Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 5,354
- 18,627
Klabu ya Simba SC itapata kitita cha dola 750,000 sawa na zaidi ya Shilingi bilioni 2 (2,006,874,750) baada ya kufuzu hatua ya Nusu Fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika. Simba SC imefanikiwa kutinga hatua hiyo baada ya kuwatoa Al Masry SC ya Misri kwa mikwaju ya penati 4-1, kufuatia sare ya jumla ya mabao 2-2 (Simba SC 2-0, Al Masry SC 2-0).
Katika hatua ya nusu fainali, Simba SC itakutana na Stellenbosch FC ya Afrika Kusini, ambapo mechi ya kwanza itapigwa kati ya Aprili 20 Dar es Salaam, na mchezo wa marudiano kufanyika Afrika Kusini kati ya Aprili 27, 2025.