Allen Kilewella
JF-Expert Member
- Sep 30, 2011
- 25,158
- 48,416
Nimeona nijaribu kulijadili hili swala kimantiki bila ya kuleta ushabiki wa kitimu.
Kwanza kabisa watu wengi wanajadili Wala hawajui jinsi bodi ya ligi inavyoundwa na yenyewe inavyoendesha ligi na bodi yenyewe inavyoendeshwa.
Bila ya kujua bodi ya ligi inaendeshaje ligi na yenyewe inaendeshwaje mwisho wa siku itaishia kutoa lawama kwa wasiohusika.
Bodi ya ligi ndiyo inayoendesha ligi, sioni watu wakijadili kanuni zinazobishaniwa hutungwaje na hutumikaje na kama timu hairidhiki na jambo lolote kwenye msimu husika hutakiwa ifanye nini.
Simba ilifika uwanjani kwa ajili ya mazoezi ya mwisho kabla ya mechi yake na Yanga siku inayofuatia. Lakini yakatokea yaliyotokea ambayo kila mtu anayajua.
Pia soma: Breaking News: Bodi ya Ligi yahairisha Mechi ya Derby
Simba ikaandika barua Kwa bodi ya ligi kutoa malalamiko ya walichofanyiwa na kusema kuwa kama bodi ya ligi haitachukua hatua basi wenyewe hawatahusika na mechi hiyo.
Bodi ya ligi hatua yao ingekuwa kuamuru mechi ichezwe bila ya mashabiki tatizo lingekuwa wapi?
Lakini kwa maelezo ya bodi walipokutana wakajikuta hawana vielelezo na taarifa za kutosha kufanya maamuzi hivyo kuamua kuahirisha mechi.
Sasa wanaosema kuwa Simba iligomea mechi yake na Yanga hoja yao wanaijenga Juu ya msingi upi?
Maana ili Simba iwe imegomea mechi ni Lazima kwanza bodi ya ligi iseme mechi itakuwepo halafu Simba isifike uwanjani.
Bodi ya ligi Kwa taarifa rasmi walisema hakuna mechi, Sasa Simba ingepeleka timu uwanjani kucheza mechi gani wakati wenye dhamana ya kuendesha ligi walisema kuwa mechi husika imeahirishwa?
Ili isemwe kuwa Simba iligomea mechi ni Lazima kwanza hiyo mechi ingekuwa haijaahirishwa na bodi ya ligi.