Simba bado imekuwa na wakati mgumu kwenye uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Leo katika mechi yake ya Ngao ya Hisani ikiwa ni mechi maalum ya ufunguzi wa michuano ya Ligi Kuu Tanzania Bara, inayocheza na Azam FC imeendelea kutoa matumaini finyu kwa mashabiki wake.
Ikiwa ni dakika ya pili tu, washaruhusu goli la kwanza na kukoswa koswa goli la pili katika dakika ya sita. Kwa ninavyoona Simba wamekuwa na tatizo kubwa katika safu ya ulinzi. Mabeki hawana umakini na wanashindwa kujipanga vizuri kucheza mipira ya kona. Acha tuendelee kufuatilia mchezo huu.