Simba vs Tiger

Simba vs Tiger

LwandaMagere

JF-Expert Member
Joined
Mar 15, 2020
Posts
264
Reaction score
2,489
Hello,habari za majukumu wadau,bila shaka mtakuwa mko vyema na mnaendelea kuchukua hatua na tahadhari dhidi ya hili gonjwa dharimu la Covid-19 linalosababishwa na virus hatari wa corona,Mungu awabariki sana!.

Niende moja kwa moja kwenye mada.
Kuna mjadala mahali fulani nimekutana nao kuhusu mnyama SIMBA na TIGER (Chui milia).

Kiukweli kama mnavyofahamu mijadala mizito mara nyingi huwa ina vuta nkuvute,kulingana na tafiti mbalimbali pamoja na Historia kadha wa kadha!,sasa kuna wengine waliosema ya kwamba SIMBA ni hatari zaidi ya Tiger na kuna wengine waliosema Tiger ni hatari zaidi ya Simba,na huo uhatari wao ni pale wanapokutana wao kwa wao.

Wapo waliosema SIMBA kwa uwezo wa nguvu,uwindaji,mapigano basi akikutana na Tiger atapokea kipondo kikali,lakini pia wapo vilevile waliosema kwamba Tiger kwa uwezo,minguvu,uwindaji na mapigano basi akikutana na Simba atampiga mpaka achakae kabisa,na si kuchakaa tu bali pia kuua kabisa.

Mtazamo wako wewe ni upi hapa,hebu lete facts za uhalisia,kiroho na kimwili pia unaweza kuhusisha!!

Tulia hivyo hivyo dawa ikuingie..
 
Kwa mimi naona tiger is better

Huyu tiger anauwezo wa kuingia kwenye mto na kumchukua mamba akiwa mle mle kwenye maji jambo ambalo sio rahisi ukizingatia na kwamba nguvu ya mamba ni maji lakini si kwa chui

Halafu hata skills za uwindaji chui yuko vizuri zaidi, kama silaha basi naweza kumfananisha na AK47 wakati simba namfananisha na gobole

Action za chui ni noma hadi ndege anawinda, yani anajiviringa juu huko huko aliko ndege kisha anamdaka kwa mikono kama mtu

Simba dume ndo kabisa hata kuwinda halijui lenyewe kula kulala tu kazi zote limemuachia shemu
 
Kama watakua na umri sawa tiger 🐅 will win ...judging by the size tiger is more heavy than lion (200kg vs 235kg)...AGGRESSIVENESS tiger is more aggressive than lion ... so if same age ... same sex lion stands no chance
 
Kwa mimi naona tiger is better

Huyu tiger anauwezo wa kuingia kwenye mto na kumchukua mamba akiwa mle mle kwenye maji jambo ambalo sio rahisi ukizingatia na kwamba nguvu ya mamba ni maji lakini si kwa chui

Halafu hata skills za uwindaji chui yuko vizuri zaidi, kama silaha basi naweza kumfananisha na AK47 wakati simba namfananisha na gobole

Action za chui ni noma hadi ndege anawinda, yani anajiviringa juu huko huko aliko ndege kisha anamdaka kwa mikono kama mtu

Simba dume ndo kabisa hata kuwinda halijui lenyewe kula kulala tu kazi zote limemuachia shemu

Sidhani kama uko sahihi huyo unaemsema wewe anaitwa jaguar 🐆 anapatikana marekani ya kusini huyo unaemuita mamba ni alligator 🐊 ... tiger kwa asili anapatikana Asia ... na kwa taarifa tu hakuna mnyama anaeweza kufanya huo upumbavu wa kuwinda mamba mtoni ( the strongest bite on earth 🌍 ) Hakuna mnyama anaeweza kuwinda hawa jamaa nile crocodile au salt crocodile labda alligator they’re more like lizards than mazafaka crocs
 
Tiger ana uwezo wa kupigana kwa kusimamia miguu ya nyuma wakati anatoa kichapo kwa adui.

Ni mnyama ambaye ni mwepesi mno na anashambulia kwa kasi kuliko simba!

Ana uwezo wa kujitupa na kujigeuza upande wowote wakati wa mapigano kwa kasi na kwa nguvu zote.

Bahati mbaya anachoka haraka tofauti na simba!

Simba anaweza asiwe na ufanisi wa mbinu za kupigana kama tiger lakini ana ujasiri na hachoki. Anapigana mpaka tone la mwisho la damu hata apigwe vipi hakimbii.

Tigers wana nguvu na ufanisi lakini ni wazembe. Anashambulia kwa kasi lakini akichoka anakimbia pambano!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Simba sio mkubwa kama Tiger

Kiasili Tiger wanapatikana Asia na Ulaya Mashariki ambayo ni Russia na Tiger wakubwa kbsa wanapatikana Siberia
Tofauti na wa india na kadhalika

Kwenye sifa za kuwinda

Simba ndio paka ambao wanawinda kwa ushirikiano tofauti na jamii nyingine ya paka

Kwenye kupiga simba Tiger wa umri mmoja

Kwanini simba atashinda na Tiger atashindwa

Simba anapigana kwa kutumia mguu mmoja wa mbele na kusimama kwa mitatu iliyobaki wakati Tiger yeye anapigana kwa miwili kwa wakati mmoja na miwili ya nyuma anasimamia
Simba kwenye mapigano anamoyo wakupigana mpaka kifo atakama anajua anashindwa lakini Tiger hanauwezo huo wakupigana kwa muda mrefu

Simba dume ana mane nywele za pale shingoni ile nisilaha tosha kwake inamkinga zidi ya Adui wakati Tiger hana hizo

Simba kwa kimkakati anauwezo mkubwa sana wakumpiga Tiger kuliko mikakati ya Tiger kwakuwa Tiger sio mvumilivu kama simba
Ukitaka kujua Roho ngumu ya simba ..Dume moja la simba lipo tayari kupigana na madume manne akijua kbsa hanauwezo ila analinda Heshima yake mpaka umauti unamkuta ,kwa hiyo simba amepewa sifa za ziada ambazo nitofauti na paka wengine

Pia tambua simba anaona usiku mara nane ya binamu kwa usiku

Tambua kuwa simba Dume anapounguruma sauti yake inasikika mile 8

Tambua pia simba nipaka wanaoishi kaya ambapo wapo mashangazi mabibi mama na watoto mabinamu na Baba zao na ni mwiko mwanaume kumpanda Mama au Dada yake tofauti na paka wengine

Pia tambua simba ndio paka pekee ambao wakiamua leo wale mnyama wanayemtaka wanafanya hivyo mfano tembo twiga nk

Simba jike watoto wao wanaruhusiwa kunyonya kwa mama yoyote wakaya yao na mtoto analindwa na kina mama wote atakama sio wake

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kabla ya kuweka mjadala ungetoa kwanza elimu kuhusu utofauti kati ya Tiger yule anayepatikana bara la Asia na Nchi ya Urusi na hawa chui wetu ambao wao wanaitwa Leopards na wanapatikana huku Africa na baadhi ya sehemu nyingine.

Maana naamini wengi kibongobongo wanashindwa kujua tofauti zao. Tukiacha hayo unachopaswa kujua ni kuwa mafanikio ya Simba kwa asilimia kubwa yanatokana na ushirikiano, katika familia ya wanyama aina ya paka (changanya paka wote hapa) simba ndiye anayeongoza kwa ushirikiano na wenzake katika mawindo wakati Tiger yeye anapambana mwenyewe, na ana size kubwa, uzito wa kutosha kumzidi simba.

Nikiangalia hizo sababu naona kama Simba atachapwa kipigo cha mbwa mwizi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sidhani kama uko sahihi huyo unaemsema wewe anaitwa jaguar anapatikana marekani ya kusini huyo unaemuita mamba ni alligator ... tiger kwa asili anapatikana Asia ... na kwa taarifa tu hakuna mnyama anaeweza kufanya huo upumbavu wa kuwinda mamba mtoni ( the strongest bite on earth ) Hakuna mnyama anaeweza kuwinda hawa jamaa nile crocodile au salt crocodile labda alligator they’re more like lizards than mazafaka crocs
Upo sahihi ndugu. Ni juzi tu niliona jaguar akiwinda majini kwa kumkaba nyuma ya shingo alligator.

Katika battle nyingi kati ya tiger na lion kiutafiti tiger anashinda au almost ku-win hayo mapigano.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
huyo unaemuita mamba ni alligator 🐊

Sio sawa mkuu, huyo sio Alligator bali anaitwa Caiman crocodile, hawa ni aina ya mamba waliopo America ya kusini ni wadogo kuliko Alligators au Nile crocodiles na huliwa sana na Jaguar, Jaguar ni mkubwa kidogo kuliko chui lakini anafanana sana na chui wa huku Africa.
 
Simba sio mkubwa kama Tiger

Kiasili Tiger wanapatikana Asia na Ulaya Mashariki ambayo ni Russia na Tiger wakubwa kbsa wanapatikana Siberia
Tofauti na wa india na kadhalika

Kwenye sifa za kuwinda

Simba ndio paka ambao wanawinda kwa ushirikiano tofauti na jamii nyingine ya paka

Kwenye kupiga simba Tiger wa umri mmoja

Kwanini simba atashinda na Tiger atashindwa

Simba anapigana kwa kutumia mguu mmoja wa mbele na kusimama kwa mitatu iliyobaki wakati Tiger yeye anapigana kwa miwili kwa wakati mmoja na miwili ya nyuma anasimamia
Simba kwenye mapigano anamoyo wakupigana mpaka kifo atakama anajua anashindwa lakini Tiger hanauwezo huo wakupigana kwa muda mrefu

Simba dume ana mane nywele za pale shingoni ile nisilaha tosha kwake inamkinga zidi ya Adui wakati Tiger hana hizo

Simba kwa kimkakati anauwezo mkubwa sana wakumpiga Tiger kuliko mikakati ya Tiger kwakuwa Tiger sio mvumilivu kama simba
Ukitaka kujua Roho ngumu ya simba ..Dume moja la simba lipo tayari kupigana na madume manne akijua kbsa hanauwezo ila analinda Heshima yake mpaka umauti unamkuta ,kwa hiyo simba amepewa sifa za ziada ambazo nitofauti na paka wengine

Pia tambua simba anaona usiku mara nane ya binamu kwa usiku

Tambua kuwa simba Dume anapounguruma sauti yake inasikika mile 8

Tambua pia simba nipaka wanaoishi kaya ambapo wapo mashangazi mabibi mama na watoto mabinamu na Baba zao na ni mwiko mwanaume kumpanda Mama au Dada yake tofauti na paka wengine

Pia tambua simba ndio paka pekee ambao wakiamua leo wale mnyama wanayemtaka wanafanya hivyo mfano tembo twiga nk

Simba jike watoto wao wanaruhusiwa kunyonya kwa mama yoyote wakaya yao na mtoto analindwa na kina mama wote atakama sio wake

Sent using Jamii Forums mobile app
Nimependa maelezo haya. Yamechambua vizuri nguvu na udhaifu wa kila mmoja katika aina hizi za paka. Ni kweli Simba hana mzaha linapokuja suala la kupambana. Huwezi ukamtoa nduki kama unavyoweza kufanya kwa Tiger and the like. Utamuua akijilinda huku akitafuta uwezekano wa kukumaliza na wewe

Ila nina swali moja mkuu. Umesema Simba ndio mnyama wa aina ya paka anaewinda kwa pamoja. Je mbwa mwitu hawako kwenye kundi hili maana wao haswaa ndio wawindaji kwa group
 
Hello,habari za majukumu wadau,bila shaka mtakuwa mko vyema na mnaendelea kuchukua hatua na tahadhari dhidi ya hili gonjwa dharimu la Covid-19 linalosababishwa na virus hatari wa corona,Mungu awabariki sana!.

Niende moja kwa moja kwenye mada.
Kuna mjadala mahali fulani nimekutana nao kuhusu mnyama SIMBA na TIGER (Chui milia).

Kiukweli kama mnavyofahamu mijadala mizito mara nyingi huwa ina vuta nkuvute,kulingana na tafiti mbalimbali pamoja na Historia kadha wa kadha!,sasa kuna wengine waliosema ya kwamba SIMBA ni hatari zaidi ya Tiger na kuna wengine waliosema Tiger ni hatari zaidi ya Simba,na huo uhatari wao ni pale wanapokutana wao kwa wao.

Wapo waliosema SIMBA kwa uwezo wa nguvu,uwindaji,mapigano basi akikutana na Tiger atapokea kipondo kikali,lakini pia wapo vilevile waliosema kwamba Tiger kwa uwezo,minguvu,uwindaji na mapigano basi akikutana na Simba atampiga mpaka achakae kabisa,na si kuchakaa tu bali pia kuua kabisa.

Mtazamo wako wewe ni upi hapa,hebu lete facts za uhalisia,kiroho na kimwili pia unaweza kuhusisha!!

Tulia hivyo hivyo dawa ikuingie..

Mkuu, Simba dume na Tiger dume wakipambana Simba ataipata, Tiger ni mnyama anayeishi Solitary kama chui anavyoishi (yaani ni mnyama anayeishi peke yake), ukiwakuta wawili basi watakuwa ni jike na dume na jike amemfuata dume ili "apigwe mashine" baada ya hapo kila mmoja utafuta ustaarabu wake.

Katika kuwinda Tiger huwinda peke yake, Tiger mmoja peke yake anaweza kumuua AUGUR (aina ya nyati waliopo India) hii ni tofauti na Simba ili aue nyati wanatakiwa wawepo sio chini ya simba wawili. Tiger anayo kasi kubwa, nguvu na uzito kuliko simba na anapowinda asilimia kubwa ni lazima apate tofauti na simba akiwinda peke yake, kifupi Tiger ni mpambanaji peke yake (a lone starring) tofauti na Simba ambao kwa tabia huwinda kwa kundi hasa majike, Tiger anaweza kuogelea na anapopigana na mwenzake huweza kusimama kwa kutumia miguu ya nyuma pekee na kutumia miguu ya mbele kama silaha hii ni tofauti na simba ambaye hawezi kusimama kwa miguu ya nyuma pekee, hivyo ukiwapambanisha simba na Tiger, Tiger anayo nafasi kubwa ya kumpiga simba na hasa simba jike kwani yeye hana manyoya ya kumkinga usoni (mane) kama ilivyo kwa Simba-dume.

Hitimisho langu ni hili; ninampa Tiger 70% ya Ushindi dhidi ya 30% ya ushindi wa Simba.

Japo Simba ni "Baba lao" ,🤣

NB:Tahadhari na Corona vaa barakoa😷
 
Nimependa maelezo haya. Yamechambua vizuri nguvu na udhaifu wa kila mmoja katika aina hizi za paka. Ni kweli Simba hana mzaha linapokuja suala la kupambana. Huwezi ukamtoa nduki kama unavyoweza kufanya kwa Tiger and the like. Utamuua akijilinda huku akitafuta uwezekano wa kukumaliza na wewe

Ila nina swali moja mkuu. Umesema Simba ndio mnyama wa aina ya paka anaewinda kwa pamoja. Je mbwa mwitu hawako kwenye kundi hili maana wao haswaa ndio wawindaji kwa group

Mbwa mwitu sio mnyama aina ya paka
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom