Simba sc: Mshusheni shipa mbuyu twite | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Simba sc: Mshusheni shipa mbuyu twite

Discussion in 'Sports' started by mwakitundilo, Aug 16, 2012.

 1. m

  mwakitundilo Member

  #1
  Aug 16, 2012
  Joined: Aug 15, 2012
  Messages: 28
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nimeudhishwa sana na kitendo cha kitapeli na kisichokuwa cha kiuanamichezo kilichofanywa na mchezaji MBUYU TWITE wa APR ya Rwanda. Mchezaji huyu alisajiliwa na Simba SC kutoka APR, lakini katika hali ya kustaajabisha mchezaji huyu akiwa kishalipwa kitita cha USD 30,000 kaamua kusajili pia YANGA. Nawashauri wanachama, viongozi, mashabiki na "wazee" wa Simba kumtia adabu mkongoman huyu ili awe fundisho kwa wachezaji wengine wenye tabia kama hiyo. Adhabu ninayopendekeza ni kumshusha shipa naamini "wazee" wangu wa Simba hili liko ndani ya uwezo wenu. NAWASILISHA​
   
 2. PrN-kazi

  PrN-kazi JF-Expert Member

  #2
  Aug 19, 2012
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 2,890
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  Though! what he did is not acceptable anywhere, but that is not punishment and remedy he deserve.
   
 3. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #3
  Aug 19, 2012
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,343
  Likes Received: 1,808
  Trophy Points: 280
  Jamani kwani mchezaji yupo yeye tu? Si mtafute wengine?
   
 4. K

  KIM KARDASH JF-Expert Member

  #4
  Aug 19, 2012
  Joined: Sep 21, 2011
  Messages: 5,083
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  Acheni kupiga mayowe,yapo mambo matatu ambayo yamemfanya beki Mbuyu Twite wa APR ya Rwanda, aachane na Simba SC na kuamua kujiunga na YANGA.

  Mambo hayo ambayo kwa mjumuisho unaweza kuyaita ‘Ujanja ujanja wa mjini’ wa viongozi wa klabu hiyo ndio leo, yanaiponza klabu hiyo kumpoteza aina ya mchezaji ambaye walimuhitaji sana kwenye kikosi chao ili kujiimarisha.

  Mosi; Namna ambavyo ‘walimuenzi’ kiungo Patrick Mutesa Mafisango (sasa marehemu), pili; desturi ya kuwaacha wachezaji wa kigeni baada ya kuwasajili, hata kabla hawajaitumikia timu mfano Lino Masombo, Derrick Walullya na wengineo na tatu hadhi ya klabu yao kwa sasa ukilinganisha Yanga na Azam FC.
  Habari za kiuchunguzi zinasema kwamba Mbuyu alilishwa ‘sumu’ za kutosha ili aichukie Simba, kwanza klabu hiyo ilivyoutelekeza mwili wa marehemu Mafisango baada ya kifo chake, ambao hakuna kiongozi mkuu wa klabu hjiyo hata mmoja aliyekwenda kumzika DRC, zaidi ya Mjumbe mmoja wa Kamati ya Utendaji na mchezaji mmoja.
  Pamoja na namna ambavyo Simba hawakujali kabisa mambo mengine muhimu kuhusu marehemu Mafisango, kama arobaini yake na kadhalika, Wakongo wameichukulia hiyo kama ni dharaua na ulipotokea mjadala Mbuyu aende wapi, watu wa Kongo wakamnyooshea kidole kinachoelekeza Jangwani.
  Ikumbukwe, Mafisango aliyejiunga na Simba akitokea Azam FC, iliyomsajili kutoka APR ya Rwanda, alifariki akiwa mchezaji muhimu ndani ya Simba akiongoza kwa kufunga mabao na mwenye mchango mkubwa kwenye timu.
  Simba, hivi karibuni ilimsajili mchezaji Lino Masombo kutoka DRC, lakini baada ya mwezi mmoja na ushei ikamtema kama ilivyofanya kwa Mganda, Derrick Walullya msimu uliopita, hilo limetajwa kumsitisha Mbuyu kuangukia Msimbazi na kuamua kurudisha fedha zote alizochukua kwa Mwenyekiti, Ismail Aden Rage (dola za kimarekani 30,000 kwa mujibu wa Simba).
  Lakini pia, wakati Mbuyu anasaini Simba kuchukua fedha, alikuwa hajui kwamba katika soka ya Tanzania hivi sasa, klabu ambazo zinachuana kwa ‘utajiri’ ni Yanga, ambao Mwenyekiti wao Yussuf Manji ni mfanyaiashara mkubwa na Azam FC ambayo inamilikiwa na mfanyabiashara mwingine, Said Salim Bakhresa.
  Yanga imemsajili Twite, wakati tayari akiwa amekwishaini Simba SC, baada ya kumrudisha kwenye uraia wake wa asili, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), badala ya Rwanda aliopewa wakati akicheza nchini humo na kumbadili jina pia.
  Kwa kumbadili uraia, Yanga walipata na Hati ya Uhamisho wa Kimataifa (ITC) ya mchezaji huyo, kutoka Shirikisho la Soka (DRC), na kuwaacha Simba wakihangaika bila mafanikio kupata ITC ya mchezaji huyo kutoka FERWAFA, Shirikisho la Soka la Rwanda.
  Yanga inamsajili Twite kama mchezaji kutoka St Eloi Lupopo, klabu ambayo aliichezea kabla ya kutua APR mwaka 2006 kwa pamoja na ndugu yake, Kabange. Lakini mchezo uliochezwa hapa ni kwamba Twite alikuwa anacheza kwa mkopoAPR.
  Habari zaidi zinasema, Yanga inamsajili pia na pacha wake Mbutu (pacha wa kuzaliwa kabisa), Kabange, kwa sababu wachezaji hao kawaida yao kucheza timu moja daima.
   
 5. mapanga3

  mapanga3 JF-Expert Member

  #5
  Aug 19, 2012
  Joined: May 1, 2012
  Messages: 666
  Likes Received: 562
  Trophy Points: 180
  Ninawasiwasi na uwezo wa kifra wa viongozi wa simba
   
 6. KASHOROBANA

  KASHOROBANA JF-Expert Member

  #6
  Aug 19, 2012
  Joined: Jul 30, 2011
  Messages: 3,249
  Likes Received: 406
  Trophy Points: 180
  nimeipenda hii kitu, hawa simba wanaweweseka tu tatinane....
   
 7. KASHOROBANA

  KASHOROBANA JF-Expert Member

  #7
  Aug 19, 2012
  Joined: Jul 30, 2011
  Messages: 3,249
  Likes Received: 406
  Trophy Points: 180
  mbona povu limekujaa, nasi tutamuotesha busha bw mwakitundilo kwa wivu
   
 8. bemg

  bemg JF-Expert Member

  #8
  Aug 19, 2012
  Joined: Apr 25, 2010
  Messages: 2,706
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  tusilipe baya kwa baya bali tunamtakia mafanikio mema huko kwenye yeboyebo na arudishe pesa zetu za usajili ili siku tukiwafunga wasiseme kwamba amehujuma timu kwakulipa fadhila kwa simba
   
 9. Zamaulid

  Zamaulid JF-Expert Member

  #9
  Aug 19, 2012
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 16,363
  Likes Received: 6,701
  Trophy Points: 280
  unacheza wewe!!uchawi wa ki-congo uko juu kuliko wa kibongo,au unataka kumuona mwenyekiti wenu akiwa na mashipa!!!!ha ha ha ha ha!!
   
 10. Mzee wa Rula

  Mzee wa Rula JF-Expert Member

  #10
  Aug 19, 2012
  Joined: Oct 6, 2010
  Messages: 8,177
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  Ni sawa na kutisha vita Syria mkuu, kiukweli uchawi wa kibongo haupandi kwa wanigeria na wacongo.
   
 11. p

  pilau JF-Expert Member

  #11
  Aug 21, 2012
  Joined: Aug 16, 2012
  Messages: 1,523
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 135
  kwa taarifa yako katika vilabu hivi viwili yanga na simba uchawi wa kweli ni 1% kwani kila mechi wanazocheza ziwe za kirafiki au ligi ya aina yoyote ndani na nje ya nchi lazima waende kwa babu (kuloga) hii ndio jadi yao lakini katika huko kutafuta uchawi hawafanyi lolote bali kuchukua fedha za uchawi pasipo kuwa na uhakika wa uchawi huo. mwanachama anaweza akamchukua mjomba wake kutoka kijijini kwao mwenye sura mbaya au barakashia akamleta klabu na kuwaambia viongozi kwamba huyu ni mchawi + mganga bahu kubwa kutoka Liwale au Rufiji na viongozi hao wanaamini na kutoa fedha, kwa kuwa wao pia wana bili kubwa ya uchawi wanayoiandikia pesa kibao katika kila mechi, kwa maana hiyo wanaoweza kumshusha MSHIPA Twite siku hizi hawapo bali utapeli na kujinufaisha fanya uchunguzi utaambiwa kuna akaunti ya kamati ya ufundi sio ufundi wa kiwanjani tu bali ufundi uchawi feki
   
 12. m

  makumvi Member

  #12
  Aug 22, 2012
  Joined: Mar 26, 2012
  Messages: 93
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  MBU HUYU ATUITE!! atakiona chamtema kuni, ajue kuwa sisi hapa ni nyumbani na yeye ni mgeni hapa. cdhani kama atakuwa huru kucheza soka la kiwango kinachokubalika maana tutamzomea kila akigusa mpila maka achanganyikiwe ki saikolojia.
   
 13. b

  boby v Member

  #13
  Aug 27, 2012
  Joined: Jul 25, 2012
  Messages: 30
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Sio kishipa tu, na kumuotesha ugonjwa wa matende. Haijuwi simba huyo kwan mafisango hakuwa mkongo? Mbona alikufa kama kuku wa mdondo.
   
 14. Mkulima wa Kuku

  Mkulima wa Kuku JF-Expert Member

  #14
  Aug 27, 2012
  Joined: Jan 13, 2011
  Messages: 1,259
  Likes Received: 81
  Trophy Points: 145
  Sikujua kuwa kumbe simba inayo taaluma ya mambo ya jinsi ya uchawi? Hii inaogopesha kwenye masuala ya soka!
   
 15. ZENITH

  ZENITH JF-Expert Member

  #15
  Aug 27, 2012
  Joined: Feb 5, 2012
  Messages: 732
  Likes Received: 158
  Trophy Points: 60
  Anhaa!kumbe ni kweli walimtoa sadaka!
   
 16. Amavubi

  Amavubi JF-Expert Member

  #16
  Aug 28, 2012
  Joined: Dec 9, 2010
  Messages: 29,491
  Likes Received: 4,764
  Trophy Points: 280
  Mkuu mbona ni kama unatabiri kifo cha Mbuyu Twite!!!!!??????
   
Loading...