Sikutegemea kama mdogo wangu Nape naye angelimia meno, wengi mjiandae

Lizaboni

JF-Expert Member
Feb 21, 2013
33,894
20,375
Wadau, amani iwe kwenu.

Ni nchi chache duniani zimebahatika kuwa na kiongozi mwenye maono na fikra ya muda mrefu juu ya nchi yake. Rais Magufuli ni mmoja wapo. Ameyastudy mazingira ya Tanzania na kuyafahamu vizuri. Anajua njia zinazotumika kuliibia taifa. Naukumbuka ule msemo wake kuwa akiwa Rais wa Tanzania, KUNA WATU WATALIMIA MENO.

Kinachoendelea sasa kwa nchi yetu ni watu kulimia meno badala ya majembe. Kawabana kila kona. Si wa CCM, si wa upinzani. Ametight ile mbaya ili wale waliokuwa wanaishi kijanja na kitapeli waweze kulimia meno. Ila sisi tunaoishi kwa Principle kwa hakika tunafurahia sana anavyofanya Rais wetu.

Naukumbuka pia msemo wake kuwa UKIONA WAPINZANI WANAKUSHANGILIA NA KUKUPIGIA MAKOFI, BASI RUDI NYUMA JIULIZE UMEKOSEA WAPI. NA UKIONA WABAYA WAKO WANAKUNUNIA NA KUKUTAKA UACHE JAMBO FULANI BASI NI VEMA UKAONGEZA JUHUDI KATIKA KLIFANYA JAMBO HILO.

UKAWA sasa wamehemewa. Wamebanwa kila kona na hawafurukuti tena. Rais anajua nini anakifanya. Kelele zao hazimzuii kufanya maamuzi kwa maslahi mapana ya Taifa. Kelele za wapinzani juu ya uhaba wa sukari na ukame zimewageuka wenyewe. Kwa sasa hayo si matatizo ya msingi ambayo wanaweza kuyatumia kuomba kura kwa Watanzania..

Nimalizie kwa kusema kuwa, Magufuli huyu wa sasa ni yule yule wa Wizara ya Ujenzi. Hajabadilika. Tusipobadilika Watanzania wengi tutajikuta tunalimia meno. Hakuna aliyetaraji kama na Nape naye angekuwa ni miongoni mwa walimia meno kwa jinsi alivyojidai eti yeye ni Kada kindakindaki.
 
Mimi Nape aliniacha hoi pale aliposema eti ameipigania CCM tangu Baba yake na kuitoa shimoni, hapo ndipo nilipochoka, kama Nape anasema hivyo Watoto wa Sokoine waseme nini ambao Baba yao alikufa akiwa kazini kuipigania CCM? Huyu Nape amepotea sana na ameniboa sana!
 
Ugomvi ulianzia hapa...

Screenshot_2017-03-25-23-55-25.png
 
Rais gani mwenye maono anaongea uwongo hadharani? Rais gani mwenye maono kila hotuba ni vitisho tu? Rais gani mwenye maono anaweza fanya teuzi na kusema ameteua kuwakomoa wapinzani wake kisa hawaelewani na aliyemteua?

Rais gani mwenye maono analazimisha kiki kwa kugombania "frent font" kwenye magazeti? Rais gani mwenye maono anavunja katiba aliyoapa kuilinda?
 
Watu wangu wanaangamia kwa kukosa maarifa sio maneno yangu nukuu ndani ya Biblia Takatifu
 
Back
Top Bottom