Simba tujitathimini huu ni udhalilishaji uliokidhiri...

Simba tujitathimini huu ni udhalilishaji uliokidhiri...

Nilisema mimi,, hatuna timu ya kuifunga Yanga hii hamkunielewa na bado kuna kipigo kingine cha haja kutoka kwa Azam kinatusubiri,, timu imejaa mafaza kibao huku madogo wenye uwezo wapo hawaaminiki kupangwa,,
 
Mkono unauma sana, bora hata ingekuwa 2-1
Mkono kweli
Manura kadaka kwa sababu viongozi wamelazimisha
 
Hongereni sana Yanga kwa ushindi mnono na poleni Simba kwa kipigo cha mbwa mwizi. Kiukweli kabisa Yanga walistahili ushindi.

Simba ni kama kenge tu mpake atoke damu masikioni ndio asikie. Hizi goli 5 ndio alikosa Al ahly hapa kwa Mkapa kwa kukosa kwao umakini lakini viongozi wa Smba na benchi lao la ufundi hawakuliona hili na kulifanyia kazi badala yake wakawa wanajisifu kupata sare na Al Ahly hapa na kujiona wakubwa. Ilikuwa na swala la muda tu madhaifu ya Simba kudhihirika wazi.

Makosa ya haraka haraka niliyoyaona leo:-
1. Unampangaje Manula kwenye mechi yenye "tension" kubwa ambaye hana match fitness mbele ya Ali Salum ambaye amecheza mechi kubwa mfululizo. Pamoja na makosa ya mabeki lakini Manula angekuwa na match fitness angepunguza idadi ya magoli. Kwa yoyote aliyelazimisha Manula acheze leo awe kiongozi au kocha mwenyewe na benchi la ke ufundi anastahili lawama zote kwa kipigo cha mbwa mwizi alichopata Simba. Na kwa wasiofahamu Manula kwa siku za karibuni huwa anakosa utulivu kwenye mechi za derby. Achilia mbali ule uwoga wake kwa Aziz Ki tangu amtungue akiwa Asec Mimosa. Mechi ya leo ilikuwa inamhusu Ally Salim.
2. Timu nzima haina stamina wala kasi. Mliambiwa hapa mapema mrudisheni Zrane nyie mkangáninia huyo Hatekigamna. Kimojawapo kilichoifungisha Simba leo niliishawambiwa hapa mara nyingi kuwa Simba ikifika dakika ya 60/65 inakata moto lakini hilo halikufanyiwa kazi.
3. Timu haina kiungo asili mkabaji. Hili kosa lilifanyika wakati wa usajili lakini haipaswi hata kidogo kuwa kisingizio kwa timu yenye benchi la ufundi lenye weledi. Kwa hili benchi zima la ufundi linahusika kwa sababu walipaswa wajue mapema haya madhaifu halafu watumie weledi wao kuitengeneza timu nzima iweze kujilinda bila ya kuwa na kiungo asili mkabaji. Nilisema hapa jamvini mara nyingi kuwa benchi la ufundi lina mapungufu katika namna ya kujilinda ndio maana Simba mwaka huu "clean sheets" zimekuwa adimu za kutafuta na tochi licha ya kuwa na mabeki wakati wawili wenye uwezo mkubwa.
4. Namba 10 pale Simba ni tatizo kubwa sana lakini haionekani kirahisi mpaka mtu aangalie mpira akiwa ametulia na awe na uelewa mkubwa sana wa mambo ya mpira. Makosa ya namba 10 ndio yanapelekea viungo na mabeki kubeba mzigo wote. Kuendelea kumtumia Saidoo kwa dakika nyingi tena kila mechi ukizingatia umri wake ni mkubwa basi shida ndio huanzia hapo. Lakini hili mashabiki maandazi hawalioni kiasi ukimzungumiza Saidoo hapa unazodolewa kwa sababu tu utakuta kabahatisha labda goli, assist au kona iliyozaa goli. Lakini kiukweli kabisa Saidoo hapaswi kucheza zaidi ya dakika 30 kwenye mechi moja ili upate kile unachohitaji toka kwake. Niliwahi kuhoji hapa je ni mkataba wake ndio unalazimisha acheze mechi zote tena dakika tisini au ni mapenzi binafsi ya kocha? Sikupata jibu.
5. Kapombe na Mohamedi Hussein. Hapa Robetino na benchi lake la ufundi waache kukariri kabisa. Hawa ni wachezaji wa mechi kubwa kitendo cha kuwatumia hata kwenye mechi ndogo bila kupumzika matokeo yake ni "fatique" kiasi wakikutana na mechi ngumu kama ya leo wanakuwa uchochoro wanabki kulaumiwa ili hali ni mabeki wazuri.
6. Kukaba kwa macho na kutegeana hili ni tatizo kubwa sana Simba. Lakini hili ni zao la kukosa stamina na kasi. Magoli mengi aliyofungwa Simba msimu huu ni kosa la mabeki na viungo kukaba kwa macho badala ya kufika kwenye mpira kwa wakati.
7. Benchi la ufundi halina "plan B" kwenye mifumo yake ya uchezaji. Matokeo yake timu ikinasa kwenye mfumo wa timu pinzani inakuwa ngumu kuchomoka matokeo yake wanachanganyikiwa na kufanya "sub" za hovyo hovyo. bila mpangilio.

Nini kifanyike kwa haraka Simba:
1. Vunjeni mkataba haraka na Hatekigamana mrudisheni Zrane kwa gharama yoyote ile. Vingenevyo tafuteni kocha wa viungo mwenye uwezo sawa na Zrane. Timu inatakiwa irudishe stamina na kasi kwa muda mfupi sana,
2. Mfukuzeni Robertion haraka kabla madhara hayajawa makubwa. Kama hili haliwezekani basi Mgunda arudishwe haraka kama kocha msaidizi hata kama Robertino hamtaki. Timu ilivyokuwa inacheza mwishoni mwa msimu uliopita sivyo kabisa inavyocheza sasa hivi ndio maana naamini kuwa Mgunda alikuwa na mchango mkubwa sana japo Robetino ndio alikuwa anasifiwa. Kwa sasa hata ushindi unaopatikana Simba ni wa bahati bahati tu hakuna mfumo unauona kwa Simba wakati wanatafuta goli tofauti kabisa na wenzao Yanga.
3, Benchi la ufundi likumbushwe umuhimu wa "rotation" ya wachezaji. Na wachezaji wazee kama Sidoo na Boko wasipewe zaidi ya dakika 30 uwanjani na wasicheze mechi mfululizo. Hii itasaidia kupunguza "fatique" kwa wachezaji. Na pia kuna umuhimu gani unamsajili Mwenda na Duchu wakati unaenda kuwatumia Kapombe na Zmbwe msimu mzima hata mechi za krafiki.
4. Mfadhili, viongozi na bodi nzima ya Simba waache mambo ya ovyo na usanii usanii badala wajikite kwenye mambo ya msingi kama vile kuachana na suala la kupeleka timu "pre season" badala ya kufanya usajili wa maana. Waachane na usajili wa mihemuko kama wa wachezaji kama Onana na kusajili wachezaji wenye uwezo. Ukisajili wachezaji wabovu hata uwapeleke "pre season" Ulaya mwaka mzima bado watakupa matokeo mabovu.


Viongozi wa Simba tulizeni akili rudini sokoni kuanzi leo mkiwa mmetulia tafuteni kiungo mkabaji mwenye "calibre" ya Fraga au Lwanga japo kwenye dirisha dogo ni ngumu kumpata. Lakini kama mkiwa na msaka vipaji mzuri na mkazunguuka Afrika nzima hata kwenye vitimu vidogo anapatikana bila wasiwasi. Pili tafuteni namaba 10 mwenye "footwork" nzuri anayeweza kuichezesha timu vizuri nakuinganisha timu mtanishukuru sana. Che Malone na Inonga ni mabeki wazuri lakini hawana ulinzi kabisa kiasi washambuliaji na viungo wa timu pinzani wanawafikia bila vikwazo vyovyote.

Mwisho bodi ya Simba na Mo Dewji kumbukeni kuwa Robertino na benchi lake la ufundi siku moja wataondoka lakini historia ya kupigwa 5 oclock a.k.a mkono itabaki milele hapa nchini mpaka mwisho wa dunia kwa hiyo fanyeni maamuzi magumu kwa kuzingatia hilo kwani kwa sasa Simba ina wachezaji mahiri lakini haina timu. Nina hakika Simba hii iliyopo sasa angekuwa Mgunda au hata Julio tu asigepigwa tano zote hizo.

Ni mtizamo tu.
 
20231105_202133.jpg
 
Mlisema kmc na jkt ni vibonde haya sasa. Mseme na leo

Kosa la kocha Robertinho kumuweka manula alafu anajua manula amekaa nje muda mrefu sana hajacheza so hayuko fit
Objective football imemponza robatinyo.... katupa fedhea kubwa sana
 
Ila maoni yangu ni kumchezesha Manula mechi hii muhimu kwa mara ya kwanza tokea apone ni kosa kubwa.

Pili, Kapombe hana nafasi mbele ya Mwenda. Kocha lazima afanye hayo mabadiliko ni muhimu sana.

Bado kuna changamoto ya kipa na kiungo mshambuliaji badala ya kumtegemea Saidoo tu.

Leo mechi ameshinda kocha bora na timu bora hapo ushabiki pembeni.

The fact that Simba hajamaliza mechi na clean sheet was a big concern to me. Sikutegemea muujiza maana kama Simba wana concede kila mechi, ina maana walitakiwa washinde kwa magoli mengi.

Something I didn’t think was going to happen.
Manula mnamuonea jamani. Hii mechi ya leo hata angekuwa Bethez angegongwa hizo hizo 5. Ona kasi ya YANGA mwanzo mwisho.
 
Mbona bado hujalala mkuu au na usingizi umegoma?
 
Manula mnamuonea jamani. Hii mechi ya leo hata angekuwa Bethez angegongwa hizo hizo 5. Ona kasi ya YANGA mwanzo mwisho.
Mpira ni mchezo wa kisaikolojia zaidi. Tizama mechi ya leo Liverpool wamekosa magoli mengi dhidi ya Luton na karibia wapoteze mechi.

Manula was below par. Kuanzia goli la kwanza.

Kapombe is unreliable.

Hakuna sub kumsaidia Saidoo.

Kama umesoma vizuri nilichoandika. Nimesema kocha bora na timu bora wameshinda leo.

Simba matokeo ya sare yangekuwa bora kwao leo.

Sasa sijui kocha hakufahamu au ni kitu gani?

Maana ni bora ange apply ile tactic kama walivyocheza na Al Ahly. Kulinda zaidi.

However baada ya Kibu Dennis kuumizwa, wale mabeki wa Yanga walifunguka zaidi. Hivyo kusaidia Yanga kuweza kufanya high pressing.

Miqueson hakuna kitu tena.

Kocha wa Yanga ni mzuri pia kwasbabu wachezaji wake wanaonyesha wana fitness ya hali ya juu. Kitu muhimu sana kwenye style ya high pressing.
 
Back
Top Bottom