Simbachawene live on Star Tv: Gesi itatunufaishaje?

Simbachawene live on Star Tv: Gesi itatunufaishaje?

Fortilo

JF-Expert Member
Joined
Apr 10, 2012
Posts
5,890
Reaction score
17,744
mh naibu wazir wa nishat na madini anaongea live statv kuhusiana na suala la ges mtwara pamoja na wachambuz wengine, anaxema ges inaletwa daslam il kuendesha uchumi wa nchi, only 14pecent to dsm, gvt shares 60percent, fuatilia
 
Atuambie gharama za ujenzi ni halisi?kuna hoja kwamba zimekuwa inflated sana je huu is ufisadi mwingine?
 
mh naibu wazir wa nishat na madini anaongea live statv kuhusiana na suala la ges mtwara pamoja na wachambuz wengine, anaxema ges inaletwa daslam il kuendesha uchumi wa nchi, only 14pecent to dsm, gvt shares 60percent, fuatilia

Ndugu Mtangazaji.

SWALI LANGU:

1. NI KWA NINI NGUVU KUBWA INATUMIKA KUTOA MAELEZO MAZURI KAMA KWELI WANAMTWARA WALISHAONA MANUFAA YA GESI HASA BAADA YA WANAMTWARA KUANDAMANA?

2. WAZIRI ANASEMA SERA NDIYO INAANDAKIWA NA WAKATI HUO HUO SERIKALI ILISHAINGIA MIKATABA NA KAMPUNI ZA GESI. NAOMBA AKIRI KWA WATANZANIA KWAMBA VIONGOZI WA SERIKALI WALIKURUPUKA KUINGIA MIKATABA KABLA YA KUWA TAYARI NA HIVYO IPO HARUFU YA UFISADI. VINGINEVYO KILA KITU KISIMAMISHWE NA KIANZE UPYA.
 
Yuko hewani moja kwa moja na anaelezea vizuri tu kwamba sera ya gesi inaandaliwa na muda si mrefu itakuwa tayari.
 
Maamuzi yalishapitishwa hata akijadili mwaka mzima ubabe ushafanyika

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
mh naibu wazir wa nishat na madini anaongea live statv kuhusiana na suala la ges mtwara pamoja na wachambuz wengine, anaxema ges inaletwa daslam il kuendesha uchumi wa nchi, only 14pecent to dsm, gvt shares 60percent, fuatilia

Korosho yenyewe mmeshidwa kuwasaidia, ss mnawanyanganya gesi. Na bomba lenyewe mmefanya ufisadi.
 
Kwa kuwa mikataba ya ujenzi ni siri sana na kwa kuwa tuna tetesi kwamba bei ambao wakandarasi wametoa kwa ajili ya ujenzi wa bomba na uchimbaji wa gesi ni kubwa kupita kiasi kwa lengo la kuwanufaisha wawekezaki na viongozi waliosaini mkataba. Waziri anasemaje kuhusu hili? Je wanancho wana haki ya kuona mikataba hii? Kama ndiyo je wananchi wafanyeje ili kuweza kuona mikataba hii?
 
wa andae tu lakini suala la UMEME-gesi kufuliwa MTWARA lipo pale pale,Kwa nini gesi isogee BAGAMOYO?,MTWARA kuna Tatizo gani?,VIWANDA viendeswavyo kwa nishati itokanayo na gesi ya MTWARA vijengwe MTWARA.acheni propaganda kwenye mambo ya msingi.
USHAURI: wana KUSINI tuwe ngangari hao magamba ndio zao wanatafuta njia ya kuwalainisha kwa kutoa virasimu vyao uchwara ili Wachote gesi yenu.rasimu watoe wasitoe GESI Ifue umeme MTWARA.tusi laghaiwe na mafisadi wa jani la tumbaku hawana jema hao lao ni 10%.
 
Maamuzi yalishapitishwa hata akijadili mwaka mzima ubabe ushafanyika

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums

Kwa nini Serikali ya CCM hakutengeneza sera ya gesi kwa zaidi ya miaka 10 tangu waanze kuchimba gesi kule Songosongo?

Wanajenga Bomba la gesi lakini wataalaam hawahusishwi? Wakati wanajenga Bomba la Songas tuliwaambia waweke Bomba mbili ( double) na pia ukubwa wa kutosha hili halikufanyika sijui design ya bomba jipya limezingatia uwezo wa kusafirisha gesi ya kutosha plus contingency? Pomoja na Hilo naipongeza team ya Muhungo kwani kwa muda mfupi tu wamechangamka na kuandaa sera ya gesi.
 
Kauli ya Waziri na Naibu waziri zinapingana...Waziri amesema 14% tu ndo ya gesi iliyopo Mtwara na 76% ipo eneo la bahari kimataifa...na Simbachawene ametaja baadhi ya maeneo kama Sudi bay, mikindani bay n.k yatajenngwa viwanda vya mbolea kutumia 76% ya gesi....hilo eneo la kimataifa tuna mamlaka nalo? Nachanganyikiwa kabisa......ila Simbachawene amekuwa muungwana kwa lugha aliyoitumia katika maelezo yake.
 
Kumbuka simbachawene ni Mwanasiasa na Waziri wake sio mwanasiasi,ukizama ndani kabisa utagundua tunapigwa changa tu na hawa wazoefu wa majukwaa,ebu fikiria ni kiasi gani wananchi wa Merereni,Nyamongo,Geita,Bulyaghulu,Kahama,Nyalugusu,Tanga,etc wamenufaika na hyo madini? Ukisoma mikataba yao inasema kabisa kuwa mwekezaji Lazima aboreshe eneo husika,hasa huduma za jamii,Hospital,skuls,na barabara,ila mtu anamaliza miaka20 bila kufanya lolote nawanakabidhi mashimo tupu,Hili group la watu Laki5 linalofaida hii nchi kuna siku walahi mtasaga meno
 
"Tutasaga meno" ww si Mtziiiiii
 
Kuna swali moja la msingi ameshindwa kulijibu, katoa bla blaa tu... Kaulizwa, kulikuwa na ishu ya southern corridor hadi leo hakuna kilichotekelea, suala hili limebaki kwenye makabrasha tu hadi, sasa hili la sasa kuwa mtwara watafaidika na gesi baada ya kuwa ishafoka Dar, kuna kitu gani kitakachowaaminisha wananchi wa huko kuwa kuna kufaidi gesi ile na haitabaki kwenye makbrasha? Mwenye jibu asaidie hapa..
 
"Tutasaga meno" ww si Mtziiiiii

Nimewalenga wale watu laki5,Dar es salaam wanaweza kuwa wapo laki2 tu the rest wako mikoa mbali mbali(hao laki3)na maamuzi yao kila kitu kiletwe Dar then ndo wanaanza kuwekeana kwenye AC zao,waendelee kuomba mikoa ya kanda ya ziwa isijitambua"note"Maoni haya ni kwa mujibu wa halmashuri ya kichwa changu
 
Swali
1. ni kwa kiasi gani wananchi wamehusishwa katika mchakato wa uvunaji wa gesi?
2. Huoni kulazimisha kuleta gesi dar bila idhini ya wananchi ni kutengeneza tatizo jingine na kukuza mpasuko kati ya wananchi na serikali?
3. Angalau kwa kifupi unaweza kutupa maelezo kuhusu mchakato wa tenda juu ya mradi huu wa utafutaji na ujenzi wa bomba la gesi
4. Tueleze hivi kila kinachopatikana mikoani kinachohamishika ni lazima kibebwe hadi dar? Kuna ubaya gani viwanda vikijengwa Mtwara? Huoni kuhamisha gesi kuja Dar liocha ya kuwa ni gharama kubwa lakini unainyima Mtwara sifa ya kipekee ya kuvutia uwekezaji wa viwanda?
5. Unazungumziaje juu ya kupaa kwa gharama za ujenzi kwani miradi kama hii ipo pakistan na ujenzi wa mile zaidi ya 700 upana inch 42 kwa 1.2bil usd wakati huku kwetu ni km 526 upana inch 36 mpaka 24 bei moja wakati mjenzi mmoja?
6. Ni kiasi gani tunatakiwa kulipa kama riba kwa mujibu wa mkataba? Na asilimia ngapi ya faida itarudi kwenye serikali za mitaa?
 
Hapa kama sera hamna tunakimbilia wapi? Hau mapercent ya wakubwa? Mtwarwa komaeni mpaka kieleweke
 
Kama sera ya gas asilia HAIPO, kulikuwa na uharaka gani wa kuanza kuchimba hiyo gas ya Mtwara na kujenga bomba la kusafirisha gas hadi Dar es Salaam.

This sounds like TO PUT THE CART BEFORE THE HORSE.

Kweli nchi hii haikosi maajabu.
 
Back
Top Bottom