FT: Simba 0-1 Al Ahly | CAF CL Robo Fainali | Benjamin Mkapa Stadium | 29/03/2024

Suley2019

JF-Expert Member
Oct 7, 2019
1,817
4,566
1711656692157.png
Leo mnamo majira ya saa 3 usiku Klabu ya Tanzania Simba Sports Club itakuwa nyumbani kumenyana na klabu ya Al Ahly ya Misri katika mechi ya mkondo wa kwanza (First Leg) wa robo fainali wa Ligi ya Mabingwa Afrika.

Maandalizi ya timu zote mbili yameenda vyema, kinachosubiriwa ni mchezo rasmi leo 29/03/2024 saa tatu usiku.

Ungana nami katika uzi huu ili kupata matukio mbalimbali yatakayojiri kabla na wakati wa mchezo huo.

Karibu.


==============

Timu ya Simba inatarajia kucheza dhidi ya Al Ahly ya Misri katika Robo Fainali ya Kwanza ya Ligi ya Mabingwa Afrika kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar es Salaam, leo Machi 29, 2024

Takwimu zinaonesha hakuna mbabe mpaka sasa, kila upande umeshinda mechi Tatu, hizi ni mechi zilizopita baina ya timu hizo:

24/10/2023 Al-Ahly 1-1 Simba

20/10/2023 Simba 2-2 Egypt

09/04/2021 Al-Ahly 1-0 Simba

23/02/2021 Simba 1-0 Al-Ahly

12/02/2019 Simba 1-0 Al-Ahly

02/02/2019 Al-Ahly 5-0 Simba

29/08/1985 Al-Ahly 2-0 Simba

22/08/1985 Simba 2-1 Al-Ahly
---
1711732319853.png

Kikosi cha Simba kilichoanza
1711732428358.png

Kikosi cha Al Ahly kinachoanza

Mchezo umeanza
3' Simba wameanza wakiwa na presha ya kushambulia, wamepata kona
5' Gooooooo Al Ahly wanapata goli baada ya safi ya ulinzi ya Simba kujichanganya
11' Kasi ya Mchezo imepungua, AlAhly wanalinda lango lao muda mwingi
13' Simba Wana Kona tatu, wageni Wana Moja
16' Al Ahly wanapata Kona ya pili na ya tatu ndani ya dakika moja
21' Al Ahly wanafanya mashambulizi ya kushtukiza na yanakuwa hatari
30' Mapumziko ya dakika moja
32' Mchezo unaendelea
40' Saido anakosa nafasi ya wazi
45 ' Mapumziko, Simba wapo nyuma kwa goli 1-0.

MAPUMZIKO

Kipindi cha pili kimeanza
49' Babacar anapata kadi ya njiano kwa kucheza faulo
55' Inonga anapata kadi ya njano kwa kucheza faulo
60' Mchezo bado ni mgumu kwa Simba wanatengenesa nafasi lakini haizitumiki vizuri
70' Simba wanaendelea kumiliki mpira lakini nafasi ya kufunga bado ni ngumu
75' Mapumziko ya dakika moja kwa timu zote.
77' Saido anapat nafasi kadhaa za wazi lakini hazitumii vizuri
80' Simba wanaendelea kutengeneza nafasi lakini wanashindwa kuweka mpira wavuni
90' Zinaongezwa dakika 5
Full Time
Sim st.png
 
Leo mnamo majira ya saa 3 usiku Klabu ya Tanzania Simba Sports Club itakuwa nyumbani kumenyana na klabu ya Al Ahly ya Misri katika mechi ya mkondo wa kwanza wa robo fainali wa Ligi ya Mabingwa Afrika.

Mpaka sasa maandalizi ya timu zote mbili yameenda vyema, kinachosubiriwa ni mchezo rasmi kesho 28/03/2024.

Ungana nami katika uzi huu ili kupata matukio mbalimbali yatakayojiri kabla na wakati wa mchezo huo.

Nini mtazamo wako kuhusu mchezo huo?
Mkuu una haraka sana. Rekebisha hiyo paragraph ya 2. Mchezo ni leo Ijumaa tarehe 29. Imaonekana hii umeiandaa jana ukasubiri ifike saa 6:01 usiku uitupie.
 
Back
Top Bottom