Silly things househelps do

Karucee

JF-Expert Member
Joined
Mar 11, 2012
Posts
18,196
Reaction score
34,502
Sometime huwaga najiuliza are they serious? Haya ni mambo ambayo nimejionea kwa wadada wangu wa home. lols.

1. Kuweka nguo na viatu kwenye fridge bovu.

2. Kutengeza juice ya passion kwa kublend kila kitu. Yes. Aliosha tu akatumbukiza kwenye blender. Tukawa tunajiuliza huu wekundu umetoka wapi. Tulipoenda kwa wakwe akawatengezea hivyo hivyo. Siku nimeenda wakaniomba nitengeze juice kama mtego. Lols. Ndo wakaniambia flani alitengeza hivi na hivi. hahaaa.

3. Kujaribisha nguo zangu na viatu, wigs etc na kujipiga picha.

4.Kuna mmoja alikuwa hapendi wageni, so mtu akija kuniulizia anasema sipo. Sasa nikaja kugundua much much later watu mtaani washanimaindi bila mi kujua.

5. Kuna mmoja alikuwa anaenda kunyonya maziwa directly kutoka kwa ng'ombe wa jirani. Aisee huyu I fired immediately.

6. Kuna mwingine alikuwa anapanda ukuta kwenda kwa jirani kuiba machungwa. Sikujua mpaka siku dirisha limevunjwa. Kumbe walikuwa wanamrushia mawe kama ka nyani. lols. I was furious. Aibu zingine bwana!! Kama vile siwezi ku afford chungwa?!

&. I had another one kuoga kwake mwiko!! Halafu kipindi kile I was so so busy. Nikawa siwezi kumfatilia. Nilipokuja kustuka ikabidi nim force aoge. Wapi? Atajipaka majo usoni mikononi na miguuni. Atamwaga maji ukutani weee.

9. Nilipoenda kujifungua house help wangu aliita bf wake wakaniibia mandoo ya rangi, mafeni ambayo hayakuwa yamefungwa, maboksi ya tiles etc etc. Damn!!

10. Kuna mmoja ambae mtoto wangu alikuwa anamuogopa kweli. Nikitoka kazini nakuta mtoto kwenye kona amejikunyata. Back then kalikuwa ma miezi 9. He was gaining weight na wakwe walimpenda sana. But siku ya siku akamwambia mtoto 'shenzi wewe mamako yupo sikufanyi chochote'. I told her to leave immediately.

Haya, wewe yamekukuta yapi?
 
Hahaa...mm bwana naomba nisiseme maaana kuna wanaopandwaga na mapepo hadi ambao hawajipendi au hawajitaki kiasi hawaogi wala kufungua nguo zao
 
Hahaa...mm bwana naomba nisiseme maaana kuna wanaopandwaga na mapepo hadi ambao hawajipendi au hawajitaki kiasi hawaogi wala kufungua nguo zao

Mnnnnh! Mimi hao wa mapepo sijaona! Nashkuru kwa kweli manake dah!! I have a little boy wasije kumdhuru.
 
Usiniambie alivunja nazi akablend pia ili kuepuka kuikuna?baadala ya machicha:shocked:
Ngoja nikuambie, kupata dada mpya mpaka aje mukae sawa inachukuaga time kweli. Na energy aisee. Ni kazi juu ya kazi.

Yet we cannot do without them.
 
Hahaha,hyo ya kujaribisha nguo za watu imenikumbusha kipindi niko boarding beki3 anafukunyua kabati anatinga viwalo vyangu weee hadi wamama wa street ndo wakamstua mama akampiga stop,
-mwingine alikuwa analewa kistaarabu (km bia 3 au 4 )mchana afu analala,anaamka kupika sa 12 jioni
-mwingine alikuwa anaflirt na shamba boy anaengalia ng'ombe,basi anamkaribisha ndani na anampelekea chai sebuleni kama wapo kwao vile,
-mwingine alikaa siku 2 akakomalia kusepa kisa tunaondoka anabaki mwenyewe siku nzima,
-huyu mwingine house boy,hana kituko wala shida yoyote,kazi zotee anafanya, lakini alikuwa hakasiriki jmn,tumekaa nae almst 3 yrs ye ni wa kucheka tu
ila wanasaidia sana hawa,ukirudi home u got a chance walau to relax
 
Nimeipenda hii mada nami nina visa vyao vingine ni most recent kabisa
Mmoja ilikuwa kila tukimaliza kula na kutumia toothpick yeye anazirudisha for reuse !mtoto ndio alikuja gundua

Mwingine alichukukua xpel dawa ya mbu akajipulizia kama pafyume

Hiii ni mwezi uliopita tu
Alikuja mgeni nikamuita dada amhudumie kinywaji chochote ,mgeni akataka soda ya tangawizi
Mara tukaona dada kaweka kwenye sahani kisu kidogo kipande cha tangawizi na maji ya kunawa mikono

Mwingine alikuwa na appetite ya kufa mtu na ukimpa apike nyama hakikisha unaongeza na nusu kilo ya kuonja la sivyo mtakula na mchuzi tuu ,na akishatenga chakula kama mkichelewa dk moja tu mnamkuta mwenzenu keshajipakulia tena lumbesa

Huyu mwingine yeye alikuwa mwanga hakai kwenye kochi anakaa chini kwenye pembe halalu na nguo na alikuwa analala uchi wa mnyama alikuwa anakula ugali pekeyake halafu mboga pekeyake alikuwa hapendi kabisa nyimbo za dini
 
Hao wa hivyo tushawazoea kuna huyo mmoja me nilipata ni balaa tumekubaliana vizuri amekuja siku ya pili tu asubuhi akaaga anaenda kanisani me nikamjibu sawa, nikajua ndo zile misa za asubuhi na kanisani si mbali na nyumbani so kwanini nimnyime uhuru wa kuabudu.

Aisee alirudi saa moja jioni, kumuuliza ananielekeza kanisa aliloenda na kwamba yeye kaokoka, duh sasa nikawa namuuliza wewe mgeni umejuaje kanisa la mbali vile, hakuwa na jibu, nilimsamehe huwa sipendi kumkosesha amani mdada.

Siku ya pili bila aibu kaniaga tena, sikutaka kumkatalia nikajua may be atawahi leo, na hapo anavyoondoka inakuwa saa kumi na moja na nusu au saa kumi na mbili, hafanyi kazi hata moja. Jamani! Karudi tena saa moja jioni sikumsemesha na akifika anaingia jikoni anaangalia chakula then anapumzika.

Iliendelea hivyo wiki nzima, nikashindwa mwenyewe, siku hiyo ananiaga nikamwambia beba na nguo zako uende nazo maana huna unachonisaidia labda ulitaka sehemu ya kukaa tu, na kama ni hivyo bora ungeniambia mapema niamue ukae au usikae, akalia lia pale ila mwisho wa siku akaondoka
 
Daaa umunikumbusha the time being Nipo boarding walileta mdada maisha yetu ya kupanga haya akawekwa rum kwangu alivaa nguo zangu hadi alipogunduliwa was too late

Hicho kitabia cha kuweka viatu vyake nje or kweny friji mbovu ni wengi, pia kujaribisha viatu au nguo kuona kama amependeza

Wengi wanapenda kula wenyew ila ukiwa na sheria mda wa mezani ni lazima kila mtu awepo ndo utaweza kumbana cos mda wa msosi yeye ndo atajifanya yupo busy kuhamisha viatu nje, Mara nguo nk
 
M nakumbuka akikasirika tu atafagia mende atawamwagia kwenye mboga,akiweka mboga mezani af anawafukia mende chini,ukichota tu mboga unakutana na mende.

Mwingine kila akibeba mtoto lazima amwangushe,ukimuuliza mtoto analia nini anajibu sijui ananjaa! badae nundu inatoka unajua dogo alibwagwa.

Mwingine anaoga midawa ya kienyeji kila siku, tatizo nini,wanaume hawamuiti wala salam anatoa nuksi.akatimuliwa
 
Niliyenaye sasa ana ugonjwa wa kucheka,hata mtoto akimsalimia anacheka tu tena kwa sauti.
 

Mmh aise huyo hafai kabisa yani anatupia mende kwenye msosi ptuuuu!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…