Angelicious
JF-Expert Member
- Apr 5, 2012
- 869
- 499
Nahisi jana baridi imeniingia kifuani. Kinauma. Sasa bwana ukinichekesha hivi ujue unanisababishia maumivu?
dah! nimeipenda hii mada mana hawa watu wana vituko yataka uvumilivu kuishi nao
mimi kuna mmoja alikuwa hali chakula cha usiku tumekaa naye miaka 4 lakini hata siku moja
hajawahi kula nilikuwa namshangaa tu
mwingine naye ulikuwa ukimtuma dukani au gengeni kama kumefungwa anakaa chini anamsubiri
mwenye duka au genge mpaka aje ndo anunue ulichomtuma
huyu mwingine naye alikuwa mtu wa mood siku akiamua haamki kufanya kazi ukimuuliza
anakwambia kazi nilizofanya wiki hii zinatosha ila alikuwa anapenda kufagia uwanja yeye muda wote na fagio loh!!!!
hilo la kuoga na kufua nguo zao naona ni janga la kitaifa mana mpaka uwakumbushe
Sweetheart nikuambie kitu? This made me very very sad. Its like a wake up call. My son is 18 months and 2 weeks. Nimeamua kumchukua cousin yake kutoka boarding nikae nae. For his own good since wazazi wao wameshaachana na pia for my son's sake.
My little man hawezi kuongea asimulie anything bad akifanyiwa. But with his cousin around it might help things.
Hawa watoto bwana. Mungu tu awalinde.
ila Karucee hao wako ni kiboko, badilisha sehemu unayowachukua
Mi kuna mmoja wakati wa kula alikuwa anajitenga anakaa nje peke yake. kumbe nyama zote anaweka kwenye sahani yake watoto wangu wawili anawapa finyango moaja moja
mwingine nilikuwa nikimsemesha/ kumpa maelekezo, ananifokea ananipandishia sauti juu kama mtoto wake. halafu alikuwa kapanda juu, mwili mkubwa. lol, nikaona nitakuja kudundwa home kwangu mwenyewe, nikamtimua
mwingine kuzurula kutwa kwa majirani. kwangu kuna geti. siku narudi toka job nakutana nae getini anatoka kabeba sufuria.nikamuuliza unaenda wapi na hiyo sufuria ndani ina ngano, akajibu anaenda kukandia maandazi ya chai kwa mama fulani huku wanapiga story
Niliyenaye sasa ana ugonjwa wa kucheka,hata mtoto akimsalimia anacheka tu tena kwa sauti.
kuna nyingine ya bamdogo wangu aliletewa housegirl kutoka huko Iringa
ye kumbe wala hafanyi kazi zozote analala huyo vibaya sana akiamshwa haamki hata
lakin wakiamka wanakuta kila kitu kimefanywa wanajiuliza huyu kafanya saa ngapi.......
huwa anachelewa kulala wakajua may be usiku ndio huwa anafanya lakin mmh asubuhi utamwamsha
we haamki unaweza hata kumwagia maji ndio ashtuke baadae wakaanza kumfatilia ndio akawaambia
ye akilala wao ndio hua wanafanya hizo kazi na muda anaaamshwa hua wanakua kwenye vikao vyao
sijui na bibi yake alirudishwa fasta kwao
Sometime huwaga najiuliza are they serious? Haya ni mambo ambayo nimejionea kwa wadada wangu wa home. lols.
1. Kuweka nguo na viatu kwenye fridge bovu.
2. Kutengeza juice ya passion kwa kublend kila kitu. Yes. Aliosha tu akatumbukiza kwenye blender. Tukawa tunajiuliza huu wekundu umetoka wapi. Tulipoenda kwa wakwe akawatengezea hivyo hivyo. Siku nimeenda wakaniomba nitengeze juice kama mtego. Lols. Ndo wakaniambia flani alitengeza hivi na hivi. hahaaa.
3. Kujaribisha nguo zangu na viatu, wigs etc na kujipiga picha.
4.Kuna mmoja alikuwa hapendi wageni, so mtu akija kuniulizia anasema sipo. Sasa nikaja kugundua much much later watu mtaani washanimaindi bila mi kujua.
5. Kuna mmoja alikuwa anaenda kunyonya maziwa directly kutoka kwa ng'ombe wa jirani. Aisee huyu I fired immediately.
6. Kuna mwingine alikuwa anapanda ukuta kwenda kwa jirani kuiba machungwa. Sikujua mpaka siku dirisha limevunjwa. Kumbe walikuwa wanamrushia mawe kama ka nyani. lols. I was furious. Aibu zingine bwana!! Kama vile siwezi ku afford chungwa?!
&. I had another one kuoga kwake mwiko!! Halafu kipindi kile I was so so busy. Nikawa siwezi kumfatilia. Nilipokuja kustuka ikabidi nim force aoge. Wapi? Atajipaka majo usoni mikononi na miguuni. Atamwaga maji ukutani weee.
9. Nilipoenda kujifungua house help wangu aliita bf wake wakaniibia mandoo ya rangi, mafeni ambayo hayakuwa yamefungwa, maboksi ya tiles etc etc. Damn!!
10. Kuna mmoja ambae mtoto wangu alikuwa anamuogopa kweli. Nikitoka kazini nakuta mtoto kwenye kona amejikunyata. Back then kalikuwa ma miezi 9. He was gaining weight na wakwe walimpenda sana. But siku ya siku akamwambia mtoto 'shenzi wewe mamako yupo sikufanyi chochote'. I told her to leave immediately.
Haya, wewe yamekukuta yapi?
Alimuiga mama mwenye nyumba!!!