Simba Taifa Kubwa!

Mbu

JF-Expert Member
Jan 11, 2007
12,753
7,844
...haya wadau, tuhabarishane maendeleo, mafanikio, kusua sua hata kuporomoka kwa chama letu, Mnyama Mkali, Simba taifa kubwa!

Wengine sie, ushabiki tuliuanzia miaka hiyo, unaunga foleni ya kuingia national stadiumtangu saa tano asubuhi... vumbi, jua, mbwa na virungu vya FFU, lakini mwisho wa siku aaah... tunatoka tunachekelea kumnywesha Yanga goli 6-0, kipigo mpaka kipa wao Benard Madale aliangua chozi!...

Enzi hizo Kajole Machela akichonga kona hizooooo zinaingia zenyewe golini!... mambo yakoje siku hizi?

Wengine na tujikumbushe!
View attachment 4037

...Haidery Abeid Muchacho, the best SSC captain ever?​
 
View attachment 4038

...pamoja na hizo pekosi, raizoni, na slim fit shirts, jamaa walikuwa wanaupiga hao si mchezo!

L-R; Yusuph K, Martin Kikwa (kwa magoli ya vichwa huyo!), Aluu Ally, Ismail Mwarabu, Mohamed Bakari Tall (Centre half wa kutuainiwa), Athuman Juma, Hamis, Mohamed Kajole Machela, na Abdallah Hussein
 
View attachment 4039

...yaani enzi hizo mtangazaji wa RTD akishamaliza kutaja listi tu, mnajua leo Kandambili kalala...!

Omar Mahadhi Bin Jabir anaonekana pale, Kajole Machela, Bakari Tall, Daud Salum Bruce Lee, George Best Kulagwa, Adam Sabu, King Kibaden naye yumo, we acha tu!
 
View attachment 4040

...kidogo kidogo ndio mwendo, makao makuu ya chama letu dhidi ya uyoga wa majengo mtaa wa msimbazi... tutafika tu!
 

View attachment 4041

...raha ya enzi hizo kulokuwa hakuna mgao wa umeme, na wala ukitumwa gengeni huendi mpaka kina Omar Jongo, Ahmed Kipozi, au Mikidadi Mahmoud wamalize kutangaza mpira!
 
View attachment 4042

Golden Boy mwenyewe huyo,...Zamoyoni Mogella anaangalia jinsi ya kumpita Yussuf Bana! ...enzi hizo kuna kina Lilla Shomari, Mtemi Ramadhani, aisee...!
 
View attachment 4043

...mnyama huyo! we acha tu!... Nadhani Simba baada ya hapa 1990's, haijawahi tena kutoa kikosi kikali kama hiki, enzi hizo George Masatu, Iddi Pazi 'Father', Mwameja, Twaha Hamidu , Method Mogella, Zamoyoni Mogella, Edward Chumila 'wote wapo fiti! ...mboni ilikuwa raha!!!
 
View attachment 4044

...picha kwa hisani ya mdau. Pamoja na mazuri yote ya kikosi hiki kufika fainali ya CAF,...doa liliingia tuliponyanganywa tonge mdomoni, mbele ya Alhaj Ali Hassan Mwinyi kufungwa na STELLA! ...aaarrgggh... Mzee Mwinyi, kama Kikwete naye Yanga tu, kimoyo moyo alifurahia tulipofungwa!

wanaonekana ni pamoja na Marehemu Ramadhan Lenny Maufi, Thomas Kipese, George Masatu, George Lucas, Kassongo Athumani, David Mihambo, Fikiri Magosso,...
 

...nitakuwa mchoyo wa fadhila nitapoacha kuwataja kikundi cha uhamasishaji cha Muchacho, wana KIDEDEA, pamoja na mzee Magoma Moto pale..."...eeeeh Kidedea,...hao Simba Kidedea, eeh Kidedea!..."

View attachment 4045
 

...washabiki wenzangu wa mnyama mwekundu, mnyama mkali wa miaka hii endeleeni kutuilmisha,...hali ikoje huko nyumbani?

halafu walotunikiwa heshima ya 'walezi' wa Klabu wa maisha, kina Mzee Samuel Sitta, Phillemon Sarungi, ...bado wapo mstari wa mbele, au nao wamejionea michosho tu?

Mo' Dewji naona kaamua kudhamini Young Lyons eh, kaazi kweli, au sio Mohamed Enterprises huyo?

Ipo siku tu atatokea ABRAMOVICH mmoja ainunue timu, kandambili ndipo mtaposhika adabu nyie,...!

SIMBA TAIFA KUBWA!
 
Mzee Mbu, mambo makubwa hayo ya mnyama! namkumbuka mchezaji mwenye mbio kama kiberenge... Sunday Juma.

Siku hizi wachezaji hawana miili... vijitu vidigi vidigo ndio vinavyosukuma Boli... yaani hamna raha kwa kweli... magoli ni ya kuyatafuta! nani alikuambia wakati wa Zamoyoni, Mnyama alikuwa na ukame wa mabao? na yule kocha mchezaji Hasan hafif! Sports Club Villa ililala tatu bila pale uwanja wa zamani wa taifa! Klabu bingwa Afrika mashariki na kati hiyo. Watu tuliimba kidedea kwa miguu toka keko hadi ubungo... we acha tu!!

Enzi za akina Ball Juggler, Moses Mkandawile, Hamis Thobias Gaga (Gagarino), ilikuwa raha kwakweli.
 
NIMEWAHI kuwaambia miongoni mwa wanafunzi wangu, "ukiwa mpenzi wa SIMBA, then LIVERPOOL should be your favourite ENGLISH TEAM"
Bado natafuta ukweli wa mawazo yanguu!
 
NIMEWAHI kuwaambia miongoni mwa wanafunzi wangu, "ukiwa mpenzi wa SIMBA, then LIVERPOOL should be your favourite ENGLISH TEAM"
Bado natafuta ukweli wa mawazo yanguu!

Mkuu hapo umeenda chaka si kweli....
Mashabiki wengi wa Simba ni Man U wengi ila wengi wao wapo hata the Gunners.
 
very interesting aiseee! but unajua hayo ya enzi hizo bongo hakuna hata luninga, sku hizi ushindani wa kinyumbani nyumbani ushatuchosha, saivi tunataka kuziona timu hizi zikishindana kuchukua vikombe vya kimataifa, sio nyumban tunatisha lakini tukivuka sudani tu tunakuwa mama.
 
very interesting aiseee! but unajua hayo ya enzi hizo bongo hakuna hata luninga, sku hizi ushindani wa kinyumbani nyumbani ushatuchosha, saivi tunataka kuziona timu hizi zikishindana kuchukua vikombe vya kimataifa, sio nyumban tunatisha lakini tukivuka sudani tu tunakuwa mama.

...naaaaaaaaam, Enzi hizo kuanzia kina Mambosasa walivyowatoa jasho El-Mahalla El-Kubra...Al Ahly na Zamalek

NIMEWAHI kuwaambia miongoni mwa wanafunzi wangu, "ukiwa mpenzi wa SIMBA, then LIVERPOOL should be your favourite ENGLISH TEAM"
Bado natafuta ukweli wa mawazo yanguu!

...Gunners for Life! japo am Liverpool 'Sympathizer!' tangu enzi za kina #10 ya Kevin Keegan, Barnes, na golie #1 Bruce David Grobbelaar...

Mzee Mbu, mambo makubwa hayo ya mnyama! namkumbuka mchezaji mwenye mbio kama kiberenge... Sunday Juma.

Enzi za akina Ball Juggler, Moses Mkandawile, Hamis Thobias Gaga (Gagarino), ilikuwa raha kwakweli.

...naaam, mbio mpaka mpira anauacha nyuma...! unamkumbuka Mavumbi Juma? ha ha ha..kwa mashuti yule! ...Taifa kubwa bila kumtaja midfielder ya kimataifa Nicodemus Njohole, alofatiwa na Deo Njohole miaka ilifuatia...!

Miaka kabla ya hapo kulikuwa na wingers machachari kina Maulid Dilunga, Abbas Kuka!

unamkumbukia na 'Alhaj' Thuwein Ally? ...kiki zake za guu la kushoto aiseee!...

SIMBA TAIFA KUBWA!
 
Nyie lakini msiwasahau vijana kama kina Mambo sasa kule songea, halafu Tanga unakutana na kina Razaki Kareka, Enzi hizo bwana.............. Mm yeboyebo lakini vikosi mlivyovitaja hapo navikubali manake enzi hizo ilikua watu twapata homa mpaka mpira unaisha, kwa sasa kijana Mrisho ngasa ndo anajaribu mbio zakina kipese
 
mbu inaonyesha huku ndani wote yanga usife moyo tuko wengi nafikiri ni msimu tu
 
mbu inaonyesha huku ndani wote yanga usife moyo tuko wengi nafikiri ni msimu tu

Tupo wengi humu, basi tu timu yetu kwa sasa iko ki-kanjanja... utamu zaidi ni pale I AM NOT WALKING ALONE

KWANGU MIMI LIVERPOOL + SIMBA = PERFECT
 
Mkuu hapo umeenda chaka si kweli....
Mashabiki wengi wa Simba ni Man U wengi ila wengi wao wapo hata the Gunners.

hao itakuwa wa hapa juzi juzi, kwa wakati huo tulikuwa tunnafata mikanda EMPIRE....!
jezi chata CANDY....! jezi nyekundu muda wote....!
 
Back
Top Bottom