Simba, tafadhali mtoeni Said Ndemla kwenye kifungo hiki

Soka ni ushindani na sio huruma kama ambavyo mnataka nyinyi, ni sawa na mwanao anapata mitihani 95 lakini kuna wanaopata 100 mitihani yote unataka apewe number moja kwa huruma!!

Ukiona hapati number ujue ushindani umemzidi hata kama kiwango chake ni cha juu.Kama Wewe ni Simba kweli unataka akiingia yeye atoke nani ambae kiwango chake kiko chini kuliko Ndemla??

Sent using Jamii Forums mobile app
Fact

Nadhani walitaka atoke Jonas Mkude aingie ndemla halafu waanze kusema kuwa Simba inamchukia Mkude

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ndemla ni mchezaji mzuri sana lakini anakosa mwendelezo. Mechi hii akicheza vizuri mechi ijayo anavurunda. Achukue mfano kwa Muzamiru Yasin yeye alionekana kama kashapotea na hana namba Simba lakini alifanya mazoezi kwa nguvu sana na akaweka malengo yake siku alipopewa nafasi na Ausems hakufanya makosa mpaka leo bado anapambana na akina Chama.Hata Sven naye ameshamuamini ila hizi mechi chache kakosekana sababu ya majeruhi. Pia ajifunze kwa mwenzake Mkude waliotoka naye timu ya vijana ya Simba jinsi alivyopambana pamoja na Simba kuleta viungo wakabaji kibao ndani ya hii miaka takribani sita lakini Mkude kakomaa mpaka leo ndio mmiliki wa dimba la kati.

Kwa Ndemla anatakiwa afanye mazoezi sana na ajiandae siku akipewa nafasi aonyeshe uwezo wake wote kwa faida ya timu nzima. Mimi ni mmojawapo wa wale wananoamini kuwa Ndemla ana kiwango kizuri lakini tatizo akipewa nafasi badala ya kuisaidia timu yeye anacheza kibinafsi ili aweze kuwaonyesha mashabiki na benchi la ufundi kuwa anaweza. Kwa mfano kwenye Mapinduzi Cup alipewa nafasi alitakiwa aonyeshe namna ya kuisaidia timu lakini alishindwa kabisa ilifika mahali hata yupo mita 45 anataka apige afunge mwenyewe. Kwa Simba ya sasa hivi ukipata nafasi itumie kuisaidia timu ipate ushindi lakini ukitumia nafasi ya kucheza kibinafsi ujue umepotea.

Ushauri wa mwisho kwa Ndemla ajifunze kucheza nafasi zaidi ya moja uwanjani. Kwa sasa Simba ina viungo wengi lakini washambuliaji wa mwisho ni wachache. Mimi namuona Ndemla kama mshambuliaji mmoja mwenye kitu cha tofauti iwapo tu atapata maelekezo kidogo kutoka benchi la ufundi na yeye mwenye akiamua kwa moyo wake wote kucheza kama mshambuliaji wakati huo huo akiwa kiungo. Lakini akishindwa yote hayo bora msimu ujao atafute timu nyingine itakayompa nafasi ya kucheza ili asipoteze kipaji chake kwani umri unaenda na yeye hii miaka miwili mitattu ijayo anatakiwa awe kwenye kilele cha ubora wake.
Fact

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kagera sugar wanaweza kumlipa mshahara anaopata Simba kwa Sasa?
Kwa mchezaji mwenye malengo, mwenye kipaji, mpambanaji na anayejiamini hawezi kukaa tu benchi kwenye timu eti kwa sababu analipwa mshahara mkubwa. Kwa vyovyote vile lazima atatafuta jukwaa sahihi kwenye hizi timu za kati kama Mtibwa, kagera, Ruvu, n.k. aonyeshe uwezo wake halafu hizi timu kubwa zitamfuata kwa mshahara mkubwa zaidi ya huo wanaompa sasa. Mfano mmoja Hasani Dilunga alikuwa Yanga yakatokea yaliyotokea lakini kwa kuwa alikuwa anajiamini aliachana na Yanga na kama sikosei akaenda Ruvu na baadae akaibukia Mtibwa na sasa yupo Simba tena akiwa na kiwango cha hali ya juu. Hata Kelvin Yondani Simba walianza kumpiga benchi kiajabu ajabu lakini kwa kuwa alikuwa anajiamini aliamua kuondoka na kujiunga na Yanga ili kuokoa kipaji chake vinginevyo angeng'ang'ania mshahara tu Simba Yondani angepotea mazima katika ramani ya soka.
 
Mlipili ndo nani?
Beki wa zamani wa Toto African ya Mwanza. Beki mmoja hivi fundi, ng'ado kwa ng'ado, mbishi mbishi fulani awapo kazini uwanjani, kwa mbali ana umbo kama la George Magere Masatu na hata uchezaji wake kidogo umefanana kama wa Masatu. Beki ambaye ndiye alikuwa muhimili wa ukuta wa Simba kwenye ligi ya ndani na michezo ya kimataifa miaka michache hivi iliyopita na ili kuujua ubora wake nenda "youtube" ukaangalie Simba VS Al Masry.Kwa sasa Mlipili yupo anaozea benchi pale Simba Sport Club na hakuna anayejua sababu hasa ni nini kwani alianza Ausems kumpiga benchi na hata Sven naye hajampa nafasi kabisa kuonyesha uwezo wake.

Kwangu mimi naona ajabu kwa Tairone na Kennedy kupewa nafasi ya kucheza wakati fundi Mlipili hata benchi hakai. Inawezekana labda makocha wameona kiwango chake kimeshuka sana maana wao ndio wapo naye mazoezini kila siku. Lakini yote kwa yote ni wakati wake sasa kuondoka Simba ili aokoe kipaji chake kwani umri wake bado unamruhusu kucheza mpira kwa muda mrefu ujao na si kuendelea kukaa Simba wakati hata kwenye listi ya wachezaji wa akiba mara nyingi anakuwa hayupo.
 
Basi mtoeni kwa mkopo ili asiue kipaji na bado aendelee kuwa msaada wa timu baadae,
Soka ni ushindani na sio huruma kama ambavyo mnataka nyinyi, ni sawa na mwanao anapata mitihani 95 lakini kuna wanaopata 100 mitihani yote unataka apewe number moja kwa huruma!!

Ukiona hapati number ujue ushindani umemzidi hata kama kiwango chake ni cha juu.Kama Wewe ni Simba kweli unataka akiingia yeye atoke nani ambae kiwango chake kiko chini kuliko Ndemla??

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Acha Majungu muda wake ukifika nae atapata tu nafasi. Mbona hamshangai jinsi Jonas Mkude alivyokaa benchi Kipindi cha akina Marehemu Mafisango ila alivumilia na kujifunza kutoka Kwake na sasa ni Mchezaji tegemeo ndani ya Simba SC?
 
Back
Top Bottom