Silaha kubwa ya Serikali na watawala wengi wa nchi za ulimwengu wa tatu ni ujinga wa raia wao.

mr mkiki

JF-Expert Member
Sep 22, 2016
5,583
11,659
Idadi ya wanasiasa wanaosema wametumwa na Mungu inaongezeka. Hii ni njia ya bei rahisi zaidi kuwahadaa na kuwalaghai masikini na watu wasiokuwa na elimu au uelewa. Silaha kubwa ya serikali na watawala wengi wa nchi za ulimwengu wa tatu ni ujinga wa raia wao.

".Msiwabomolee Nyumba Mwanza Hata Kama Walikosea Hawa Ndio Walinipa Urais."→ Magufuli

".Mtulia Ameangalia Akaona Watu Wanabomolewa Nyumba Zao Ameamua Ajiunge Na CCM Ili Wasiendelee Kubomolewa."→Paul Makonda

".Nchi Inaongozwa Na Washamba Na Malimbukeni Wa Madaraka."→Zitto

Katiba Ya Tanzania!!
DVupYZ7X0AAcku8.jpg

mr mkiki.
 
Mara paap Nissan nyeupe, Hapa sichangii kitu naogopa Mamlaka
 
Jibu swali, hamtaki wageni ,mmezoea mkianzisha tu thread na timu yenu ya kuponda ipo stanby! Bongoland bana!, Mmh!
Siasa zetu zinakosa TATHMINI ndio maana zinakimbikia SYMPATHY zaidi kuliko FACTS wimbo huu haujaanza Leo wala Jana na haujaimbwa na MTU Bali hata VYAMA
 
Hiyo ni hadaa tu hakuna aliyewahi kumwona Mungu. Hata wanaosema ni chaguo la Mungu, wanasahau tu kuwa hata shetani ana machaguo yake na maagizo yake.Wanatuhadaa kutumwa na Mungu wakati matendo yao ni ya kishetani
 
Waga nawaza ,hivi walimu wa primary wanachangishwaje michango ya mwenge kwa lazima??
Mbona watumishi wengine hawanyanyaswi kama walimu wa primary??

Ukiangalia kwa undani utakuta walimu wengi wa primary elimu zao ni ndogo na za kuunga unga....wakitishiwa kidogo tu wanatepetaa
 
sio walimu Wa primary tu.kwa kuwa mwalimu qualification yake ya kwanza ni kufeli mtihani hiyo inawanyima si tu confidence but also option nyingine
 
Waga nawaza ,hivi walimu wa primary wanachangishwaje michango ya mwenge kwa lazima??
Mbona watumishi wengine hawanyanyaswi kama walimu wa primary??

Ukiangalia kwa undani utakuta walimu wengi wa primary elimu zao ni ndogo na za kuunga unga....wakitishiwa kidogo tu wanatepetaa
Mungu nae anawaona tu atawaaibisha mchana kweupe
 
Ujinga +umasikini
Ni philosophy ya third world, wanaamini ukitaka kuwatala watu wafanye kuwa wajinga utawala, wanyime elimu,wabane kwenye kodi,nk.MTU akiwa masikini na upeo wake wa kufikiri unapungua.Kuna sera za kuzalisha masikini mfano sera za ujamaa lengo lilikuwa kuzalisha masikini zaidi,ili iwe rahisi kuwatawala.Masikini ukimpa kanga,Kofia,elf tano na t-shirts yeye atakupa kura.
 
Nimekuelewa sana
 
Mkuu hao viongozi wetu wanatoka katika jamii zetu hizo hizo,na viongozi hao hao ni jamii ya sisi wananchi.Wanaukwa uongozi kutegemea na utaratibu wa nchi zao.
Maadamu hawatoki mbiguni au sio wakimbizi au wahamiaji kutoka nje ni wawakilishi wetu wenye mawazo au uwezo kama wewe na mimi.
Kuwacheka ni kujicheka wewe mwenyewe,Labda kuna mambo hatujayafikia kama jamii ya nchi hizo.
Na njia rahisi,ni kuondoa rushwa,kuheshimiana,haki sawa kwa wote,na wananchi wenyewe kujiamlia mambo yao wenyewe.
 
Back
Top Bottom