Mami, naona umekula Propaganda sana. Hata mambo ya Cosmos, USA walikuwa wanadhani ni wakali ila waliposhindwa kujenga Station ya angani wakati Warusi waliona heri wafe njaa na wafilisike ila washinde vita ya Cosmos, wakaweza kujenga na kuiweka kwa miaka mingi Station yao ya MIR.
Walipokuja kujenga hii ya Kimataifa, Mrusi ilibidi uzoefu wake utumike sana na Rocket zake zikawa ndiyo Trucks za kubeba mizigo kwenda kujenga hiyo Space Station.
Unapokuja kwenye Ndege, Warusi ni wazuri sana na hasa wanajua mno kucheza na Aerodynamics (mambo ya Coanda Effect). Pia Pilots wa Kirusi ni wakali kuzidi wa USA kwa sababu inabidi wawe hivyo kutokana na hali mbaya ya hewa ya Urusi. Sehemu kama Kamchatka, ni balaa tupu maana unatua kwenye Snow....
Kwenye ndege za kivita, USA walikuwa wanatisha kwenye hiyo midude kama B-2, B-52, Black bird nk ambazo nafikiri Warusi wao waliwekeza zaidi kwenye Makombora na si ndege za aina hiyo. Ila unavyokuja kwenye hizi ndege kama F-16, F-22 Raptor nk ukilinganisha na Sukhoi kama Su-27, Su-35/Mig 27, Mig 29 basi Mrusi alikuwa anakwenda ngoma droo na USA. Speed ya ndege karibu zote ni sawa. Silaha zake ni zilezile ila tu USA kama nilivyosema, Radar zake ni kali zaidi ya Warusi kama ambavyo hiyo video inasema. Sidhani kama ulisikiliza na kama ungelisikiliza, basi ungelielewa ninasema nini. Jamaa kaelezea uzuri na ubaya wa kila ndege na mwisho kakuachia wewe uamue nani mkali kati ya SU-35(Russia) vs F-22 Raptor (USA).
Hata vita ya Cuba, waliwaonyesha Wanajeshi wa USA wakicheka na Warusi walio ndani ya Submarine na bila kujua Warusi walikuwa tayari na NUKE kwenye hizo Submarine. Walipokuja kuambia ukweli, wakaanza kujikojolea.... Ahh, USA unapokuja kwenye Manowari na hasa hizi za kubeba ndege ndani, nakubaliana na wewe kuwa ni mtu pekee duniani.
USA vitu vyao aghali sana na naona ni ufisadi hufanyika hapa na hawa akina Martin/Boeng kwa kupandisha sana gharama.
Mami kwenye conventional weaponry USA iko juu bana. Haina mpinzani kabisa. Urusi imejitutumia ku-maintain parity lakini wapi...hamna kitu.