Simba kumkosa mbuyu twite kosa ni la rage | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Simba kumkosa mbuyu twite kosa ni la rage

Discussion in 'Sports' started by KIM KARDASH, Aug 12, 2012.

 1. K

  KIM KARDASH JF-Expert Member

  #1
  Aug 12, 2012
  Joined: Sep 21, 2011
  Messages: 5,083
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  MWENYEKITI wa Simba SC, jana amekaririwa na vyombo vya habari nchini akimshutumu mtoto wa kigogo kimoja nchini kumshinikiza Rais wa APR ya Rwanda, Meja Alex Kagame ampeleke Yanga, beki Mbuyu Twite, wakati alikuwa amekwishasaini Simba na kupewa fedha.
  [TABLE="class: tr-caption-container"]
  [TR]
  [TD="align: center"][​IMG]
  [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD="class: tr-caption, align: center"]Na Mahmoud Zubeiry
  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  Rage amelalamika sana na akapiga hatua kubwa zaidi, akaanza kuwakashifu viongozi wa Yanga, wana fedha chafu za EPA.
  Yote haya yanakuja baada ya kuzidiwa kete katika kuwania saini ya Twite. Namfahamu Rage na hii ndio desturi yake. Anapopandisha jazba huweza kusema lolote, bila ya kujali chochote.
  Kabla ya kuzungumzia sakata la mchezaji huyo, nianze kwa kumuelewesha tu Rage, asitazame boriti kwenye jicho la wapinzani wake, Yanga akasahau kibanzi kilichopo kwenye jicho lake.
  Rage anafahamu fika, mambo ambayo yako mahakamani huwa hayajadiliwi nje ya Mahakama na hakuna asiyefahamu kwamba suala la wizi wa fedha kwenye Akaundi ya Madeni ya Nje (EPA), lilifikishwa mahakamani na baadhi ya waliokutwa na hatia, hivi sasa wanatumikia kifungo jela.
  Na hivi karibuni, rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete alipokutana na Wahariri wa vyombo vya Habari nchini, Ikulu mjini Dar es Salaam, amerudia kusema juu ya hilo, kwamba serikali haimlindi yeyote na ilizikabidhi mamlaka husika zichukulie hatua hilo na kwa kuwa mamlaka hizo ni huru, hawawezi kuziingilia.
  Sasa inakuwa jambo la ajabu, Rage anapothubutu kumuhukumu mtu mwingine nje ya Mahakama juu ya EPA.
  Ni sawa tu na leo hii, atokee mtu aanze kumzungumzia yeye kuhusu dola 40,000 za Yanga za mwaka 1998 alizochukua CAF (Shirikisho la Soka Afrika) au tuhuma nyingine lukuki za ubadhirifu wa mali za Chama cha Soka Tanzania (FAT, sasa Shirikisho, TFF), atakuwa hamtendei haki, kwa sababu Mahakama ilikwishaamua.
  Awali, Rage alihukumiwa kifungo jela, kabla ya kutoka kwa msamaha wa Rais, baadaye akaenda Mahakama ya Rufaa, kukata rufaa kupinga hukumu hiyo, akafanikiwa, mahakama ikamsafisha na ndio maana leo ni Mbunge na Mwenyekiti was Simba, vinginevyo asingeweza kupata haki ya kugombea hata Ukatibu Kata.
  Naomba niwaombe radhi wasomaji wangu na Rage pia, kwa kukumbushia suala la dola 40,000 na kifungo cha Rage kabla ya kutoka kwa msamaha wa Rais, kwa kuwa natambua si busara kuzungumzia mambo ambayo yamefikishwa Mahakamani.


  MTOTO WA KIGOGO;
  Hajamtaja jina, lakini dhahiri hapa anazungumziwa Ridhiwani, mtoto wa Rais Jakaya Mrisho Kikwete. Nani asiyejua kama Ridhiwani ni Yanga na Mjumbe wa Kamati ya Uchaguzi ya Yanga na sidhani kuna dhambi katika hilo, ikiwa Waziri Mkuu wa zamani, ‘Simba wa Vita', Mzee Rashid Mfaume Kawawa alikuwa Simba.
  Simba na Yanga ni timu za Watanzania, na ndio maana Profesa Juma Athumani Kapuya, Rage mwenyewe, Waziri Mkuu mstaafu, Frederick Sumaye, Zitto Kabwe, Iddi Azzan na wengine miongoni mwa vigogo wa nchi yetu ni Simba.
  Kama Ridhiwani alijaribu kuisaidia Yanga, timu yake kuna dhambi gani, ikiwa mwaka 2005 Kapuya aliisaidia timu yake, Simba SC kutompoteza beki Victor Costa, ingawa alikuwa amesaini Yanga na kupewa fedha?
  Mimi namheshimu rais wetu, Kikwete na sidhani kama ana muda wa kushughulika na ‘upuuzi' wa Simba na Yanga- lakini kama mzazi pia ambaye anatambua Ridhiwani kijana wake naye ni baba wa familia pia, ana uhuru wake katika mambo yake. Hawezi kumuingilia.
  Yanga imepitia wakati mgumu na Kikwete yupo pale pale Ikulu na hajaonyesha hata dalili za kutaka kuwasaidia Yanga. Kikwete akiwa Ikulu, alileta kocha kwa ajili ya timu ya taifa, turudi enzi zile Rage na Samuel Sitta wakiwa CDA, walilitumia shirika hilo kwa manufaa ya timu ya taifa au Simba? Watu wanakumbuka haya mambo ndio maana namtahadharisha Rage, asiangalie boriti kwenye jicho la wapinzani, wakati jicho lake lina kibanzi.
  Mambo ya kuchafuana si mazuri na yamepitwa na wakati- Rage kama ameamua kuwa Mwenyekiti was Simba, basi apambane na changamoto zote bila ya kumnyooshea mtu kidole na kwa kweli umefika wakati Rage aachane na ‘Saisa za Majitaka', kwanza hata umri wake tu haumruhusu tena kufanya mambo kama hayo, amekwishakuwa mtu mzima sasa.
  Huyo Ridhiwani kama ndio staili yake hiyo kutisha watu, kwa nini asianzie hapa nyumbani kuwatisha viongozi wa Azam katika suala la Mrisho Ngassa wampeleke Yanga? Rage amewahi kupewa onyo kali na TFF kwa kosa la kutoa kauli za uchochezi na ajabu hajaacha, kwani kauli zake dhidi ya mtoto wa kigogo ni za uchochezi. Ni za hatari.


  SAKATA LA MBUYU TWITE
  Kama kuna mtu wa kwanza wa kulaumu juu ya Simba kumpoteza Mbuyu Twite, basi ni Aden Rage. Kwa nini? Alipofika Kigali, baada ya kumpa fedha beki huyo na kumsainisha mkataba, alijua fika na Yanga nao wanamfuatilia mchezaji huyo.
  Yanga wale wale, waliomchukua Kevin Yondan na kumsainisha mkataba, wakati tayari amesaini mkataba (kwa mujibu wa Simba) wa kuendelea kuichezea klabu yake, Simba SC.
  Ajabu Rage akijua kabisa, Yanga si waungwana, akamuacha Twite Kigali, yeye akawahi Mkutano Mkuu na baadaye shughuli za Bunge, huku nyuma Yanga wakafanya ambacho kinamsababisha leo yeye azungumze huku mapovu yanamtoka mdomoni.
  Rage alitakiwa arudi Dar es Salaam na Mbuyu Twite, apokewe na maelfu ya wana Simba halafu tungeona kama angethubutu kusaini Yanga. Rage pamoja na uzoefu wake wote katika masuala ya usajili na fitina za mpira, hapa alichemka na badala ya kutafuta mchawi, ni vema akajilaumu mwenyewe.
  Nimependa alivyomalizia mazungumzo yake jana, alisema wao watatafuta mchezaji mwingine mzuri na anachoomba tu, Simba warudishiwe fedha zao, kiasi cha dola 40,000 hivi, pamoja na gharama za nauli, kwake, mchezaji mwenyewe na mawakili waliotayarisha mkataba aliosaini Twite. Safi.


  TUACHE UHUNI KATIKA SOKA YETU:
  Soka yetu imegubikwa na mambo ya kihuni, ambayo wenyewe wanayaita ya kimjini, ambayo siku zote mimi tangu nipo DIMBA, kuanzia Mwandishi hadi Mhariri, nilikuwa nayapinga vikali, kwa sababu najua athari zake ni kuididimiza soka yetu.
  Leo Simba wakilia kuhusu Twite, Yanga watawaambia; Mnakumbuka Costa? Na bado historia inaanzia mbali tangu ya 1960, Simba na Yanga zilikuwa zinapokonyana wachezaji.
  Ila katika dunia ya leo, inayotawaliwa na utaalamu, taratibu, kanuni na sheria, kwa nini tuendelee kuyalea mambo kama haya?
  Siyo tu sijapendezewa na staili waliyoitumia Yanga kumsajili Twite, lakini pia sijapenda staili waliyotumia Simba kumsajili Ramadhan Chombo ‘Redondo', ambayo leo inawaliza Azam.
  Huo ni upande mmoja, upande wa pili, kuhonga wachezaji wa timu pinzani na marefa- hili pia silipendi na ni sehemu ya uhuni, ambao unapoteza maana halisi ya soka ambayo FIFA wanaitaka. Soka ya kiungwana. Hayo yalikuwa mapitio tu, leo ujumbe wangu ulikuwa Mh. Alhaj Rage; asikumuke EPA tu, kuna dola 40,000 za Yanga, je watu wakumbushie hizi? Nawatakia saumu njema na kwa ujumla mfungo mwema wa mwezi mtukufu wa Ramadhan inshaallah.
   
 2. steveachi

  steveachi JF-Expert Member

  #2
  Aug 12, 2012
  Joined: Nov 7, 2011
  Messages: 4,128
  Likes Received: 1,726
  Trophy Points: 280
  kwanza atoe maelezo,hela za mazishi ya mafisango kapeleka wapi kabla ya lawama zake
   
 3. K

  KIM KARDASH JF-Expert Member

  #3
  Aug 12, 2012
  Joined: Sep 21, 2011
  Messages: 5,083
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  [TABLE="class: tr-caption-container, align: center"]
  [TR]
  [TD="align: center"][​IMG][/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD="class: tr-caption, align: center"]Mbuyu akitia dole gumba fomu za Yanga. Kulia Bin Kleb
  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
   
 4. I

  Independent Voter JF-Expert Member

  #4
  Aug 12, 2012
  Joined: Jan 25, 2012
  Messages: 279
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Wapenzi na wanachama wa simba tumewahi kujiuliza maswali haya?

  1.Kwa nini habari zilivuja Mwenyekiti wa Simba SC alimpa Mbuyu Twite dola za Kimarekani 30,000, wakati sasa inaelezwa mchezaji huyo alipewa dola 10,000 tu


  2. Simba ilisema ilimuongezea mkataba Kevin Yondan, je ilimpa na fedha? Na kama ilimpa fedha mbona hazijavuja habari zozote juu ya fedha alizopewa, wakati inajulikana hadi Felix Sunzu analipwa dola za Kimarekani 3,500 kwa mwezi?


  3. Simba ilimsajili na kumpa fedha beki Lino Masombo kutoka DRC, tena inaelezwa ni fedha nyingi tu, je baada ya kumtema bila kumpa muda wa kutosha kujiridhisha kuhusu uwezo wake (mdogo au mkubwa), ili kukwepa kurudia makosa yaliyofanyika katika kumtema Derrick Walullya, fedha hizo zinarudishwa au?


  4. Ukitazama kikosi cha Simba kwa sasa utagundua wamesheheni viungo kibao, Amri Kiemba, Jonas Mkude, Christopher Edward, Mussa Mudde, Haruna Moshi, Kanu Mbivayanga, Mwinyi Kazimoto, Uhuru Suleiman, Kiggi Makassy, Salim Kinje, Ramadhan Singano ‘Messi’, Mrisho Ngassa na Ramadhan Chombo ‘Redondo’, wakati mabeki wa kati ni Juma Nyosso, Shomary Kapombe na Obadia Mungusa, (Zingatia, kiasili Kapombe na Maftah kiasili ni viungo) je, hii iko sawa?


  5. Nani huwa anashauri masuala ya usajili ndani ya Simba…Kusajiliwa au kukatwa kwa mchezaji, je anafanya kazi yake vizuri?


  6. Kitaalamu inafahamika, kumchezesha mchezaji mechi, kabla hajawa fiti kwa angalau zaidi ya asilimia 50 ni kumtengenezea mazingira ya kuumia na tumeshuhudia majeruhi wengi katika siku za karibuni Simba SC, je kwa nini Kocha Mkuu, Mserbia Milovan Cirkovick anaruhusu hali hii?
   
 5. K

  KIM KARDASH JF-Expert Member

  #5
  Aug 12, 2012
  Joined: Sep 21, 2011
  Messages: 5,083
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  [TABLE="class: tr-caption-container, align: center"]
  [TR]
  [TD="align: center"][​IMG]
  [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD="class: tr-caption, align: center"]
  PACHA; Mbuyu (kushoto) na Kabange (kulia) wanakuja Yanga
  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]

  Na Mahmoud Zubeiry
  KLABU ya Yanga ya Dar es Salaam imeifanyia kitu mbaya sana Simba SC ambacho hawataamini maisha yao yote.
  Kitu gani hicho? Ni kumsajili Mbuyu Twite na kumrudisha kwenye uraia wake wa asili, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), badala ya Rwanda aliopewa wakati akicheza nchini humo na kumbadili jina pia.
  Kwa kumbadili uraia, Yanga wamepata na Hati ya Uhamisho wa Kimataifa (ITC) ya mchezaji huyo, kutoka Shirikisho la Soka (DRC), wakati huo huo, Simba wanahangaika kupata ITC ya mchezaji huyo kutoka FERWAFA, Shirikisho la Soka la Rwanda.
  Yanga inamsajili Twite kama mchezaji kutoka St Eloi Lupopo, klabu ambayo aliichezea kabla ya kutua APR mwaka 2006 kwa pamoja na ndugu yake, Kabange. Lakini mchezo uliochezwa hapa ni kwamba, APR imemrudisha Mbuyu Lupopo akitoka kucheza kwao kwa mkopo, ambao sasa wanamuuza Yanga.
  Habari za kiuchunguzi, ambazo BIN ZUBEIRY imezipata zinasema kwamba, Simba ilimsaini beki huyo wa APR kupitia Mwenyekiti wake, Alhaj Ismail Aden Rage, kwa dola za Kimarekani, 10,000, lakini Yanga baadaye wakampandia dau.
  Habari zaidi zinasema, Yanga inamsajili pia na pacha wake Mbutu (pacha wa kuzaliwa kabisa), Kabange, kwa sababu wachezaji hao kawaida yao kucheza timu moja daima
   
 6. Blood Hurricane

  Blood Hurricane JF-Expert Member

  #6
  Aug 12, 2012
  Joined: Jun 21, 2012
  Messages: 1,151
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 145
  Huyo Mahamoud Zubery alifukuzwa gazeti la dimba kutokana na kuandika unafiki na majungu. Nini hiki sasa? Simba siku zote wastaarabu wanaona hamna haja ya kulumbana ngoja tuone huyo Twite atakavyopigana na akina Canavaro na Yondani.
   
 7. Gang Chomba

  Gang Chomba JF-Expert Member

  #7
  Aug 13, 2012
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 8,790
  Likes Received: 810
  Trophy Points: 280
  simba pia mkalipe deni lenu la chapati mnalodaiwa na yule Bimkubwa
   
 8. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #8
  Aug 13, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Zuberi hii pia unapeleka Mpoto.
   
 9. M

  Masuke JF-Expert Member

  #9
  Aug 13, 2012
  Joined: Feb 28, 2008
  Messages: 4,606
  Likes Received: 108
  Trophy Points: 160
  Kwa hiyo alitaka Rage aje naye Dar es Salaam halafu awe anazunguka naye kokote aendako ili Yanga wasimuone au alitakaje? Kosa la Rage hapo liko wapi? Ni sawa na mwanamke kwenda kumtolea mahari halafu unaanza kuzunguka naye kisa unahofia wanaume wengine watamchukua kama sio ujuha huo nini?
   
 10. Anselm

  Anselm JF-Expert Member

  #10
  Aug 13, 2012
  Joined: Nov 16, 2010
  Messages: 1,705
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  Hiyo Mahari umeilipa kwa nani,mimi nimechukua House girl huko Kijijini nimekaa naye let say mwaka,umefika bei unanipa Mahari mimi badala ya kupeleka kwa Wazazi wake? hiyo ni akili kweli?
   
 11. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #11
  Aug 13, 2012
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  Acha ujinga pesa ya Mafisango ilisha tolewa ufafanuzi labda unataka aje akutolea nyumbani kwako....
   
 12. M

  Masuke JF-Expert Member

  #12
  Aug 13, 2012
  Joined: Feb 28, 2008
  Messages: 4,606
  Likes Received: 108
  Trophy Points: 160
  Pointi hapa si kutoa mahari wapi, pointi ya mwandishi ni kwamba kosa la Rage ni kutoondoka na mchezaji, kumbuka APR wenyewe wamesikika radio one kwamba mkataba na Twite uliisha na ndo maana Rage aliongea na Twite kama mchezaji huru na shirikisho la soka la Rwanda kama wasimamizi wa mpira Rwanda, na kama hapakuwa na dili chafu kwa nini abadilishwe jina, na Lupopo wadai ni mchezaji wao wakati kachezea APR kwa miaka sita, wewe ulishawahi kuona mkopo wa miaka sita?
   
 13. m

  mahdam New Member

  #13
  Aug 13, 2012
  Joined: Aug 10, 2012
  Messages: 3
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  ama kweli hii ndio simba na yanga,hii yote ni Yanga kutafuta magoli 6 kwa nguvu zote hata kupora mchana wa jua kali!!!!
   
 14. Anselm

  Anselm JF-Expert Member

  #14
  Aug 13, 2012
  Joined: Nov 16, 2010
  Messages: 1,705
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  Hilo nakataa,huo ni mtazamo wake Mwandishi,Mwandishi kama alivyo binadamu yeyote ana mtazamo wake lkn ukiliangalia vizuri sakata la Twite unaona kabisa sehemu Rage alipokosea, na hii si mara ya kwanza hata msimu uliopita Rage aliingiza team yake hasara kwa kumtuma mtu Ghana kwenda kumalizana na Asante Kotoko akiamini kuwa ndo ilikuwa mmiliki halali wa Keneth Asamoah kipindi kile walipojaribu kumsajili,kufika kule waka'fail (hivi hili ulikuwa unalifahamu?) nashindwa kuelewa kwanini Mheshimiwa hajifunzi tu!!
   
 15. M

  Masuke JF-Expert Member

  #15
  Aug 13, 2012
  Joined: Feb 28, 2008
  Messages: 4,606
  Likes Received: 108
  Trophy Points: 160
  Kwa hiyo Rage kosa lake ni kuamini kuwa mkataba na APR uliisha au kosa lake ni nini? Wewe naona unafurahia kwa sababu ni mdau wa Yanga, lakini siku zote mimi nasema ukiona mwenzako kajenga nyumba nzuri sio lazima uvunje nyumba yake ili uchukue tofali zake nawe ukajenge nyumba yako, unaweza tumia tofali zingine na nyumba ikawa nzuri kuliko ya mwenzako.

  Hata hao Lupopo wanasema alishamaliza mkataba wa mkopo toka January sasa swali linakuja hadi July alikuwa anafanya nini APR? Sisi tunasema mmeshinda kwa Twite lakini mkubali mkatae nguvu kubwa ya pesa na madaraka ya baba yake na mtoto wa kigogo yametumika kuihujumu Simba, ungemsikia jana huyu kiongozi wa APR alivyokuwa anajichanganya ungeamini niyasemayo, sisemi haya kwa sababu mimi ni mdau wa Simba hata kama Simba wangefanya hivyo kwa timu nyingine bado ningeona ni kitu kibaya vile vile, mfano swala la Redondo kama kweli ana mkataba na Azam viongozi wa Simba hawajafanya fair, labda ni turufu wanayotaka kuitumia kuona double standard ya TFF itakavyotumika maana swala la Redondo na Yondani ni kitu kile kile.
   
 16. Ngongo

  Ngongo JF-Expert Member

  #16
  Aug 13, 2012
  Joined: Sep 20, 2008
  Messages: 12,155
  Likes Received: 3,634
  Trophy Points: 280
  RAGE kwa kubwabwaja hajambo wapenzi wa Simba hawatamsahau Simba wa Yuda [Kaduguda] yeye alikuwa muungwana sana alitumia fedha zake kuwanunulia wachezaji chapati Rage na ujanja wake wa kufungwa mpaka leo ubani wa Mafisango hajaufikisha.
   
 17. K

  KIM KARDASH JF-Expert Member

  #17
  Sep 16, 2012
  Joined: Sep 21, 2011
  Messages: 5,083
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145

  Kosa la ADEN hili hapa..."alikuja haraka haraka akazungumza na kiongozi mmoja wa FERWAFA (Shirikisho la Soka Rwanda), akapiga picha na Twite akaondoka.Karudi Dar es Salaam kwenye Mkutano Mkuu anasema amemsajili Twite, baada ya mimi kuonyesha vielelezo vya kumsajili huyo mchezaji kama mikataba na picha akiwa anasaini na kukabidhiwa jezi, akaanza kusema kuna mtoto wa kigogo, huyo mzee vipi? Mbona anakuwa muongo namna hii. Yeye aseme kweli tu, hana uzoefu na mambo haya, yeye ni mtu wa kuropoka tu, hawezi kazi,"alisema Bin Kleb.
   
Loading...