saidi bunduki
Member
- Mar 10, 2018
- 24
- 23
1. Penzi pendezo la moyo, kwa uliye mkhiyari
Moyo usemapo ndiyo, na mwili huwa tayari
Kwa jumla yote hayo, ndio pendo hutabiri
ila wewe sikupendi, na wala huna kasoro
Moyo usemapo ndiyo, na mwili huwa tayari
Kwa jumla yote hayo, ndio pendo hutabiri
ila wewe sikupendi, na wala huna kasoro
2. Nimechora kwenye jiwe, hakuna nilichopata
Liwalo basi naliwe. Nilichoka kukuota
Ulinipa nini wewe, mpaka nikakufata?
ila wewe sikupendi, na wala huna kasoro
Liwalo basi naliwe. Nilichoka kukuota
Ulinipa nini wewe, mpaka nikakufata?
ila wewe sikupendi, na wala huna kasoro
3. Mejikuta nakutaka, siku isiyo na saa
Heti swaga zikashuka, kwako? Laa laa laa
Nikakuona wacheka, hukutaka kukataa
ila wewe sikupendi, na wala huna kasoro
Heti swaga zikashuka, kwako? Laa laa laa
Nikakuona wacheka, hukutaka kukataa
ila wewe sikupendi, na wala huna kasoro
4. Ukenda kwa zako shoga, haraka kunitangaza
“Jama niwape m boga?, tayari kunitangaza
Yule nilo mtakaga, leo amenitongoza
ila wewe sikupendi, na wala huna kasoro
“Jama niwape m boga?, tayari kunitangaza
Yule nilo mtakaga, leo amenitongoza
ila wewe sikupendi, na wala huna kasoro
5. Ulinipa nini dada, nashindwa kutafakari
Nafikiri kila muda, hwenda ikawa SIHIRI
Kweli mapenzi uroda, ila hii ni shubiri
ila wewe sikupendi, na wala huna kasoro
Nafikiri kila muda, hwenda ikawa SIHIRI
Kweli mapenzi uroda, ila hii ni shubiri
ila wewe sikupendi, na wala huna kasoro
6. Tuwapo ndani wawili, hisia sina kabisa
Nakuona ka rijali, mpaka pozi nakosa
Nafanya kufosi mwili, sije niona KIBISA
kwakweli inaniuma, sina njia ya kufanya
Nakuona ka rijali, mpaka pozi nakosa
Nafanya kufosi mwili, sije niona KIBISA
kwakweli inaniuma, sina njia ya kufanya
7. Kizito kitendawili, zaidi ya vya wahenga
Kichwa changu chajadili, nahisi machenga chenga
nikipiga moja chali, nishapoteza uwinga
kwakweli inaniuma, sina njia ya kufanya
Kichwa changu chajadili, nahisi machenga chenga
nikipiga moja chali, nishapoteza uwinga
kwakweli inaniuma, sina njia ya kufanya
8. Wanipenda ki ukweli, hilo halinaga wasi
Yasemekana hulali, nisije nikakuasi
Lakini bado najali, upendo kwako nafosi
kwakweli inaniuma, sina njia ya kufanya
Yasemekana hulali, nisije nikakuasi
Lakini bado najali, upendo kwako nafosi
kwakweli inaniuma, sina njia ya kufanya
9. Ukiniona furaha, washindwa hata kusema
Maneno yangu mzaha, karibu uwe kilema
Wapenda yangu fasaha, niendapo uko nyuma
naumia roho yangu, mungu wangu nisamehe
Maneno yangu mzaha, karibu uwe kilema
Wapenda yangu fasaha, niendapo uko nyuma
naumia roho yangu, mungu wangu nisamehe
10. Si kwamba wewe m baya, sijawa na mana hiyo
Si kwamba wewe Malaya, si mtu wa mambo hayo
Si maharage ya MBEYA, kuiva pasi mboyoyo
naumia roho yangu, mungu wangu nisamehe
Si kwamba wewe Malaya, si mtu wa mambo hayo
Si maharage ya MBEYA, kuiva pasi mboyoyo
naumia roho yangu, mungu wangu nisamehe
11. Uko radhi nile mimi , wewe ulale na njaa
U radhi upigwe ngumi, unilinde mimi “daa”
Yote tisa ila kumi, “wataka witwe mamaa
naumia roho yangu, mungu wangu nisamehe
U radhi upigwe ngumi, unilinde mimi “daa”
Yote tisa ila kumi, “wataka witwe mamaa
naumia roho yangu, mungu wangu nisamehe
12. Nakuonea huruma, kwakweli nakuumiza
Jinsi ninavokuchuma, ndugu nitakumaliza
Roho yangu yaniuma, bora ungejiongeza
naumia roho yangu, mungu wangu nisamehe
Jinsi ninavokuchuma, ndugu nitakumaliza
Roho yangu yaniuma, bora ungejiongeza
naumia roho yangu, mungu wangu nisamehe
13. Mapenzi ni msawazo, si ya nguvu wala dawa
Alama mlizonazo, angalau ziwe sawa
Lipatikane tulizo, kila mtu awe powa
naumia roho yangu, mungu wangu nisamehe
Alama mlizonazo, angalau ziwe sawa
Lipatikane tulizo, kila mtu awe powa
naumia roho yangu, mungu wangu nisamehe
14. Nashindwa kukuambia, ubinadamu ni kazi
Kila nikifikiria, siwezi tena siwezi
Ila moyo waongea, kulikoni kinywa wazi
naumia roho yangu, mungu wangu nisamehe
Kila nikifikiria, siwezi tena siwezi
Ila moyo waongea, kulikoni kinywa wazi
naumia roho yangu, mungu wangu nisamehe
15. Najua ni yako haki, kunipenda si hatia
Si kama hustahiki, kuwa wangu malikia
Ila mapenzi ashiki, kwako haijatimia
Ninajisikia dhiki, nahisi nakuonea
Si kama hustahiki, kuwa wangu malikia
Ila mapenzi ashiki, kwako haijatimia
Ninajisikia dhiki, nahisi nakuonea
16. Unahaki msichana, kuwa na umpendae
Kupata mno endana, maishani uwe nae
Kwa kuwa umeniona, mimi ndio nikufae
Muombe Mola jalali, anipe penzi na wewe
Kupata mno endana, maishani uwe nae
Kwa kuwa umeniona, mimi ndio nikufae
Muombe Mola jalali, anipe penzi na wewe
17. Sipendi nikusaliti, siijui kesho yangu
Kwakuwa mejidhatiti, basi sina budi kwangu
Twende nyumbani kibiti, wajue wazazi wangu
Nitakuoa mamii, nikutulize dadaa
Kwakuwa mejidhatiti, basi sina budi kwangu
Twende nyumbani kibiti, wajue wazazi wangu
Nitakuoa mamii, nikutulize dadaa