Simba vs Mbeya City: kutoka Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam

Simba vs Mbeya City: kutoka Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam

Leo humu jamvini mumetulia sana, wale jamaa wachonga droo wapo busy na kupaka vanish droo zao walizochonga. Ahsante sana mbeya city kwa kuleta heshima mitaani.
 
Waliongea sana siku walipo bahatisha kwa ndanda ya mtwara, wakasema ndio kwanza wameanza ligi, wakaanza kuufananisha uwezo wa mjomba mpoto na professional player KPAH SHERMAN!!!! Wakaanza kumfananisha winga teleza tanzania nzima SIMON MSUVA na Ramadhan singano!!!, Huo ni mwanzo tu mtakapostuka mtakuwa mmeshashuka daraja.
 
Bantu lady leo utaongea sana. hamna shida yote maisha wametuzid wameshinda wala hatutasingizia uchawi au refari. si tunakubal mpira ndo uungwana. lakini bado sana ligi na usitukane mamba kabla hujavuka mto. sisi raha yetu ni kumfunga yanga tu. nyie yanga fanyeni muwezalo ila mkija kwa simba mnakaa. mi nipo tayar simba ifungwe na team zote lakini si na yanga.

Unaonesha kweli umepagawa mkuu, mbona kile kikombe uchwara cha mapinduzi mlivyoshinda mlifurahi sana mpaka mkachanganikiwa na Yanga hamkuifunga wala hamkucheza nao. Halafu ikifungwa mechi zote si itashuka daraja mkuu au hilo halikuhusu ?
 
Huyu Kapteni wetu Simba aache kulalamika hivyo, akubali kuwa hatukustahili kushinda. Nafikiri udogo bado unamsumbua, hajajifunza!! Nimemsikia redioni analalamika kweli kuhusu refa wakati tulipewa penati tukashindwa.
Tumefungwa fairly, tumekosa penati sababu mara nyingi penati za magumashi zinaotaga mbawa.
Tulistahili kufungwa, tujipngae tena!

Wewe umeongea kimichezo, huyo kapteni wenu aliyetoa malalako kwa refarii ana lake jambo. Yaani mbele ya kupewa penalt ya bure kabisa bado anatoa malalako kwa refa!!!! Tangu nianze kuangalia mpira sijawahi kuona refa anatoa penati kama ile, ajabu ndo nimeanza kuiona jana. Ameacha kuongea ukwel kwamba timu yao ilichoka sana kuanzia dak 70 yeye analeta mambo ya kishabiki!!!!?. Huyo kapten ajitathimini kwanza je, wale wachezaji aliowasajili wana hadhi ya kuichezea simba!!
 
kwa mara ya kwanza nimelala kwa kusimama kitandani
Mkuu Amavubi, hadi muda huu Today 02:52 (tazama post #273 hapo juu) ulikuwa hujalala? Mbeya City hawajakutendea haki aisee! Mkuu Viol naye ka-post Today 04:01 (tazama post #274 hapo juu), pole pia. Tulidhani mtalala mapema, kumbe usingizi uligoma! Leo lazima msinzie huko kazini kwenu.
 
kwa mara ya kwanza nimelala kwa kusimama kitandani

Mara yako ya pili kulala wakati umesimama itakuwa mtakapo kutana na JKT ruvu ya Minziro. Ha ha ha ha ha ha ha ha mwaka huu kazi munayo watani.
 
10958196_783465445033849_3975089073627728060_n.jpg
 
Mbona tupo kama kawaida, kwanza tunatafakari kama familia kuhusu hasa kilichotokea.
Ova

Mtatafakari sana mwaka huu watani na mtakapo stuka kutoka kwenye tafakari timu itakuwa tayar imeshashuka daraja.
 
Back
Top Bottom