Simba, tafadhali mtoeni Said Ndemla kwenye kifungo hiki

MAKULUGA

JF-Expert Member
Jan 21, 2011
7,159
9,360
Kwa kiwango cha uchezaji cha kiuongo mahiri Said Ndemla hastahili kufanyiwa haya anayofanyiwa. Kumuweka benchi kijana huyu kwa miaka mitatu (03) haiko sawa na kuto mtendea haki.

Inanawezekana yeye ameridhika na malipo anayopata Simba, ila atambue kuwa mpira ni kazi inayodumu kwa miaka michahche sana, ukiwa na bahati ni miaka 12 tu.

Kijana huyu nitaendelea kumbuka sana. Kwa wasiojua huyu ndio aliyeiokoa Simba na ile aibu, pale ambapo Yanga walikuwa wanaongoza Magoli matatu kipindi cha Kwanza! Kipindi cha pili Kibadeni alimuuingiza kinda huyu na akaenda kulisambaratisha eneo la kiungo la Yanga na tukawasawazisha.

Ndemla unaipenda sana Simba lakini hustahili kukaa mbenchi

ONDOKA KATAFUTE MAISHA KWINGINE!
 
Aende Yanga huko hana mpinzani dimba la kati anajua sana dogo.
 
Soka ni ushindani na sio huruma kama ambavyo mnataka nyinyi, ni sawa na mwanao anapata mitihani 95 lakini kuna wanaopata 100 mitihani yote unataka apewe number moja kwa huruma!!

Ukiona hapati number ujue ushindani umemzidi hata kama kiwango chake ni cha juu. Kama wewe ni Simba kweli unataka akiingia yeye atoke nani ambae kiwango chake kiko chini kuliko Ndemla?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Soka ni ushindani na sio huruma kama ambavyo mnataka nyinyi, ni sawa na mwanao anapata mitihani 95 lakini kuna wanaopata 100 mitihani yote unataka apewe number moja kwa huruma!!

Ukiona hapati number ujue ushindani umemzidi hata kama kiwango chake ni cha juu.Kama Wewe ni Simba kweli unataka akiingia yeye atoke nani ambae kiwango chake kiko chini kuliko Ndemla??

Sent using Jamii Forums mobile app
Akianza Chama, au shibobo amalizie Ndemla, or viseversa.
 
Nakumbuka Simba walimruhusu aende nje (Sweden) kwa majaribio mwaka 2017 wakasema amefuzu sijui ikawaje akarudi tena, mwaka 2019 akaruhusiwa tena akaenda Sweden kwani iliishia wapi?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Katika Soka hakuna kitu Huruma ila kipo kitu Bidii. Bidii ya Samata ndiyo iliyomfikisha huko. Kocha huwa anawachezesha wachezaji watakaomwezesha kufanikisha ndoto zake.

Wachezaji wetu wanatakiwa kuwa na washauri wa Soka Binafsi wanaoweza kumjengea mchezaji uwezo wa kujiamini na kucheza kwa kiwango Chake cha Juu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ndemla ni mchezaji mzuri sana lakini anakosa mwendelezo. Mechi hii akicheza vizuri mechi ijayo anavurunda. Achukue mfano kwa Muzamiru Yasin yeye alionekana kama kashapotea na hana namba Simba lakini alifanya mazoezi kwa nguvu sana na akaweka malengo yake siku alipopewa nafasi na Ausems hakufanya makosa mpaka leo bado anapambana na akina Chama. Hata Sven naye ameshamuamini ila hizi mechi chache kakosekana sababu ya majeruhi. Pia ajifunze kwa mwenzake Mkude waliotoka naye timu ya vijana ya Simba jinsi alivyopambana pamoja na Simba kuleta viungo wakabaji kibao ndani ya hii miaka takribani sita lakini Mkude kakomaa mpaka leo ndio mmiliki wa dimba la kati.

Kwa Ndemla anatakiwa afanye mazoezi sana na ajiandae siku akipewa nafasi aonyeshe uwezo wake wote kwa faida ya timu nzima. Mimi ni mmojawapo wa wale wananoamini kuwa Ndemla ana kiwango kizuri lakini tatizo akipewa nafasi badala ya kuisaidia timu yeye anacheza kibinafsi ili aweze kuwaonyesha mashabiki na benchi la ufundi kuwa anaweza. Kwa mfano kwenye Mapinduzi Cup alipewa nafasi alitakiwa aonyeshe namna ya kuisaidia timu lakini alishindwa kabisa ilifika mahali hata yupo mita 45 anataka apige afunge mwenyewe. Kwa Simba ya sasa hivi ukipata nafasi itumie kuisaidia timu ipate ushindi lakini ukitumia nafasi ya kucheza kibinafsi ujue umepotea.

Ushauri wa mwisho kwa Ndemla ajifunze kucheza nafasi zaidi ya moja uwanjani. Kwa sasa Simba ina viungo wengi lakini washambuliaji wa mwisho ni wachache. Mimi namuona Ndemla kama mshambuliaji mmoja mwenye kitu cha tofauti iwapo tu atapata maelekezo kidogo kutoka benchi la ufundi na yeye mwenye akiamua kwa moyo wake wote kucheza kama mshambuliaji wakati huo huo akiwa kiungo. Lakini akishindwa yote hayo bora msimu ujao atafute timu nyingine itakayompa nafasi ya kucheza ili asipoteze kipaji chake kwani umri unaenda na yeye hii miaka miwili mitattu ijayo anatakiwa awe kwenye kilele cha ubora wake.
 
Back
Top Bottom