Simba yaifuata Yanga fainali ASFC

Simba yaifuata Yanga fainali ASFC

TheGreatASA

JF-Expert Member
Joined
Jun 26, 2014
Posts
302
Reaction score
393
BAO la jioni dakika ya 87 la Luis Miquissone dhidi ya Azam limeifanya Simba iwafuate watani zao Yanga kwenye fainali ya Kombe la Azam Sports Federation (ASFC) iliyopangwa kuchezwa mwezi Julai mkoani Kigoma.

Mechi hiyo ilianza kwa kasi, nguvu na mashambulizi ya kupokezana kwa timu zote mbili katika kipindi cha kwanza licha ya kwamba hakuna timu iliyopata bao ndani ya dakika 45 za kwanza.

Daniel Amoah wa Azam alioneshwa kadi ya njano dakika ya 14, Baada ya kumchezea rafu Luis Miquissone wa Simba katika mchezo huo uliokuwa na faulo nyingi kutokana na timu hizo kuonekana kukamiana.

Kipindi cha pili kilianza kwa Simba kufanya mabadiliko ya kiufundi kwa kumtoa kiungo Mzamiru Yassin na nafasi yake kuchukuliwa na mshambuliaji Meddie Kagere aliyeingia kuipa uhsi timu hiyo eneo la mbele.

Simba waliendelea kuingiza washambuliaji kwa kumtoa Rally Bwalya dakika ya 60 na nafasi yake kuchukuliwa na Benard Morrison ambaye wakati anaingia shangwe zilijaa uwanjani hapo.

Azam walifanya mabadiliko ya kwanza dakika ya 66 kwa kumtoa Ayoub Lyanga na kuingia Ismail Kader eneo la winga wa kushoto.
Mechi hiyo iliyotawaliwa na nguvu iliendelea kupigwa kibabe kwa timu zote mbili kutafuta bao lakini hadi dakika ya 80, ngoma ilikuwa bila bila.

Dakika ya 32, Azam Iliad ya mabadiliko mengine kwa kumtoa Salum Abubakar ‘SureBoy’ na nafasi yake kuchukuliwa na Never Tigere.
Dakika ya 87 Simba walipata bao la kwanza kupitia kwa Luis Miquissone aliyeanzishiwa na kupiga shuti harakaharaka mpira wa faulo baada ya Morrison kufanyiwa madhambi.

Bao hilo lilizua taharuki kwa wachezaji wa Azam na kumzonga refa lakini hiyo haikubadili msimamo huo na kuendeleza kabumbu hadi dakika 90 zinamalizika.
......


luis-pic-data.jpg
full-pic.jpg
f-pic-data.jpg
 
Kwani yanga na simba kuna soccer la maana?

Tunasubiria
-mateke,
- butuabutua,
-vikumbo
-ubabe,
-kadi za ajabuajabu,
-offside za kubumba na za kufumbia macho

Ilimradi ushenzi tu. Kuanzia marefa haswahaswa.
 
Back
Top Bottom