majoto
JF-Expert Member
- Jul 19, 2013
- 2,751
- 5,340
Hivi mimi ni wa kumhonga mwanamume? Loh hivi nimepatwa na nini? Mwenzenu najishangaa sijawahi honga kidume chochote na si utaratibu wangu hata siku moja! Cha ajabu nimeangukia eti kwenye penzi, kidume hakina kazi, nakipa nauli, pesa ya kula, ya dawa na nguo nakinunulia! loh najishangaa nimekuwaje mie???? Najua vidume vitapiga kelele lakini ukweli utabaki pale pale, nimezaliwa mwanamke nastahili kupata huduma zote kutoka kwa mwanamume, nastahili kulelewa na sio kulea kidume chochote! Ndio je, ... mnataka kubisha, nyie bisheni tu ila nahitaji kukiondoa hiki kilichoniingilia na kupelekea mimi kuhonga kidume! eti penzi; loooo penzi gani la kulea dume zima lenye nguvu zake.
Kama kupenda ndio huku sitaki tena, nahitaji kuwa freee, nahitaji kupenda atakayenitunza na kunirusha rusha kwenye bahari ya maraha niufurahie uanamke wangu. Potelea mbali acha niliue hili penzi ingawa limenikaba koo maana kidume kiroho changu kimeridhika ila akili yangu haikubali kabisa... nitajitahidi niliepuke nipumue mtoto wa kike loH! nisaidieni jamani ili hiki kiroho changu kiache kupenda janga, yes, hili ni janga kwangu maana bajeti zangu zinaharibika kisa kuhudumia kidume... uwiiiiiiiiiiii