Ghazwat
JF-Expert Member
- Oct 4, 2015
- 23,718
- 66,262
Naaam...Patashika ya michuano ya Simba Super Cup (SSC) imeendelea kuvurumishwa leo January 29, 2021 ambapo TP Mazembe ya Congo, walikuwa wakipambana vilivyo na Al Hilal SC kutoka nchini Sudan.
Mchezo ulionza kwa kila timu kuusoma mchezo wa mpinzani wake ambapo iliwachukua dakika ya 11' ya mchezo kwa TP Mazembe kuandika bao la kwanza lililofungwa na Moustapha Kouyate.
Al Hilal waliweza kujibu mapigo ambapo dakika ya 29' walisawazisha kupitia kwa mshambuaji Bonganga Vinny, hadi kumalizika kwa kipindi cha kwanza matokeo yalikuwa 1-1
Kipindi cha pili kimeanza kwa mashambulizi kwa pande zote mbili huku mabadiliko kadhaa yakifanyika, lakini Al Hilal waliweza kunufaika zaidi kwa mabadiliko hayo kwani katika dakika ya 90' mchezaji Mohamed Mussa wa Al Hilal alizima ndoto za Tp Mazembe kuibuka na ushindi baada ya kukwamisha wavuni mpira na kuandika bao la pili
Hadi mwisho TP Mazembe 1 Al Hilal 2