Simba inapodanganya Watanzania

Simba inapodanganya Watanzania

ili wapuuzi waamini wabayoraja kuyasikia wakuvalieni kuwa simba haikucheza au waambieni haiko afrika kusini iko kijenge..
 
Labda ni unazi wa klabu unakusumbua.lakini kiufupi kuwa hyo ling waliocheza ORLANDO JMOS ni kama capital one kule uingereza na inaonekana ni ya kawaida sana inaonekana mara nyng kikos B hupewa nafasi.
JMAMOS kwa mujbu of the news kikosi A kwakuwa ni mapumzko ya mech za kmtaifa na lig muhmu hsimama wao waLIjpma na SIMBA katka mtanange wa krafk tu kukiweka xawa kikosi KAMA MAZOEZI
 
Wana jamii forum, nikiwa kama mwanamichezo nashangazwa kuona report kwamba Simba imecheza na Orando Pirates ya Africa Kusini. Bila kupepesa macho, Orando Pirates imecheza na Black Ace siku ya 11/10/2014 na kushinda bao 1 kwa 0. Hivi wahusika hawajui kama dunia ni kama kijiji?, nn malengo ya kuwanganga wapenzi wao juu ya hili?

attachment.php


NAWASLISHA MAJBU
simba ilicheza na orlando pirates ijumaa kikosi cha kwanza kilitumika mechi ilichezwa katika dimba la rand stadium johansberg.
 
Ukikosa cha kufanya unapost ujinga tu, Azam alicheza mechi 2 siku moja huko Kagame hapa na Mtibwa sembuse Orlando!?
Nona mapovu yanawatoka kwa kuambiwa ukweli.....we unadhani Orlando ni wababaishaji kama sisi....nitafutie mechi report ya Orlando na Simba then urudu humu.
 
Mimi naamini kuna udhaifu ndani ya uongozi wa vilabu vyetu na kwa waandishi wetu wa habari.

Lakini siamini kwamba Aveva & Co. ni washenzi kiasi cha kuthubutu kutudanganya kama inavyofikiriwa.

Ninahisi:

1. Ni kweli Simba ilicheza na Orlando Pirates ya Afrika ya Kusini na kutoka 0-0, lakini si hii Orlando ya Premeir. Hata hapa Tanzania kuna Simba (na Small Simba) nyingi tu huko mitaani, au

2. Inawezekana wamecheza na Orlando Pirates yenyewe na kutoka nayo 0-0, lakini ni Orlando ya wachezaji wa akiba na wa akademia, huku wa kikosi cha kwanza wakiwa mashindanoni. Ndio maana Malinzi anasisitiza kuanzisha akademia kwa 5%, au

3. Inawezekana walicheza na timu waliyoamini kwamba ni Orlando Pirates, kwenye uwanja walioamini kuwa ni wa Orlando Pirates, lakini kumbe walicheza na kundi la wajanja fulani hivi walioona wasipoteze fursa ya kula mshiko wa nje nje. Nani kasema wenye bongo za kutapelia wako Bongo tu?, au

4. Simba hawajacheza wala hawajamwambia yeyote kwamba wamecheza na Orlando Pirates, ila wanaudaku (wanahabri?) wetu wakajua tu kimahesabu kwamba kwa sababu Simba huwa inatoa sare kila mechi, na kwa sababu awali ilisemwa kwamba wangecheza na Orlando Pirates, na kwa sababu sare pekee ambayo Simba haijatoa kwenye mfululizo huu ni hiyo ya 0-0, basi mkokotoo (calculation) rahisi ni kuwa hiyo ndiyo sare iliyopatikana. Hivyo ndivyo udaku unavyokokotolewa, au

5. Hatuwezi kujua, labda 'Kamati ya Ufundi' iliagiza kwamba ili ishinde mechi ya 18/10, Simba lazima itoe sare nyengine kabla ya hapo, hata kama ni ya kubuni, au

6. Jinsi Simba inavyoendeshwa Kisayansi, wameona wawazuge watani wao kwamba wametoka sare nyengine, watani hao wazidi kubweteka ili Mnyama awashtukize hiyo siku ya siku, au..........

7. Wamecheza lakini kwa namna kama ya yule mjumbe aliyepiga kura akitokea ulimwengu mwingine...yaani si kimwili zaidi.
 
Mkuu, si kila wakati kwamba habari isipotokea katika website ya timu husika maana yake ni kwamba hilo jambo halijatokea. Mfano mzuri ni Yanga ilipofungwa 3-1 na Simba katika mchezo wa Mtani Jembe. Pamoja na kwamba website ya Yanga kabla ya mechi iliandika kwa mbwembwe maandalizi ya mechi hiyo, habari kuhusu mechi hiyo ilivyofanyika haikuandikwa kabisa, badala yake ilikuja kuandikwa ya YM kuomba msamaha na kumfukuza kocha Brandts. Sasa kwa mantiki yako, kwa kuwa habari ya mechi yenyewe haikuandikwa, unataka kusema mechi haikufanyika?

attachment.php

Sasa ndugu hebu tuelekeze wewe matokeo umeyapata wapi maana wakati ule ulinukuu taarifa ya mipango kwamba wanatarajia kucheza. Tunaomba utuonyeshe ambapo wewe umeyapata hayo matokeo na sisi wapenzi wa timu tujiridhishe ili watani hawa wasiendelee kutupiga vijembe
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom