Faana
JF-Expert Member
- Dec 12, 2011
- 31,829
- 33,225
Tumetoka ibadani, rafiki yangu akaniambia nimsindikize farm kwake apeleke dawa za mifugo, tulipofika farm, hatukumkuta kijana wake wa kazi (farm boy) tukaenda nyumba ya jirani kuulizia, akatoka binti wa kama miaka 17 au 18, akajibu huyo kijana hayupo hapo, tukarudi bandani, baadaye akaja dakitari wa mifugo, akachukua dawa na kuanza kuwatibu mifugo, yule farm boy akaja, alipoulizwa alikuwa wapi akasema alikwenda kuchota maji, rafiki yangu akamkazia macho, akamwambia " acha mchezo huo mara moja, nakukanya usirudie tena, nadhani umenielewa" kijana akaingiwa aibu fulani, daktari wa mifugo akaongezea "dogo utakuja katwa mapanga hapa, huku siyo .... akataja Mkoa" muda huo sikuelewa kwanini dogo anaonywa kwa kwenda kuteka maji, kumbe wenzangu wamegundua dogo alikuwa na yule binti wa jirani, nilichoshangaa ni pale rafiki yangu na daktari wa mifugo waliposema hawa watoto wamevunja the sixth commandment of God, baada ya kuona macho yao yamevimba design fulani. Nikajifunza kwamba kumbe tukiiba huo mtaa tunajulikana, ila huwa hatuambiwi tu🤣!