Simba, tafadhali mtoeni Said Ndemla kwenye kifungo hiki

Mleta na kuungamkono kwa kutumia Uhuru wa kutoa mawazo ni wakila mtu ila inategemea na mawazo gani unayoyatoa. Mawazo mengine yanahitaji utaalam na sio mihemko au unazi kwa mlengwa unaempigia chapuo.

Kitaalam
Kila mchezaji hapangwi kwenye mechi kama haonyeshi juhudi kwenye mazoezi ndugu.

Huwezi bweteka alafu ukategemea upate upendeleo uwanjani. Wote nilazima tujue makocha ndio watu wanao kaa na wachezaji kwa muda mrefu na kuona jiudi zao katika program zao za mazoezi.

Haiwezekani kocha akakupanga au akakupa kipaumbele kwenye list yake kama hujitumi na kujitambua kama unawajibu wa kuipigania namba nakuipa timu Matokeo.

Wote ni mashahidi wakati mwalim ven ameanza kazi jukum LA kwanza ilikua kuwapa wachezaji nafasi ili kila mmoja aonyeshe uwezo wake uwanjani. Lakini kidogo kocha huyu afurushwe kotokana na baadhi ya wachezaji kutokuonyesha kujituma uwanjani.

Sasa huyu ndemla mnae mpigia tarumbeta je! Hakupewa nafasi? Nakama alipewa nafasi ni result gani alileta kwa timu?

Tuache kujidai sisi ni wajuaji kuliko coach. Mpira sio kamari mpira ni taaluma na ndio maana yupo ven na matola pale simba. Angalia sasa hivi coach walivyopata kikosi chao na kinavyotupa raha Sana wana simba. Angalia Kandanda murua linavyotandazwa na maquison ni habari nyingine.

Aishi Manila
Shomari kapombe
Paschal wawa
Erasto nyoni
Mohammed Hussein
Jonas mkude a.k.a Nungu Mungu
Fransice kahata
Cloutus chotta chama
Jose Luise maquisson
Medie kagere
John boko

Hapa hata haje nani mziki juu ndio mambo kwa sasa wa kocha ven na matola na Matokeo tunayaona jani. Hawa ndio wanaojitambua na kujituma uwanjani. Anaetaka kuingia hapo basi ni.lazima jasho limtoke kuwanyanganya namba hawa askari wetu.

SAID-NDEMLA.jpg

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Yale mashuti yake angekua anafunga angepata number ya kudumu, Ye anapiga tu ili ajulikane ni mpiga mashuti
 
Acha Majungu muda wake ukifika nae atapata tu nafasi. Mbona hamshangai jinsi Jonas Mkude alivyokaa benchi Kipindi cha akina Marehemu Mafisango ila alivumilia na kujifunza kutoka Kwake na sasa ni Mchezaji tegemeo ndani ya Simba SC?
Mkuu haya Ni majungu, asubiri muda ufike, kumbuka huu Ni mwaka wa nne anakaa benchi, Kama SI jukwaani
 
Tusiwe tunaongea tu bila sababu ni wazi vijana wetu hawafanyi vyema mazoeni hawajitumi ndio sababu makocha hawawapi nafasi na wakipewa nafasi hawana wanachofanya

yawezekana ndemla anacho kipaji lakini je anamshawishi kocha mazoezini na anapopewa nafasi
yawezekana mlipili anachi kipaji lakini je anamshawishi kocha mazoezini.

mfano mzuri ni muzamir yassin alipokuja simb alikuwa mchezaji wa benchi lakini alipopata nafasi tumeona kazi yake

mo hussein alipoteza namba kwa asante kwasi lakini juhudi yake tumeiona hadi kwasi kakimbia

Haruna shamte anaoata nafasi sasa hivi lakini anaonyesha nini ni wazi.simba watatafuta beki mwingine wa kulia kusaidiana na kapombe

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom