Hapa utaona kwamba kusema kweli viongozi wengine akili zao ni kama mchwa...Yaani ni ajabu sana kwa Mwinyi ambaye ni mchwa kuweza kuzungumzia ubovu ama uimara wa msonobari alokula ukaisha na kubakia ganda tupu.
.
Ni hawa hawa akina Mwinyi na viongozi wengine walioua mashirika ya Umma.. wao kama mchwa waliyafilisi mashirika kisha wakaamua kuyauza kama vile mapungufu yapo ktk mashirika..tatizo ni mchwa kwa nini wakayauza mashirika na sio kuthibiti hao mchwa? sii ndio yale yale ya kugawa vyandarua kuzuia malaria hali wakiacha mbu wakizaana!.
kwa akili zake za ajabu, Mwinyi anakiri kwamba kwamba haya mashirika yaligunguliwa na mchwa, ambao ndio wao...cha ajabu wameuza mashirika ambayo tayari yamekwisha liwa na mchwa, kisha Hilo Azimio la Zanzibar likawapa RUKSA hao mchwa walio yaharibu mashirka ya Umma wahamie miti mingine..
Mimi nadhani huyu Mwinyi anazeeka vibaya, anakosa hekima na busara zake za awali kwani hakuwa na sifa yoyote ya Uongozi zaidi ya hekima zake!
Companero thanks for this useful post, nadhani Mwinyi yuko sahihi kusema hakuliua. Hakuna sentensi inayo suggest hivyo, na sababu zake alizozitoa are still concrete
Companero,
Mkuu wangu ktk hotuba ile alisema hawakulifuta Azimio la Arusha ila wameliboresha kwa kufuta baadhi ya sheria ili kutuwezesha kitaifa kwenda na wakati! akilenga soko huria na Utandawazi.
Lakini kama kweli walitaka kulenga Soko Huria na Utandawazi, hapakuwepo na sababu ya kuuza mashirika ya Umma ikiwa makosa ni WATU walioharibu mashirika hayo. kifupi hawkuuza nyumba ama gofu ila waliuza viwanja..Sisi wananchi tunatazama thamani ya viwanja vile, wakati wao wanatupa hadithi za magofu...Ni hadithi hii hii wnaitumia kuuza pia nyumba za National housingi na Msajili.
Pili, hapakuwepo na sababu ya kuondoa miiko na maadili ya Uongozi ikiwa soko huria halihusianai na viongozi kufanya Biashara...kuepuka conflict of interest ni moja ya Maazimio makubwa ya Arusha.
Ndani ya roho zetu sisi sote tunajua fika kwamba - Siasa ya Ujama na Kujitegemea ilikufa na hakuna kitu wala mfano hata mmoja kiutawala unaolenga siasa ya Ujamaa na Kujitegemea hii leo, sasa nambie wewe mkuu wangu, ikiwa Ujamaa na Kujitegemea umekufa hilo Azimio la Arusha ni lipi analozingimzia Mwinyi?....
Mkuu ulitegemea aseme nimeliua Azimio la Arusha?? Ni mgeni na wanasiasa?
Ni wazi Azimio la Arusha linauliwa kwa vitendo, sera na misimamo mipya ya kiserikali zaidi kuliko hutba za kisiasa.
Sitaki kumtetea Mwinyi lakini naomba kuuliza hadi alipoingia Mwinyi madarakani hali ya uchumi wetu ilikuwa vipi tukifananinisha na hali ilivyokuwa wakati tunapata uhuru?
Serikali ya Mzee Mwinyi haiwezi kukwepa makosa ya kuyaua mashirika ya umma kwani hao mchwa walioyala yakaisha waliteuliwa na walikuwa wakilindwa na serikali hata pale wafanyakazi walipotaka kupambana nao.
Serikali kwa ujumla ndo ilikuwa mwangalizi wa mashirika hayo ikiteua menejimenti na bodi za kuyaendesha mashirika na kuzisimamia. .
Unachosema ni sahihi, kuwa hajasema directly kuwa ameua, at the same time tunataka kusema ameua! kwa sababu ya kuruhusu mambo mengi!
Hoja yangu ni kuwa AD lilikufa natural death, lilishakufa kabla ya kuanza kuw in effect, unless mtu aje na atoe mafanikio ya azimio wakati liko in effect
Huwezi kuchanganya UJAMAA NA KUJITEGEMEA wakati mmoja, hakuna kitu kama hicho! ukisema kujitegema na ujamaa lazima viende pamoja lazima uweke mipaka ya kujitegemea basi.
Lilikufa natural death si Mwinyi aliliua wala nani, after all nataka niwafahamu hao waanzilishi wa Azimio, kuwa walikuwaje waka 'kubaliana' na sera za Mwinyi kiasi hicho? what made them to abandon Azimio?
...........wangeacha hata ile miiko ya uongozi....duh hivi ile tume ya maadili ya viongozi pale Ohio next to Holland house inafanya kazi bado?....
Sidhani kaa ni kweli kwamba kuwa na Ujamaa na Kujitegemea kwa pamoja ilikuwa ni kuji-cotradict. Kujitegemea kunakoongelewa ni kama taifa kuwa na uwezo wa kukidhi mahitaji yake na kuagiza kutoka nje ya nchi yetu tu vile vinavyotushinda kuwa navyo kutokana kuwa nyuma kitecknoljia au kihali yeyote ile.
Ujamaa ni kwamba state have a total control of major means of economy, kama mashirika ya kutoa huduma a.k.a mashirika ya umma, n.k. Ndo maana kwamba kulikuwa na kuanzishwa viwanda ambavyo mchwa walikuja kuviua, kuimarisha kilimo, kujenga miundombinu kaa Tazara etc etc..
I' m still a big fan of this ideas. Yet I know things never turned-out, lakini kulikuwa na prospect ya kuwa na nchi imara ktk muda wa miongo miwili mitatu. Pia ni shurti izingatiwe maadui wa siasa hii walikuwa wengi na very strong polarization hasa kutoka kwa mabwanyenye waliokuwa wamejikita huko Kenya na wakoloni waliokuwa Norh & South Rhodesia na maadui wote wa vita ya ukombozi kusini mwa Africa.
Waberoya,
Hao mabepari wenyewe wamekwama. USA walipewa uhuru wa watu/mashirika binafsi kujifanyia kila kitu wanavyotaka wenyewe. Nini kimetokea?
Msiandike kwa kutumia mfano mmoja. Angalieni mbele na nyuma na ndipo mje na hizo zenu za kutetea kufa kwa Azimio la Arusha. Mwinyi na Mkapa walitakiwa kurekebisha yale tu ambayo kwao wanaona yanafanya uchimi ukwame. Pia unaporekebisha si kuwa ubadili kila kitu. Unafanya kwanza majaribio na kidogokidogo unaangalia umetoka wapi na umefikia wapi. Wachina wanafanya hivyo hadi leo kwa mafanikio makubwa. Wangelitangaza kuwa wako HURU kama sisi tulivyofanya, nafikiri leo wangelikuwa na vita na machafuko ya kila aina.
USA kimegoma na mwisho serikali imerudi na kusema itakuwa inaweka mkono wake kila sehemu ili walau wafahamu nini kinaendelea kwenye mashirika. Ilishindikana nini kuwapa Watanzania hata kama kwa Mkopo mashirika yote na serikali ibaki kuwa mwangalizi tu na kuchukua kodi. Leo hii haya mashirika yangelikuwa yanaongozwa/kumilikiwa na wazawa na sidhani kama yangelikuwa yamekufa.
Siyo siri kuwa wapinzani wa NYERERE walifanya makusudi kuyauwa mashirika ili tu kuonyesha Azimio la Arusha ni la ovyo. Walipokipata wanachokitaka, wakaliingilia Azimio la Arusha na kuliuwa kwa ndani na kuacha mwili wake nje (jina) ili mtu akisema, wawe wadai kuwa ahhh, AD bado ipo hai kabisa na inaendelea vizuri sana. Too sad.
Ndiyo maana Nyerere anasema "wenye akili tukajua AD imekufa". Yaani hata Miiko ya viongozi? Nakubaliana na member mmoja hapo juu kuwa AD iingizwe kwenye Katiba ya nchi hasa kile kipengele cha Miiko ya viongozi. Haya ya juzi kumsikiliza Mkono na Genge lake wakitetea kuwa CCM inatakiwa iwe na mafiga matatu yaani Wakulima, wafanyakazi na Wafanya biashara, kwa kweli ni kichekesho. Wafanyabiashara wenyewe ni CCM ambao hata unashindwa lini wameanza kuwa wafanyabishara zaidi ya kuwa na pesa za ufisadi.
UJAMAA na Kujitegemea: Wayahudi waliweza sana kuanza na hii system. Imewasaidia sana sana. Sisi tumekwama sijui ni Miafrika ndivyo tulivyo au viongozi wetu?
Huwezi ukafananisha ujamaa wa Nyerere na hao wachina, warussia n.k ,. Ujamaa wa Nyerere ulikuwa ni hybrid ya hizo siasa na influence ya watu wengi
Hakuna sehemu pia ninayosuggest kuwa Ubepari ni bora, mind yangu haijawekwa kwenye kapu kuwa kama si ujamaa basi ni ubepari!
Nyerere na waasisi wengine wa siasa ya ujamaa ya Tanzania, still they have credit to gain, wanastahili sifa na heshima zao na hasa kuwa na siasa ya ujamaa na kujitegemea ya kwetu sisi! Nyerere angeiga wachina angekuwa dictator!
My argument katika dunia ya leo, na kizazi cha leo, cha watu millioni 45 we have to sit down na kuona AD ilikuwa na uzuri upi, na kasoro ipi! lazima tujue pia nature na tabia zetu watanzania wa leo, lazima tuangalie influence ya globalisation, climate change, terrorist, ambayo hatuwezi kujitoa kwayo, lazima tuangalie je Kujitegemea kunakosemwa kulikuwa na vision ipi, malengo yapi?
Hakuna siasa 100% perfect kama JKN aliweza kutoka na siasa yake, we dont have people ambao wakasimama na kusema lets take Nyerere's idea na kujumlisha na idea zingine na tufuate hivi kwa leo hii.JKN idea will never be our compass.
Kurudi nyuma na kulilia AD ni sawa na kurudi tulipofeli, AD is katiba? ni biblia au Quran? watu leo hii wameiba hawapelekwi jela wala kurudisha mali zetu ni kwa sababu ya AD haipo?? i dont get it!
Hata leo hii JKN angekuwa hai , na tukampa nchi tena, his mind today lazima ni tofauti na nyakati hizo. We need to start now and make our future! siamini kabisa kuwa system za dunia hii ni ubepari na ujamaa tu. Tumefikia hapo, tumekwama hapo na kuamini ubepari mzuri kwa sababu hatujafanya assignment zetu vizuri.
Kulilia AD ni kupoteza muda, kama hakuna anayeweza kupima mafanikio ya siasa hii na imebaki fiction, then ndiyo kufeli kwenyewe huko, hatuihitaji story nyingi wala sababu, ambazo tunazo kila siku na hazikosekani!
Kama leo hii mtu bado anaona pamoja na hii kitu kufail still anaona ni bora zaidi, basi tuna matatizo mengi na makubwa ambayo lazima tuyatatue hayo ili kufikia ujamaa na kujitegema, kwa namna nyingine JKN alitoa idea ambayo pengine it will work next century! we have big big problems na matabia yetu haya ili kuishi kwenye hilo azimio!
However, I am still thinking whether kama matatizo ya leo ni kutokana na sera ya ujamaa!
If this is our mind, lets Kikwete and his partner plunder our wealthy because AD IS DEAD na yeye siye aliyeliua!
I believe in Law, order and JUSTICE.
I believe every human shall work and improve our society and the universe siyo kwa sababu mtu fulani kasema ni kwa sababu tumezaliwa tukijua hilo!
Ninachokataa ni kuwa kuna watu hawataki kungalia failure ya hizi siasa, hatutaki kukaa chini na kusema JKN and so and so walikosea hapa na walipatia hapa., na sisi leo tuchuke idea znuri za JKN na kuacha makapi na kuungansiha na hali yetu ya sasa na kusonga mbele!
NINAMUHESHIMU MZEE MWINYI ZAIDI YA MAELEZO ! UJAMAA(azimio la arusha) LINABAKI KUWA PEKEE MPAKA SASA LENYE NIA YA KWELI NA YA DHATI KUMSAIDIA MTANZANIA....! HUENDA BABA YETU MWINYI AMEGUNDUA HILO NDO HATA SASA AMEKUJA NA HOJA HII....MZEE HAJAKOSEA INABIDI TUMPONGEZE KWA KUNG'AMUA HILO.......AMELETA UBEPARI LAKINI AMEONA YOTE SI MAJIBU KWA MTANZANIA BALI UJAMAA....(azimio la arusha)HONGERA NA PONGEZI MZEE WETU KWA KUJIREKEBISHA....WENGINE NAO WAUNGE MSTARIIIIII....!