Damaso
JF-Expert Member
- Jul 18, 2018
- 6,132
- 10,514
Ndondi ni mchezo mzuri sana kama hakuna ndugu yako ulingoni ila kama kuna ndugu yako basi si burudani ya mzaha; ni mchezo unaobeba hatari inayoweza kubadilisha historia ya maisha ya mtu kwa sekunde chache.
Uliza familia ya Marehemu Hiromasa au familia ya Segun Olanrewaju ambao walikata moto kizembe kizembe tu kama masihala vile. Mtoto kautaka na akaupata, wakati akidhani atakutana na pambano kama la Tyson akakutana na mwamba akiwa hana masihala kabsa ulingoni. Skyports walitoa msimamo wao kuwa “it’s going to be a suicide unless AJ knows what he is doing”.
Kwenye pambano kati ya Anthony Joshua na Jake Paul—tunaona somo kubwa kuliko matokeo yenyewe. Alichokifanya Jake Paul ni sawa hadithi ya simba kukutana na kiboko kwenye maji: mazingira yasiyo sahihi, ujasiri usio na mizani, na adhabu isiyojali jina. Simba ana hatari zake ila akiingia kwenye maji kupambana na boko huwa ni stori nyingine.
Baada ya Jake Paul kuonja ushindi dhidi ya mpinzani mstaafu, fikra zikachochea ndoto ya kukabiliana na wanandondi hai wa uzani wa juu na management yake ikaona ni sahihi kabsa kwenda kukubali pambano na AJ. Ndoto hizo, katika simulizi hii, ziligeuka kuwa funzo kali.
Ndondi si mchezo wa majaribio au mzaha; ni taaluma yenye misingi ya nidhamu, uzoefu na heshima kwa hatari. Ndani ya ulingo, kila ngumi hubeba historia ya mazoezi, makovu ya zamani na uamuzi wa papo kwa papo, ndio maana sio ajabu kuona watu wakipoteza maisha ulingoni.
Majina kama Hugo Santillán na Patrick Day yanabaki kuwa kumbukumbu nzito—si kwa kushinda au kupoteza, bali kwa gharama ya juu ya mchezo huu. Ni mapambano yanayotukumbusha kuwa ulingo ni eneo la mapambano halisi, kama vita ndogo zilizoidhinishwa, ambapo makosa hulipiwa kwa afya, au zaidi.
Hapo ndipo kauli kwamba bondia “ana leseni ya kukutoa uhai” inapopata uzito wake halisi, dancing assassins* ingawa kwa watu kama **Jake Paul wanaona ni kama mzaha.
Miaka ya 70 mpaka 80 hakuna mtu wala bondia alitamani kukutana na Joe Frazier ama Trevor Berbick, hawa jamaa kukusaidia kuyaona malango ya mbinguni ni sekunde chache sana ulingoni.
AJ, katika muktadha huu wa anawakilisha uzoefu wa muda mrefu: mpiganaji aliyewahi kuwazima mabondia kama Charles Martin, Kubrat Pulev, Robert Helenius pamoja na Francis Ngannou.
AJ sio mtu wa kuchezewa na yeye binafsi amekuwa akiwakumbusha watu kuwa bondia haswa wa uzito wa juu amepewa leseni ya kutoa uhai. Ndondi hazitambui umaarufu wa mtandaoni wala hadhi ya burudani; zinatambua tu ulinzi, muda, na nguvu ya mikono.
Pole bwana mdogo Jake Paul, umepata majeraha ya kuvunjika taya mara mbili, ila picha yako kabla AJ hajakukalisha chini imekuwa meme mitaani huko na imetosha kuonesha kuwa uzito wa heavyweight sio uzito wa kitoto.
Jake Paul ni simba ila tatizo uliingia kwenye mto ambao ndio makazi ya boko, na ambacho umefanywa kitakuwa ni mfano bora kwa wenzako kina KSI kuwa kina AJ, na Deontay sio sample specimen.