Simba azua varangati - Mbagala | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Simba azua varangati - Mbagala

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by kilimasera, Mar 7, 2011.

 1. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #1
  Mar 7, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  WAKAZI wa maeneo ya Mbagala Kizuiani, Rangitatu na maeneo mengine ya karibu jana waliingia katika wasiwasi mwingine wa kuhofia kuondoa uhai wao baada ya Simba kuvamia maeneo hayo.

  Wasiwasi mkubwa ulitanda kwa wakazi hao kuanzia majira ya asubuhi jana baada ya kuikia ngurumo ya Simba jike likilia kwa kutoa ngurumo la kuashiria alikwua maeneo hayo.
  Wakazi hao walikumbwa na dhoruba hiyo na kufanya wakimbie huko na huko kunusuru maisha yao.

  Ilifahamika kuwa kijana mmoja aliyetambulika kwa jina moja la Abdallah alimuona Simba huyo na kupishana naye majria ya alfajiri alipokuwa akienda kisimani kuchota maji huko maeneo ya mtaa wa Kimbangulile eneo mabalo liko karibu na mto Mzinga.

  Kwa mujibu wa maelezo ya Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa huo Bw. Kessy zilisema kuwa awali baadhi ya watu walimuona Simba huyo lakini hawakuweza kuthitisha kutokana na giza lililokwua limetanda lakini kadri kulivyozidi kupambazuka ngurumo zake zilizidi kusikika na wakazi wa maenejno hayo kubaini kuwa walikuwa na mnyama huyo katika mtaa huo.

  Hivyo kutokana na hilo kijana mmoja aliyetambulika wka jina la Nassoro Allly alianza kumfurumusha Simba huyo kwenye gofu la nyumba dambalo lilikuwa halijamalizika kiujenzi ambako alikuwa amejificha na hatimaye alimruki maeneo ya shingoni na kujeruhiwa vibaya na simba huyo.

  Alisema baada ya kuhakikisha ukweli huo alipiga simu polisi kwa msaada zaidi ambapo askari watano wa Kituo cha Polisi Kizuiani walifika hapo majira saa 1:30 na kuanza kumsaka kwenye maficho yake na kumpiga risasi bila mafanikio kutokana na bunduki aina ya SMG kuonekana kutomudu kumuua mpaka zilipotumika silaha kubwa zaidi

  Alsiema samba huyo aliweza kuuwa majira ya Saa 2 asubuhi na wananchi wa maeneio hayo kupiga shangwe kwa kufanikiwa kuuawa kwa sima huyo.

  Hata hivyo NIFAHAMSIHE iliabarishwa na mpasahji habari aliyekwua eneo la tukio kuwa kioja kilitokea wka wakazi hao kuonekana kuanza kufanya fujo kugombania viungo kwa matumizi yao wanayoyafahamu huku wengine wakidai kutaka kuchukua nyama na vurugu ikatanda maeneo hayo hadi askari polisi walipowatawanya wananchi hao kwa kurusha risasi hewani na kukimbia ambapo awali walilizingiri gari la polisi lililobeba mnyama huyo.


  Hata hivyo baadhi ya wakazi waliokuwa wastaarabu waliendelea kufanya fujo hizo na hatimae walienda hadi kituo cha polisi cha Kizuiani kwa maandamdano na kuimba nyimbo 'tunamtaka simba wetu', wakijaribu huku wakijaribu kumchukua kwa nguvu simba huyo hivyo polisi walilazimika kumepelekea kusikojulikana
   
 2. L

  Leornado JF-Expert Member

  #2
  Mar 7, 2011
  Joined: Nov 12, 2010
  Messages: 1,534
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Simba kweli?? Dar es salaam kuna mbuga maeneo jirani? au katoroka zoo? au ni binadamu alikuwa kajibadilisha kuwa simba? au ni wa JK?

  maana bongo kila kitu possible.
   
 3. AK-47

  AK-47 JF-Expert Member

  #3
  Mar 7, 2011
  Joined: Nov 12, 2009
  Messages: 1,381
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Yaani tatizo kwetu Mbagala hapa bomu huku simba
   
 4. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #4
  Mar 7, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,496
  Likes Received: 19,903
  Trophy Points: 280
  hahhaha inabidi diamond a edit nyimbo yake ile aweke na simba na mabomu
   
 5. k

  kituro Senior Member

  #5
  Mar 8, 2011
  Joined: Dec 25, 2010
  Messages: 176
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35

  jamani huyu jk sasa anaonewa! hata simba ni wa jk?. jamani mnyonge mnyongeni lakini hakiyake mpeni!.

  wananchi wa mikumi waishio pembezone mwa hifadhi ya mikumi wamekuwa wakivamiwa na wanyama tokea hata kabla ya uhuru lakini miaka hii wanasema ni serikari ya ccm. ndugu tuangalie na vitu vya kuwarushia ccm na si kila kitu!.
   
 6. Obuntu

  Obuntu JF-Expert Member

  #6
  Mar 8, 2011
  Joined: Feb 6, 2008
  Messages: 512
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Uswahilini kuna vituko...
  Hivyo ni vituko vya Uswahilini..
   
 7. M

  Mgalatia JF-Expert Member

  #7
  Mar 8, 2011
  Joined: Nov 28, 2007
  Messages: 297
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Nijuavyo ni kuwa simba wanaonekana sana latika vijiji vya mkuranga kwa hiyo si ajabu kuonekana mbagala.:rain:
   
 8. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #8
  Mar 8, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  ila mbagala ni town kabisa alipitapitaje mpaka akaingia mjini na kuanza kukatisha vichochoroni
   
 9. Tram Almasi

  Tram Almasi JF-Expert Member

  #9
  Mar 8, 2011
  Joined: Feb 26, 2009
  Messages: 755
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Kijana aliyejeruhiwa na simba huyo anaitwa Yasin Hamis Mussa(42)na amelazwa wodi na 17 sewahaji Block ambayo ni wodi ya Taasisi ya Tiba ya Mifupa(MOI). Kwa mujibu wa msemaji wa Taasisi hiyo,Bw. Alikuwa na majeraha sehemu mbalimbali za mwili lakini zaidi ktk shingo na mikononi.
  Na kwamba majeruhi anaendelea vema.
   
 10. Gama

  Gama JF-Expert Member

  #10
  Mar 9, 2011
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 9,223
  Likes Received: 1,412
  Trophy Points: 280
  we kilimasera, si umeambiwa alionekana karibu na mto mzinga! Hujui kuwa Mto mzinga unatokea mkuranga?!. Anyway, ni jk alimleta ili tusahau machungu yanayotupata tufikiri kuwa ni mazingaombwe?‎؟‎?‎؟‎?‎؟‎?‎؟‎!!
   
 11. L

  Leornado JF-Expert Member

  #11
  Mar 9, 2011
  Joined: Nov 12, 2010
  Messages: 1,534
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  umeona eeh, hata mi nilijua atakuwa katumwa na JK. JK anavyotuchukia angeweza angetuma hata bomu la nyuklia mbagala, cjui tumemkosea nini.
   
Loading...