Silent killers

Silent killers

KIUNGOMCHEZESHAJI

Senior Member
Joined
Oct 4, 2013
Posts
120
Reaction score
255
Kuna watu wanaitwa "Silent Killers", au "Simba mwenda pole..." Umeshawahi kujiuliza kama kuna watu wa aina hiyo kwenye jamii au sehemu ulipo? Watu wa aina hii, wana pande 2 za shilingi. Kama hauko very close na yeye, na kama hakushirikishi mambo yake, unaweza ukasema waoooooow, mtakatifu si ndo huyu. Kama ni mwanamke utamwita mama Mchungaji.

Kama ni ME utamwita mchungaji au askofu. Ni mpole, mwenye staha, anaongea kwa hekima, hanywi pombe, havuti sigara, hutamwona akiongea hovyo mambo ya wanawake na hutamwona na mwanamke huko mtaani. Wako serious muda mwingi, na hawaruhusu watu wajue in and out ya maisha yao.

Wengi huishia kujua official view yao. Ni wachache sana wanaowajua hawa watu kuhusu upande wa pili wa maisha yao. Ukija kusiimuliwa unaweza ukasema jamaa anasingizia..

Hivi karibuni kuna wafanyakazi wapya waliajiriwa, miongoni mwao walikuwepo akina dada fulani. Baadhi yao kwa kweli walikuwa warembo haswaaa, kila mwanaume timamu lazima pale mshipa wa mapenzi uliamka "Paaaaah". Sasa vijana wakaanza makeke yao kurusha karata kwa dada hawa.... aaah wapi, hakuna inayonasa. Mwishowe wakaleta visingizio, eti mabosi watakuwa wamekula, wengine wakasema aaah, hawa watoto hawaingiliki walokole sana.

Sasa kuna mmoja wetu sisi wakongwe tunamfahamu sana, tunamwita simba mwenda pole, au Silent killer. Jamaa hana papara na huwezi kujua kama ana malengo yoyote ya kumtokea demu. Ila ukisimuliwa mademu anaotoka nao ni hatareeee, ni sheeeedah. Wazuri sana, waliotulia, wanaojiheshimu sana.

Basi bana hivi majuzi kukawa na sherehe ya wafanyakazi kumaliza na kukaribisha mwaka mwingine wa kazi. Vijana wakajipanga kimkakati, wakati wa kuanza safari basi wakahakikisha wamekaa siti moja na hawa dada. Mbwembwe nyingi. Silent killer (SK) kumbe alishalenga shabaha yake, alibakiza tu kuachia kombora. Na SK alishapanga siku hiyo ndo ataachia kombora na gemu kuisha.

Yeye wala hakuhangaika na usafiri. Akawaacha watangulie. Yeye kaja na usafiri wake. Shughuli ilipoanza, madogo wakaanza mara vinywaji, jiuce, maji, pombe etc, hawakai mbali na mabinti hawa. SK yeye hagusi pombe, ni juicee na maji kwa kwenda mbele. Watu wakaanza kupiga selfie na smartphone zao, yeye katulia, akisimama anapiga zilizo muhimu tuu anarudi katulia.

Mara watu simu zikaanza kuisha chaji, SK yeye yuko full na powerbank. Madogo wakabloo. Huyo binti ambaye SK alimlenga naye kumbe simu haikuwa na Megapixel kubwa haipigi picha vizuri, alafu chaji ndo hivo inaisha. Akaona isiwe tabu, kavuta kiti kaenda kukaa na SK. Msosi ukaendelea, binti akaomba SK ampige picha alafu atamrushia. Sk akaanza yake hapo. Baadaye kumrushia, ikabidi binti atoe namba ili amrushie kwa whatssap.

SK akazirusha, binti anasema kifurushi kimeisha, SK karusha credit. Binti anajisogeza. Shughuli ikaendelea. Sasa vijana wakaanza kumind eti SK ni married lakini bado anatubania. SK na binti story kwa kwenda mbele, hapo anapiga story za kawaida tuu, za kiutu uzima zimetulia heshima na adabu. Masikini binti kumbe ndo hvyo anaenda na mkondo wa maji. Ukawadia muda wa kucheza, SK yeye wala hachezi, akinyanyuka kucheza anastua kidogo anarudi zake kukaa.

Saa ya kuondoka kurudi town, usafiri wa kugombania kwa sababu kuna watu walikuja na magari yao wakawabeba watu wengine, sasa wamewahi kuondoka. Itabidi kwenye coaster wabanane. SK kwa kuwa alikuja peke yake yuko free. Binti na rafiki yake wakajisogeza kwa SK, na kuacha vijana wakihangaika na coaster. SK akawasindikiza hao mabinti mpaka makwao, akaanza na yule mwingine akamalizia kwa yule target. Daaah, they call it mission accomplished. Kesho yake hatukuonana, ila siku ya pili nilimtafuta kwenye simu anasema amepata dharura hayupo kazini, kumbe alienda kumalizia mission yake. The game is over.

Watu wengine mimi nawavulia kofia aisee.
 
  • Thanks
Reactions: Paw
Nilifikiri ni lara 1 kaja na part 2 ya Silent Killer.
 
Last edited by a moderator:
Kwanza, kwanini usifiwe kwa mambo ya ngono? Ukiona mtu anajisifia sana mambo ya chumbani ana matatizo huyo
 
Watu wa hivyo mi nawapendaga sana sema changamoto zao ndo kama hizo huwezi hata kumshitukia
 
kuna jamaa yangu m1 ndivyo alivyo hivyo ..alikula office nzima hadi boss kimya kimya ....shikamoo SK
 
Ogopa sana Silent Killers.
Wanapanga kitu leo kitakachotakiwa kukamilia miaka 10 mbeleni.
 
Kwa muktadha wa story,huitaji kuwa SK kumng'oa mfanyakazi mpya kazini...,anaetegemea usafiri wa jumuiya kwenda na kurudi kwenye sherehe..,anaeishiwa na kifurushi...,mwenye simu ya Megapixels ndogo!!
 
Kwa muktadha wa story,huitaji kuwa SK kumng'oa mfanyakazi mpya kazini...,anaetegemea usafiri wa jumuiya kwenda na kurudi kwenye sherehe..,anaeishiwa na kifurushi...,mwenye simu ya Megapixels ndogo!!

Ha ha ha ha ha ha.......SK ni wa kawaida tu ila hao madogo hawana game!
 
why do i feel like u r sk? ?-???‚ alafu si ajabu na yule rafiki nae hakulaziwa damu
 
Back
Top Bottom