo Naibu Waziri huyo alidaiwa kwenda kutoa taarifa katika kituo cha Polisi mkoani Singida, ambapo ilidaiwa kuwa katika maelezo yake aliandika jina la Josephat Joseph badala ya kutumia jina lake halisi.

  Hata hivyo, Mbunge Christina Lissu, alisema anashangazwa na taarifa za yeye kuhusishwa kueneza uvumi huo.

  Alisema walikutana na Naibu Waziri huyo, katika hoteli hiyo, wakiwa wanatoka mkoani Tabora katika kesi na wabunge wa Chadema, Conchesta Rwamlaza, Philipa Muturano na John Mrema ambaye ni Mkurugenze wa Bunge na Halmashauri ya chama hicho.

  " Tulipofika Singida nilimwoa Simbachawene nimwita jina, alitufuata na kutununulia vinywaji hapo hotelini," alisema Lissu na kuongeza;

  "Hata tulipofika hoteli, baada ya muda tukasikia kutoka kwa mmiliki wa hoteli akisema kuna watu wanataka kumharibia biashara. Tulipomuuliza kulikoni? Akasema kwani hamna habari si mmewaona Polisi wakati mnaingia hapa, huku akisema kuna kigogo wa Serikali amefumaniwa na mke wa askari."

  Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Singida, Linus Sinzumwa alipoulizwa na Mwananchi Jumapili alisema hakuna tukio kama hilo lililotokea mjini Singida wala mahali popote katika mkoa huo.

  "Huo ni uzushi tu, hakuna tukio hilo mjini Singida na wala sijasikia taarifa zozote za aina hiyo kutoka maeneo mengine mkoani hapa, alisema Sinzumwa.

  MY TAKE:
  Kweli Pesa mwanaharamu! Uongo unaweza kugeuzwa kuwa ukweli na ukweli kuwa uwongo!
  Kamanda wa Polisi ndiyo katuchanganya kabisa. Simbachawene amekiri kuwa ni kweli tukio lilitokea katika hoteli hiyo, lakini lilimhusisha mtu mwingine, huku RPC anatuambia hakuna tukio kama hilo!
  Au ndio ukweli umeuzwa?


   
 2. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #2
  Jun 24, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Pigo lingine kwa chadema, uongo na uzushi ndio uliowajaa vinywani mwao.
   
 3. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #3
  Jun 24, 2012
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,986
  Likes Received: 445
  Trophy Points: 180
  CHADEMA wanahusika vipi na fumanizi hili mkuu?
  Tutajuaje kama Simbachawene kanunua media pamoja na idara ya usalama kuugeuza ukweli kuwa uwongo?
   
 4. sweetlady

  sweetlady JF-Expert Member

  #4
  Jun 24, 2012
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 16,982
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Ukweli umeuzwa!
   
 5. sweetlady

  sweetlady JF-Expert Member

  #5
  Jun 24, 2012
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 16,982
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Kwani wewe una uhakika gani kama simbachawene hajahonga vyombo vya habari?
   
 6. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #6
  Jun 24, 2012
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,986
  Likes Received: 445
  Trophy Points: 180
  Simbachawene alifumaniwa, na picha alipigwa. wasi wasi wangu ni kwamba labda kawahonga mpaka waliompiga picha hahaaaaaaaaaa!!!!!!!!!
  Mi nasubiri gazetu la uwazi tutacheka sana!
   
 7. mtotowamjini

  mtotowamjini JF-Expert Member

  #7
  Jun 24, 2012
  Joined: Apr 23, 2012
  Messages: 4,540
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  mwenye hoteli:kigogo wa serikali kafumaniwa na mke wa askari
  Kigogo wa serikali:sikufumaniwa mimi ila ni mtu mwingine
  Polisi:hakuna tukio kama hilo limetokea katika hotel hiyo

  labda tumuulize na Rais labda yeye amepewa information nyingine
   
 8. B

  Bob G JF Bronze Member

  #8
  Jun 24, 2012
  Joined: Oct 5, 2011
  Messages: 2,354
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Mi siwagi na imani na Polisi kutokana tabia yao ya kutoa taarifa iliyotofauti na tukio lenyewe. Niwie Radhi Mh. Simbachawene.
   
 9. M

  Mjenda Chilo JF-Expert Member

  #9
  Jun 24, 2012
  Joined: Jul 20, 2011
  Messages: 1,425
  Likes Received: 63
  Trophy Points: 145
  Asubiri tu, kwa unywaji wake anytime, au kwakuwa kawa waziri? sisi wazee wa vingunguti twamjua huyu bwana mkubwa.
   
 10. t

  thatha JF-Expert Member

  #10
  Jun 24, 2012
  Joined: Apr 29, 2011
  Messages: 15,234
  Likes Received: 179
  Trophy Points: 160
  simbachawene ni mzinzi sana huyo jamaa mi namfahamu sana anakula mpaka watoto wa shule.
   
 11. sweetlady

  sweetlady JF-Expert Member

  #11
  Jun 24, 2012
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 16,982
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Teh teh teh......hata hawajui kujipanga ..... yaani huyo kamanda wa police ndio kauza mechi manake anakataa hakuna tukio kama hilo mkoani kwake!
   
 12. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #12
  Jun 24, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Kama kweli mbona nyuzi imeondolewa humu au na kina Max nao wamehongwa?
   
 13. Lyimo

  Lyimo JF-Expert Member

  #13
  Jun 24, 2012
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 3,828
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Scenario kama hii ilitegemewa. Tutarajie mkanganyiko zaidi wa hii habari kama ile ya Morogoro iliyotokea hivi Karibuni.
   
 14. Nsabhi

  Nsabhi JF-Expert Member

  #14
  Jun 24, 2012
  Joined: Feb 23, 2011
  Messages: 1,096
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Kafuniwa Simbachawene. Kwa nini taarifa yake na ile ya RPC zinajichanganya? Mbona Mwigulu Nchemba alifumaniwa? Ni kawaida yao CCM kufumaniwa maana wamewekeza kwenye ngono badala ya maendeleo ya wananchi.
   
 15. sosoliso

  sosoliso JF-Expert Member

  #15
  Jun 24, 2012
  Joined: May 6, 2009
  Messages: 7,519
  Likes Received: 1,857
  Trophy Points: 280
  Ni vizuri kama habari hii ingekuja na pics..
   
 16. t

  tupak Member

  #16
  Jun 24, 2012
  Joined: Jun 22, 2012
  Messages: 32
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Huyu kamanda bure kabisa tukio ni kweli limetokea ila siyo mheshimiwa unaposema hakuna tukio kama hili tumweleweje?
   
 17. Nduka

  Nduka JF-Expert Member

  #17
  Jun 24, 2012
  Joined: Dec 3, 2008
  Messages: 8,483
  Likes Received: 765
  Trophy Points: 280
  Wewe amekuacha kweli?
   
 18. sembuli

  sembuli JF-Expert Member

  #18
  Jun 24, 2012
  Joined: Feb 3, 2012
  Messages: 762
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 45
  Mazingira ya tukio yanachanganya, KWANI MH SIMBACHAWENE , KULIKUWA NA ULAZIMA GANI WA KULALA NYUMBA YA WAGENI KWA SAFARI FUPI KAMA HIYO YA KWENDA KARATU?? ndio maana wanakuhusisha na hilo tukio,,, kwa nini ulale guest house njiani wakati unasafiri safari fupi ya kufika siku hiyohiyo? kuna kitu lazima kama hukufumaniwa wewe basi ungeweza kufumaniwa ki mazingira
   
 19. N

  Njoka Ereguu JF-Expert Member

  #19
  Jun 24, 2012
  Joined: Apr 7, 2012
  Messages: 822
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 35
  Haya ndiyo watanzania tunapenda kupotezea muda. Amefumaniwa au hajafumaniwa si sehemu ya mkakati wa maendeleo ya taifa hili, zaidi ya gharama kwa maana ya muda tunaotumia kujadili na kutafuta ukweli kuhusu hili. Ukweli anaujua mwenye mke, mke na aliyefumaniwa.
   
 20. F

  FJM JF-Expert Member

  #20
  Jun 24, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Mh Simbachawene kafanya vizuri kutoa maelezo, huo ndio ukomavu wa kisiasa. Ila naona bwana afande kaharibu kabisa maana anasema hakuna tukio la fumanizi liliotekea mkoani Singida! tuko ground zero?

  Simbachawene pia anatakiwa achunge mdomo wake, unless ana ushahidi- beyond reasonable doubt, kitendo cha kuanza ku-link hizi taarifa tata na watu/chama ni kuzidi kuendeleza malumbano. Ana tofauti gani na hao anaowatuhumu kuwa wanaeneza uwongo kama na yeye anazua uwongo dhidi ya wengine?
   
Loading...