Siloam church

To be honest nilishawahi kufanya maombi na hawa watu!
Yaani sikuwaelewa kabisa,kwanini kwenye maombi halitajwi jina la Yesu wala damu ya Yesu? Instead anatajwa mjumbe WA mapenz ya mungu sijui eliya Mara tebethi,Mara damu ya haki kweli na hukumu,ndo IPI hyo?!
Sikuelewa na nikaenda kuomba toba kwa kufanya nao hayo maombi manaake unaweza kuingizwa chaka kuabudu usichokujua hivihiv
 
Mkuu BT in kwa wale waaminio na kumfuata
Sio eti ndo tuendelee kutenda dhambi kisa zilishalipiwa gharama bila toba no...lazima utubu na umpokee kuwa Bwana na mwokozi wako hapo ss unakuwa umelipiwa

Acheni kufanya mambo ya kawaida magumu. Yesu alituweka huru bila masharti yoyote,alijitoa kwa hiari yake bila masharti yoyote akalipa garama ya dhambi na kufuta dhambi kwa wamwaminio.

Yesu alisema kumkubali tu unakua huru na dhambi,unakua huna hatia na dhambi. Hakuna dhambi duniani yesu alishafuta zote.
 

Kwa hiyo imani yenu ni sawa na ISIS, Boko Haramu, Osama nk.? Tupe mahusiano ya makundi hayo na uislam wako.
 

Sasa unashangaa nini kuhusiana na "wakristo", sio kila anayejiita mkristo/mkristu huyafuata mafundisho ya Yesu Kristo mwana wa Mungu.
 

Maana wewe hata Roho Mtakatifu hujampokea, naona tayari uko kwenye imani potofu, fanya haraka utafute kanisa litakalo kupatia mafundisho sahihi ili usalimishe roho yako.

Usiende Siloum, maana hawa sio wakristo kwa imani yao. Na haimaanishi kwamba kila anayetumia Biblia katika mafundisho yake anaamini katika kristo, mfano waislamu wengi hutumia Biblia katika mafundisho yao japo kwa namna ya kupinga.
 

Siloam sio wakristo.
 

Wajumbe wa shetani sio lazima wawe na pembe. Yesu alikuja kukufungua kutoka gereza la dhambi na hukumu ya dhambi ukiwa chini ya mamlaka ya Shetani, akiisha kutoa huko anakuingiza kwenye nuru na kukupa uwezo wa kuukataa ubaya. Sasa kama wewe unang'ang'ania kurudi gereza la Shetani unataka Yesu afanyeje. Wokovu haulazimishwi kwa mapanga na kuchinja watu.

Hivi wafungwa wakifunguliwa gerezani humaanisha wamewekwa huru kufanya makosa ya kijinai. Usipotoshe watu na kumtafutia shetani wafuasi.
 
Naona hakuna tofauti ya Mola wa Babu wa Samunge na kiongozi mkuu wa siloam aliyekufa na kwenda hukumuni(WAEBRANIA 9:27)

Soma mistari michache ya Mathayo 24:

4 Yesu akajibu, akawaambia, Angalieni, mtu asiwadanganye.

5 Kwa sababu wengi watakuja kwa jina langu, wakisema, Mimi ni Kristo; nao watadanganya wengi.

11 Na manabii wengi wa uongo watatokea, na kudanganya wengi.
 

Toba ni nini...?
 

Hahahaha kwakweli hiki ni kipindi cha mwisho
 
Kwa hiyo imani yenu ni sawa na ISIS, Boko Haramu, Osama nk.? Tupe mahusiano ya makundi hayo na uislam wako.

Hujauelewa huu mjadala, mimi sizungumzii taasisi au mtu, kinachozungumzwa hapa ni kwamba kwenye uislam hakuna mahedhebu, full stop, sasa ukianza kuniambia habari za ISIS, BAKWATA au AL-QAIDA nenda kawaulize wenyewe kwa maana hizo ni taasisi ambazo kila moja inamalengo yake.
 
Sasa unashangaa nini kuhusiana na "wakristo", sio kila anayejiita mkristo/mkristu huyafuata mafundisho ya Yesu Kristo mwana wa Mungu.

Mi sishangai ila nimeeleza uhalisia katika dini ya uislam, sasa kama ni hivyo, ndio uniambie wewe sasa kati ya madhehebu yenu ya kikristo zaidi ya 3,000 duniani, ni dhehebu lipi linafuata mafundisho ya yesu na lipi halifuati!
 
Itafute kweli ikuweke huru, kubaki kwenye kanisa lako la "kimwili" hakukuhakikishii usalama wa roho yako.

Kweli haitafutwi kwa kuhama makanisa bali inatafutwa kutokana na nia ya ndani ua kumjua Mungu na Neno lake na kulitenda pasipo sahau kumwomba akusaidie....Sidanganyiki ng'oo! Wala simtuzi muhubiri jukwaani.
 
Kweli haitafutwi kwa kuhama makanisa bali inatafutwa kutokana na nia ya ndani ua kumjua Mungu na Neno lake na kulitenda pasipo sahau kumwomba akusaidie....Sidanganyiki ng'oo! Wala simtuzi muhubiri jukwaani.

Hiyo kweli uliyoipata yaweza kuwa inatokana na udanganyifu wa moyo wako maana kama unayabeza mambo ya rohoni hiyo kweli ya Mungu unaipataje? Kumbuka Mungu ni Roho.
 
Mi sishangai ila nimeeleza uhalisia katika dini ya uislam, sasa kama ni hivyo, ndio uniambie wewe sasa kati ya madhehebu yenu ya kikristo zaidi ya 3,000 duniani, ni dhehebu lipi linafuata mafundisho ya yesu na lipi halifuati!

Mwamini Bwana Yesu kuwa ni Mungu na kwamba aliacha utukufu wake Mbinguni na kukubali kuzaliwa kama mwanadamu ili afe na kuchukua adhabu ya dhambi zako. Huyu Yesu alifufuka na alirudi Mbinguni kwa babaye. Sasa, muombe atakujulisha inakupasa kufanya nini.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…