Mohamed Ismail
JF-Expert Member
- Mar 16, 2014
- 227
- 246
SIMBA WA VITA MUGABE
Ardhi imejaa taharuki na aibu huku mbingu tayari zimeishafunguka kwa furaha na bashasha za kupokea roho ya jemedari Mugabe simba wa vita.
Mlimwengu mimi nimeshindwa kukaa kimya kuhusu huu msiba mkubwa wa Afrika.
Najua Mugabe huko ulipo unajiuliza kwanini haya hayakusemwa wakati upo hai lakini moyo wako na dhamira yako kubwa ilikiwa siku ukiwa haupo watu watambue mchango wako. Na huku kwetu mpaka uage dunia ndio tunakuita shujaa.
Robert Mugabe alizaliwa 24/02/1924 huko Kutama Zimbabwe katika familia ya kawaida.
Alipata nafasi ya kupata elimu na baada ya kuhitimu alifanya kazi kama mwalimu. Na alifundisha kwa muda mrefu bila kujihusisha na masuala ya siasa. Baadae akapata nafasi ya kwenda kusoma South Africa na kupata shahada yake ya kwanza ya historia na mambo ya fasihi. Huko aliweza kukutana na vijana wenzake ambao walikuwa masomoni lakini wana harakati za kujikomboa kupata uhuru. Alivyorudi kutoka masomoni akaendelea na kufundisha huku akijihusisha na siasa kidogo. Baadae alipata nafasi ya kwenda kufundisha Ghana ambapo yeye alipapenda kwa sababu ilikuwa ni kujifunza ni namna gani nchi inajiendesha ikiwa imeishapata uhuru. Kwa wakati huo Ghana ilikuwa tayari imeishapata uhuru wake chini ya Nkwame Nkrumah. Mugabe katika maisha yake yote aliamini kwenye Ujamaa hivyo Nkwame Nkrumah alikuwa role model wake.
Wakati yupo Ghana alimpata mchumba wake wa kwanza ambaye jina lake ni Sally Hayfron Mugabe alimpenda sana huyu mwanamke kwa sababu naye alikuwa na damu ya kimapinduzi hivyo aliamini katika harakati zake za kupigania uhuru angekuwa msaada kwake. Siyo vijana wa sasahivi wanaangalia sura na umbo huku wakijidanganya akili watatumia zao. Mugabe baada ya kumpata mchumba aliona siyo vibaya kumpeleka nyumbani kwao na ili waweze kufunga ndoa yao takatifu. Walifunga ndoa kanisani lakini hakuweza kurudi tena Ghana ilibidi aanze harakati za kupigania uhuru nchini kwake. Tayari vyama vingi vilikuwa vimeishaanzishwa na watu walikuwa wana imani naye kutokana na utendaji wake wa kazi pamoja na dhamira kubwa aliyokuwa anaionyesha ya kupata uhuru. Mke wake Sally naye alikuwa mwanaharakati aliwahi kusema kuwa Queen Elizabeth wa pili ataenda kuzimu ( Queen Elizabeth ii must go to hell) na alivyoitwa alikubali kusema hivyo bila kusita hivyo basi alikuwa mpambanaji.
Mugabe alikuwa mpiganaji na kinara katika kuhakikisha Zimbabwe wanapata uhuru. Wakoloni walijaribu mara nyingi kumfanyia assasination lakini walifeli. Kama unavyojua siku zote wenye akili ndogo hukimbilia kumdhuru anayedai haki yake badala ya kumpatia haki yake. Waliweza kumkamata pamoja na viongozi wengine ambao walikuwa wakifanya harakati za kudai uhuru. Mugabe alikaa jela kuanzia mwaka 1964 hadi 1975. Kitu ambacho hakuwahi kusahau ni suala la kufiwa mwanae wa kwanza wa kiume wakati akiwa kifungoni. Aliomba apewe nafasi ya kumzika mwanae na kumuona mkewe lakini walikataa kata kata kumpa ruhusa.
Mugabe baada ya kumpata mtoto wake huyo wa kwanza alimpatia jina la Mhamodzenyika ni jina la kishona ambalo maana yake ni nchi inayotaabika (suffering country) kwenye jina tu tunaona jinsi Mugabe alivyokuwa anaumia kuona watu wanapata taabu katika nchi yao kwa manyanyaso na uonevu kutoka kwa watu weupe. Hayo ni mapenzi makubwa kwa nchi yake maana anapomuona mwanaye anaona jinsi nchi inavyoumia. Ni kama Rais wa nchi fulani alivyotangaza kuwa wafanyakazi wa serikali waweke picha za watoto wao maofisini ili wanapotenda maovu roho zao ziwasute.
Mugabe kukaa gerezani ilikuwa changamoto lakini alibadili changamoto kuwa fursa. Kipindi chote akiwa gerezani alitumia muda wake kuwafundisha watu kwa kuwapa elimu vilevile ilikuwa muda wake wa mzuri wa kujisomea. Miaka yote aliyokaa gerezani alipata Masters of Economics, Bachelor of Administration na Degree 2 za sheria kwenye chuo cha University of London. Wakati huku kwetu watu wanashindwa kusoma wakisingizia uchumi na mambo mengi. Kupitia uthubutu wa Mugabe tunaweza kujifunza vitu vingi.
Alivyoachiwa gerezani alikatazwa kujihusisha na mambo ya kisiasa bila hivyo angekamatwa na kuendelea kusota rumande. Lakini nia na dhamira yake ilikuwa bado ni kuhakikisha Wazimbabwe wanajitawala. Alivyotoka huko alitafuta sehemu ya kujificha na baadae akaenda msumbiji huko alikutana na Samora Machel ambaye alimpatia hifadhi kwa kumpatia nyumba ya kuishi pamoja na kumpa msaada wa mawazo ya kuikomboa Zimbabwe. Chama chao walianzisha movement ambapo ilikuwa ni vita ya msituni (Guerilla war) kuanzia 1975-1979 . Hii vita walikuwa wanachoma mashamba ya wazungu na kuharibu mali zao na watu walikuwa wanauwawa . Mugabe hakuishia hapo alikuja Tanzania akakutana na Gwiji wa siasa Hayati Mwl Julius Nyerere naye alimpatia msaada wa kutosha na kama mnavyojua Mwl Nyerere alitoa mchango mkubwa wa upatikanaji wa uhuru kwa mataifa ya Afrika ambayo yalichelewa kupata. Mugabe aliamini sana kwenye ujamaa hivyo alitembelea nchi nyingi zenye falsafa ya ujamaa kama Cuba akakutana na Fidel Castro ambaye naye kwa sasa ni marehemu.
Na nchi nyingi za ujamaa zilitoa msaada mkubwa kama China waliisaidia sana Zimbabwe.
Mambo yalivyozidi kuwa magumu kwa Zimbabwe nchi haikaliki waliamua kuitisha mkutano Uingereza ili wakae mezani watoe tofauti zao. Mugabe hakuwa tayari kwenye kukaa nao meza moja. Lakini Samora Machel alimuambia usipoenda na mimi ninasimamisha msaada wangu kwako. Hivyo Mugabe ilimbidi apande mwewe aende ughaibuni kwa shingo upande kutokana na shinikizo la Samora Machel. Kikao kilikaa ni namna gani watakavyoongoza nchi bila vurugu pamona na ugawanyaji wa ardhi kati ya wazawa na wazungu (Lancaster House Agreement) kwenye kikao hicho alikuwepo Nkomo ambaye naye alikuwa mzimbabwe lakini Mugabe alimuona kama Kibaraka cha wazungu. Baada ya kikao walirudi zimbabwe na kufanya uchaguzi ambapo chama cha Mugabe ZANU-PF kilijinyakulia kura nyingi ambapo Mugabe akachaguliwa kuwa Waziri mkuu wa kwanza mnamo 1980 kwa kipindi hicho cheo cha Urais kilikuwa hakina mamlaka yeyote mbele ya Waziri Mkuu. Mugabe aliamini ubaya haulipwi kwa ubaya hakuwafukuza wazungu na bado wengine aliwachagua kuwa mawaziri katika baraza lake la mawaziri.
Mwaka 1987 katiba ilipitiwa upya akawa Rais hivyo mke wake Sally akawa first lady kwa kwanza ingawa wazimbabwe walikuwa hawamkubali sana kwa sababu hakuwa mzawa lakini ilibidi wakubaliane na hali ndio mwenyewe kashaamua .Walibahatika kupata watoto wawili. Bahati mbaya mwaka 1991 Sally alifariki kwa ugonjwa wa ini. Maisha yaliendelea ikabidi amuoe mwanamke mwingine ambaye ni Grace Marufu .Walifunga tena ndoa ya kanisani mwaka 1996 na sherehe ilikuwa kubwa. Na wao walibahatika kupata mtoto mmoja kwa ujumla ameacha watoto watatu pamoja na wawili wa mke wa kwanza.
Urais wake uliweza kudumu hadi 2017 baada ya nafasi yake kuchukuliwa na Emmerson Mnangagwa ambaye alikuwa makamu wake.
Leo Mugabe ametangulia mbele ya haki anaenda kukutana na waasisi wengine ambao walitumikia nchi zao katika maisha yao yote.
Swali linabaki kwetu kuwa kabla ya kulaumu nchi yako umeifanyia nini? . Mugabe hakuwahi kuwa muoga na ni Rais ambaye aliamini katika elimu na amewafanyia makubwa wazimbabwe.
Alikuwa ni simba hakutishwa na vitisho vya mataifa ya nje. Alisimamia kile anachokiamini , alikataa kata kata masuala ya ndoa ya jinsia moja na aliona kama ni ushetani uliopitiliza. Alikuwa tayari kupoteza misaada ya mataifa ya nje kama IMF pamoja na World Bank kwa masharti ambayo anaona siyo tija kwa nchi yake.
Na hili tunaliona kwa Rais wetu Dr John Magufuli hayupo tayari kusaini mikataba ambayo haina tija kwa nchi yetu.
Huu ni msiba mkubwa kwa Afrika simba kaondoka lakini katuachia alama mioyoni na mfano wa namna gani kijana wa Afrika anapaswa kuipambania nchi yake.
Kuna picha ambayo wazungu waliitengeneza tumuone ni mtu wa ajabu lakini dhamira yake ni kuona Afrika tunajitegemea ( Pan- Afrikanisim )
Rest in peace true son of Africa.
Mlimwengu mimi ngoja niishie hapa kwa leo ni yuleyule uliyeambiwa kuwa usipofunzwa na mama yako atakufunza.
Imeandikwa na
MOHAMED ISMAIL RWABUKOBA
0761070361
mohammedismail613@gmail.com
#mlimwengumimi
#jicholamlimwengu