Simba Super Cup | Al Hilal wawatuliza TP Mazembe, wapigwa 2-1 Uwanja wa Mkapa

Ghazwat

JF-Expert Member
Oct 4, 2015
23,718
66,262
Naaam...Patashika ya michuano ya Simba Super Cup (SSC) imeendelea kuvurumishwa leo January 29, 2021 ambapo TP Mazembe ya Congo, walikuwa wakipambana vilivyo na Al Hilal SC kutoka nchini Sudan.

Mchezo ulionza kwa kila timu kuusoma mchezo wa mpinzani wake ambapo iliwachukua dakika ya 11' ya mchezo kwa TP Mazembe kuandika bao la kwanza lililofungwa na Moustapha Kouyate.

Al Hilal waliweza kujibu mapigo ambapo dakika ya 29' walisawazisha kupitia kwa mshambuaji Bonganga Vinny, hadi kumalizika kwa kipindi cha kwanza matokeo yalikuwa 1-1

Kipindi cha pili kimeanza kwa mashambulizi kwa pande zote mbili huku mabadiliko kadhaa yakifanyika, lakini Al Hilal waliweza kunufaika zaidi kwa mabadiliko hayo kwani katika dakika ya 90' mchezaji Mohamed Mussa wa Al Hilal alizima ndoto za Tp Mazembe kuibuka na ushindi baada ya kukwamisha wavuni mpira na kuandika bao la pili

Hadi mwisho TP Mazembe 1 Al Hilal 2

Screenshot_20210129-190914.jpg
 
Simba SC ni Bingwa wa Simba Super Cup

TP hawezi kufunga mabao matano bila majibu dhidi ya Mnyama Jumapili ilhali tayari leo ameruhusu mabao mawili.

Hivi hizi hesabu za bao tano bila umezipigaje mkuu ?
Ukweli ni kwamba Mazembe akishinda tatu bila anakua bingwa.

NB: Tutakubaliana kwamba ni ngumu sana Simba kupoteza kwa tofauti ya magoli matatu.
 
Hivi hizi hesabu za bao tano bila umezipigaje mkuu ?
Ukweli ni kwamba Mazembe akishinda tatu bila anakua bingwa.

NB: Tutakubaliana kwamba ni ngumu sana Simba kupoteza kwa tofauti ya magoli matatu.
Hata wewe pia umekosea hesabu hapo. Tp Mazembe wana goal difference ya -1 huku Simba wana goal difference 3. Hivyo Tp Mazembe wanatakiwa washinde goli nne kwa sifuri ndio atakuwa amemfikia Simba kwa kuwa nae sawa kwa kuwa na goal difference 3. Na ili amzidi Simba basi anatakiwa ashinde goli tano kwa sifuri
 
Yes...Nilipita njia ya mkato tu, Tp awe bingwa lazima ashinde 5 kitu ambacho hakiwezekani kwa sasa..!

Nadhani amekuelewa..!
 
Yes...Nilipita njia ya mkato tu, Tp awe bingwa lazima ashinde 5 kitu ambacho hakiwezekani kwa sasa..!

Nadhani amekuelewa..!
Ulichosema mwanzo ni sahihi.
Sudani hadi sasa ana goal difference -2 kafungwa 5 kafunga 3.

Mazembe akimfunga Simba 3-0, Simba atakuwa wa goal difference 0 maana ana goal 4 na kafungwa 4.
Hivyo Mazembe atakuwa Bingwa kwakuwa na goal difference 2 kafunga 4 kafungwa 2.

Mazembe akimfunga Simba 2-0 atakuwa na GD 3-2 =1 na Simba atakuwa na GD 4-3=1 hivyo Mazembe anaweza kuwa Bingwa kwakuwa kamfunga Simba ktk mechi yao.
Karibuni kuchangia.
 
Hata wewe pia umekosea hesabu hapo. Tp Mazembe wana goal difference ya -1 huku Simba wana goal difference 3. Hivyo Tp Mazembe wanatakiwa washinde goli nne kwa sifuri ndio atakuwa amemfikia Simba kwa kuwa nae sawa kwa kuwa na goal difference 3. Na ili amzidi Simba basi anatakiwa ashinde goli tano kwa sifuri
Yes...Nilipita njia ya mkato tu, Tp awe bingwa lazima ashinde 5 kitu ambacho hakiwezekani kwa sasa..!

Nadhani amekuelewa..!
Hapo mmepiga hesabu ya aina moja mmesahau kuwa TP Mazembe akimfunga Simba goli nne kwa sifuri ni kwamba Simba atapungua goal difference na itakuwa karuhusu magoli matano huku Simba akiwa amefunga goli nne. Hivyo atakuwa na -1 goli tatu tu kwa bila, zinamtosha Mazembe kuwa bingwa japokuwa ni jambo gumu kutokea ila tunazungumzia kimahesabu tu.
 
Ulichosema mwanzo ni sahihi.
Sudani hadi sasa ana goal difference -2 kafungwa 5 kafunga 3.

Mazembe akimfunga Simba 3-0, Simba atakuwa wa goal difference 0 maana ana goal 4 na kafungwa 4.
Hivyo Mazembe atakuwa Bingwa kwakuwa na goal difference 2 kafunga 4 kafungwa 2.

Mazembe akimfunga Simba 2-0 atakuwa na GD 3-2 =1 na Simba atakuwa na GD 4-3=1 hivyo Mazembe anaweza kuwa Bingwa kwakuwa akimfunga Simba ktk mechi yao.
Karibuni kuchangia.
Upo sahihi mkuu
 
Back
Top Bottom