sikujua wanandoa wana hizi haki.

sikujua wanandoa wana hizi haki.

Red Giant

JF-Expert Member
Joined
Mar 9, 2012
Posts
15,650
Reaction score
21,014
nilikuwa nasoma kitabu kinaitwa jukwaa la sheria cha Rev. Justine Kaleb.
Kumchukulia hatua za kisheria mtu aliyetoa ahadi ya kukuoa au kuolewa na wewe na baadaye kuvunja ahadi hiyo kwa sababu isiyo halali.
Kumchukulia hatua za kisheria mtu ambaye amethbitika kufanya vitendo vya uzinzi na mume au mke wako.
Kumchukulia hatua za kisheria mtu yoyote ambaye atathibitika kumshawishi au kumsababisha mume au mke wako kuondoka nyumbani na kuiacha au kuitelekeza familia yake.
Kudai mali, mahali au zawadi yoyote iliyotolewa kwa lengo la baadaye kufungwa ndoa endapo itathibitika kuwa ndoa hiyo haitaweza kufungwa kutokana sababu mbalimbali..
 
Hizi mbili zingetumika sawasawa.....

Michepuko ingepungua

Kumchukulia hatua za kisheria mtu ambaye amethbitika kufanya vitendo vya uzinzi na mume au mke wako.
Kumchukulia hatua za kisheria mtu yoyote ambaye atathibitika kumshawishi au kumsababisha mume au mke wako kuondoka nyumbani na kuiacha au kuitelekeza familia yake.
 
mmmmh!!! hiyo ya kwanza tungefungwa wengi
 
Inawezekana sana kuchukua hatua za kisheria kwenye hayo maswala sema tu watu wengi hawajui sheria. Pia kibongo bongo usimbufu unaweza ukazidi kwa mtoa mashtaka kuliko kwa mshtakiwa.
 
hahahaaaa!!! hiyo ya kutoa ahadi alafu hutimizi ni janga la wengi, si wanawake si wanaume, ila wanaume zaidi

Hamna bhanaa wanawake ndo hugeuka wakijiwa na anae zidi
 
Inawezekana sana kuchukua hatua za kisheria kwenye hayo maswala sema tu watu wengi hawajui sheria. Pia kibongo bongo usimbufu unaweza ukazidi kwa mtoa mashtaka kuliko kwa mshtakiwa.

Point.
 
Tabu yake madai haya unachoweza kufungua ni civil case. Kesi ya madai.
 
nadhani ningehukumiwa jela maisha kwa hiyo sheria ya kwanza
 
Ukinyimwa Papuchi na mamsapu bila sababu ya msingi sheria inasemaje?
NB: Na kinyume chake inahusika.
 
hiyo ya kwanza nataka nianze kuitumia sasa ole mtu atoe ahadi asitimize namfunga

Mimi nitaanzia kufunga watu humu JF, ole wake mwanadada aniahidi kitu kitamu iwe hadharani au kwa pm halafu asitimize. Na ushahidi wa maandishi upo kwenye server za JF...
 
Back
Top Bottom