...haya wadau, tuhabarishane maendeleo, mafanikio, kusua sua hata kuporomoka kwa chama letu, Mnyama Mkali, Simba taifa kubwa!
Wengine sie, ushabiki tuliuanzia miaka hiyo, unaunga foleni ya kuingia national stadiumtangu saa tano asubuhi... vumbi, jua, mbwa na virungu vya FFU, lakini mwisho wa siku aaah... tunatoka tunachekelea kumnywesha Yanga goli 6-0, kipigo mpaka kipa wao Benard Madale aliangua chozi!...
Enzi hizo Kajole Machela akichonga kona hizooooo zinaingia zenyewe golini!... mambo yakoje siku hizi?
Wengine na tujikumbushe!
Jamani wakati tunaangalia historia ya Wekundu, Simba na Azam jana vipi katika kuitafuta nafasi ya pili?.
Mbu usinikumbushe shemeji yangu Eddo Chumilia,imebaki ni hadithi tu!
Mvua ilivunja mchezo... ndio nimeona kwenye TV
View attachment 4069
Mashabiki wa soka wa timu ya Simba ya Dar es Salaam, wakijaribu kuondoa maji ya mvua kwenye uwanja wa Uhuru jana, baada ya mvua kubwa kunyesha katika kipindi cha pili wakati timu hiyo ilipokuwa ikipambana na Azam na kuongoza kwa 1-0 kabla mchezo kuvunjwa katika kipindi cha pili kutokana na mvua.
source; Mwananchi Read News
Nimeangalia mtandao wa dullonet.com, Wekundu wa Msimbazi wamewafunga Azam bao 3-0. Hivyo nadhani nafasi ya pili sasa tunaisogelea vyema.
...na lile la jana wamelihesabu? 😀
Mechi ngumu ni ya Kagera & ya Yanga, lakini wote wanafungika tu!
Date::4/6/2009
Simba yazidi kupaa yaichapa Kagera Sugar 2-0
Lily Lugakingira, Bukoba
SIMBA imethibisha kweli inataka kuiwakilisha nchi kwenye michuano ya kimataifa msimu ujao baada ya kuwachapa wapinzani wake nafasi ya pili, Kagera Sugar kwa mabao 2-0 kwenye uwanja wa Kaitaba mkoani Kagera.
[
Taifa kubwa kutafuta nafasi ya pili?
Simba leo wameshika nafasi ya pili na watacheza Confederation cup baada ya kuwafunga Polisi Dodoma 2-0
Vila Squad na Polisi Dodoma wameshuka daraja leo rasmi!
Hongereni watani wetu Simba!
...hivi kuna watu walidhani Mnyama ataikosa nafasi ya pili? nyie mnacheza kweli 🙂
SIMBA TAIFA KUBWA!