SIKUJUA: sehemu ya 01.

Dec 25, 2017
13
2
Nilijikuta sina la kufanya katika wakati ule mgumu nikiwa mpweke
Kitandani macho yangu yakiangalia mwanga wa jua ulio penya katika tundu la paa lililochoka na kurusu mwanga kupita kila sehemu ya chumba kile kutokana na paa hilo kuwa na vidirisha vidogo ambavyo viliifanya chumba kuwa na Giza ata wakati wa mchana,,, na ndivyo pia ilivokuwa wakati wa masika maji yaliingia ndani kirahisi,,,,
Nakujikuta nikifanya kazi yakuhamisha hamisha kitanda angalau kupata sehemu ambayo inauwafadhali....kutokana na chumba kile kuwa na mwanga mdogo basi nilijua bado ni mapema sana kunyanyuka kitandani....Mara nilipitiwa na usingizi mzito ulionifanya nilale nakusahau kibarua changu kilichonipa angalau pesa ya kula........
Uuuuuh!!!!!!! Nimechelewa kazini ni sauti ya mbwa waliokuwa wakibweka ndio walionitoa usingizini nilitoka nje haraka haraka huku nikifunga vifungo vya shati langu la kazi.....ilikuwa ni sa nne na nusu nilijisemea peke angu "ooh masikini kazi yenyewe niliipata kwa tundu la sindano......Mungu nisaidie sitorudia kitendo hiki"
Kwakuwa nilikuwa ni kijana wa maji ya moto basi nilianza kutroti kama wasemavyo yani kamchakamchaka kadogo ili angalau nisiendele kuchelewa zaidi......
Haikuchukuwa muda mrefu nikawa nimefika kazini kwangu nikiwa na jibu la kumjibu boss ili kutuliza hasira zake ile kufika tu kabla sijafanya lolote niliwauliza wafanyakazi wenzangu kama boss amekuja ama bado
Ilikuwa ni saa tano sasa wakiwa bize kidogo na kazi woote waliniangalia na kucheka sana,,,,,...
Nanisijue sababu iliowafanya wacheke vile kwa utofauti wake Njoza yeye hakucheka ila alinionesha tu kwa vitendo niangalie shati langu........Loooh!!!!!¡yani ndo nimetembea Hivi kutoka.......sikumalizia kuongea baada yakukatishwa nasauti zakicheko hii sasa ata Njoze aliachia kicheko......lakini wazee nambieni basi boss yupo ama!!!???
Kodraki alijibu akimwigilizia boss anavoongeaga "wee kijana unapenda kazi ama hupendii huu ndo muda wakuja kaziniii".... Basi nilishusha pumzi zangu maana nilijua kama boss angekuwa maeneo Ya kazi basi Kodraki asingeigilizia vile.......
Nilivua shati nakuliweka pembeni tayari kwakuanza kazi
Tukiwa tunaendelea na kazi utani haukukosa maana ndo ulitufanya tuwe na hamasa na tusijihisi
Kumechoka..
Hii siku ikawa yangu kwa sababu tayari nimeonekana katika kila kichwa cha habari cha magazeti ya Leo apa kazini......
Baada ya ukimia wa kama dakika tatu Njoze aliuanzisha tena mjadala wakunihusu mimi.....
Akiniuliza sababu iliyonifanya Leo nikachelewa kazini ila katika kuuliza swali hilo hakuniacha hivihivi bali aliwafanya watu wote wanguke kicheko baada yakusema " au ndo Jana umezindua mwali nini Pastor".......swali hili lilinibadilisha kimawazo japo sikutaka kuonesha wazi kwamba limeniumiza.....
"Oyaa leta mchanga huo"...aliniita Kodraki huku akimalizia kwakusema au ndo utaki utani Leo..!??
Nilimjibu kwaharaka hapana Kodraki nilikuwa najipangusa jicho nilitoswa apa,.......
Hatimae siku hii ilimalika vizuri japo ilionekana kuanza vibaya
Tuliagana pale kila mmoja akapita njia yake na hapo ndipo hali yangu ya mawazo ikarudi nikiwa njiani naelekea pangoni kwangu nilikutana na msichana mmoja akionekana aliyepoteza matumaini kabisa.......
Alikuwa ni msichana mrembo sana ila tu kutokana na ile hali niliyomkuta nayo usingeweza kulitambua hilo basi kwakuwa nilijua nimpita njia tu kama Mimi niliendelea kupiga hatua nikisogea lakini kabla sijapiga hatua nyingi nilisikia sauti ikiniita " Kaka...kakaa samahani kaka angu"........

Nini kitaendelea.......usikose sehemu ya pili

Imeandikwa na shamsi shabani,

0759 859030:WhatsApp
 
Naombeni comments maana ni kazi yangu ya kwanza please!!!!!!!!!!
 
Karibu na kazi yako ya kwanza, tunaamini itakuwa nzuri, ila ongeza urefu kidogo.....
 
We ni mgeni humu? "Comments" haziombwi automatically zinakuja zenyewe ikiwa kazi utaifanya vizuri. Piga mzigo mkuu.
 
Cha muhimu tu usilete ule mchezo wa kutuma after miezi miwili au kuishia hewani kama story zingine.
 
SIKUJUA:sehemu ya pili,
Mwandishi:shamsi shabani

********
Ilipoishia.....alikuwa ni msichana mrembo sana ila kutokana na hali niliyomkuta nayo usingeweza kulitambua hilo..basi kwakuwa nilijua nimpita njia mwenzangu tu kama Mimi..
Niliendelea kupiga hatua nikisogea ,lakini kabla sijapiga hatua nyingi nilisikia sauti ikiniita....
"Kaka...kakaa..samahani kaka angu""

SONGA NAYO SASA

***
Muito wa kwanza nilijifanya sijasikia lakini muito wa wapili uloita tena ukiwa na maneno yakuudhunisha na kuupa simanzi moyo wangu...
Ili bidi nigeuze shingo yangu japo kujua kama kweli huyu Dada alikuwa ananita Mimi ama MTU mwingine..
Nilipogeuka japo sikuona mtu mwingine aliyekuwa maeneo yale lakini nilimuliza tu "waniita mimi???!!!"... Huku akionekana amechoka sana alijibu" ndio ni wewe kaka" kutokana na dhamira tulizonazo binadamu pindi tunapokutana na mtu au kitu kwa Mara ya kwanza huwa hatukiamini kwa asilimia 100 zote
Basi sikutaka kumsogelea karibu zaidi nilimuliza nimsaidie nini kwa wakati kama ule Giza likianza kutia nanga katika uso wa dunia.....
Cha kwanza alichoanza nacho kuongea ni ...."Samahani Kaka angu kwakukufanya usiendele na safari yako na kunisikiliza mimi mtu ambae ata unijui....!!!!......baada ya hapo alianza kudondosha machozi na ikapelekea ata kushindwa kuendelea kuongea
Kwakuwa mimi ni binadamu basi taratibu nilianza kuingiwa na roho ya huruma...na nikikumbuka mama angu alikuwa akinisisita kuwa saidia wenzangu wanapokuwa na shida ata kimawazo kama nitashindwa kihali na Mali..... nilianza kumsogelea karibu ili nijue nini zaidi kilichomsibu
Nilimbembeleza ili aendele kuongea..japo alikubali kuendelea kuongea ila wakati huu sasa aliongea kama mtoto anaejifunza kusoma..alisema"ka..ka angu m..imi apa nilipo kW..anza ata sijui nikuelezaje...!!!..ila tu kaka angu naomba unisaidie vitu viwili tu siku ya leo Chakula na hifadhi ya kulala..Naomba kaka angu ni Leo tu nakesho nitaondoka....na kiukweli mimi nimetoroka.....kabla hajamaliza nikadakia "Umetoroka jela ama wapi usije ukaniletea matatizo mimi wewe Dada....?????...
Akaendelea kuongea.. sasa aliongea huku akilia kabisa...kaka angu sijatoroka jela kama unayoijua wewe ila mimi nilitekwa na watu wasiojulikana na mpaka kufika hapa nilipo ni uwezo wa Mungu tu.....kaka angu naomba unisadie naomba kaka angu ni Leo tu yakesho mimi nitajua.....
Mmh ili bidi niheme kidogo japo sikutaka kumwamini kwa asilimia zote ila moyo wa huruma ulinijaa na kuushinda moyo wa ukatili
Lakini sasa kwa kile kipango changu nilichokizoea mimi tu atakiweza kweli...basi ilibidi tu nimweleze ukweli kwamba kwa maisha yangu yakubangaiza sina nyumba ila Nina pango tu almarufu " Mbavu za Mbwa"....kiukweli kutokana na hile hali ata kama angekuwa ni mzuri kiasi gani angekubali tu chochote ambacho kingemsaidia katika shida kama hiyo.....
Basi ilibidi tu akubaliane na hilo na mimi nikawa tayari kumsaidia kwakujikongoja tuliondoka nakuelekea pangoni kwangu........

****
Katika familia yakitajiri na maarufu katika mji wa kichuna...
Pamoja na vitu vyote hivyo familia hi imeonekana kukosa kabisa furaha na kuingia katika mgogoro mkubwa usiojulikana mwisho wake.....
.."hivi Baba Shiny mbona huonekani hata kujali wala kushughulika na mtoto wangu.....aliongea kwa jaziba lakini kabla hajaendelea zaidi alikatizwa na sauti ya mngurumo lakini iliyonekana kubembeleza zaidi......"lakini Mama Shiny huyo mtoto ulimleta wewe tu duniani???? Mbona unapenda kuniongezea mawazo nakunifanya nionekane kwamba sina upendo ma mtoto wangu wakipeke inaumiza sana....nakumalizia kuongea kwa jazba...."ila nitampata tu mtoto wangu ata kama itagharimu mamilioni ya pesa.......
Alisema hayo huku akiondoka nakumwacha mkewe akiomboleza kwa maneno yakulaumu......"yani wewe kila siku maneno yako ni hayo hayo tu nimeshayachoka kwanza kwangu ni kama makelele tu...mi ninachotaka nikumuona mtoto wangu shiny....huku machozi yakimtoka....."
******
Ilituchukua kama dakika arobaini na tano kufika pangoni kwakuwa nilijua hali aliyokuwa nayo huyu Dada basi ilibidi siku ya Leo ninunue chakula chakutosha ili aweze kula aridhike.....
Hapa ndipo ninapoishi dada angu ila tu utavumilia maana kama unavoona hali halisi ndiyo hii.....kutokana na ile hali alokuwanayo hakuonekana kujali hali ile kabisa...
Japo kulikuwa na Giza sana nje ila nilimuomba akajimwagie maji ili kuondoa uchovu......apo ndipo mamimi nikapata muda wakutandika na kutengeneza tengeneza kidogo maana ile hali aloikuta nayo haikuwa nzuri maana Mimi nilishazoea mwenyewe nikirudi ni kujitupia na kulala ......kutokana na woga wa Giza lile hakuchukua muda mrefu akawa amerudi maana lile Giza halikuwa la mchezo...tulikula tukamaliza alinishukuru sana...baada ya hapo aliniuliza hiki kijiji kinaitwaje nikamjibu...hapa panaitwa semanga mkoa wa kishana....alidakia kumbe wamenileta mkoa mwingine kabisa...nilimuliza kwani wewe Dada umetokea mkoa gani...."ni mkoa jirani tu na huu japo sijawahi kufika huku"....alijibu
Na kabla hajalala aliniomba kitu kimoja pakikucha nimsaidie kumpeleka stendi ya mabasi yaendayo kichuna mkoa jirani na hu Mimi nilipo....kabla sijamjibu ili bidi nijiulize sawa.....
Nitampeleka je ana nauli???? au wanafahamiana na hao madereva??au ana ndugu huku??lakini kama angekuwa na ndugu siangenda huko na si kwangu!!!?? kama hayo yoote siyo je atatoa wapi nauli?? Ni maswali yalioyokosa majibu..........!!!!!!!!!!
Nini kitafuata baada ya hapo..?..
Nikusihi tu endelea kufuatilia simulizi hii sehemu ya 03......

Karibu na kazi yako ya kwanza, tunaamini itakuwa nzuri, ila ongeza urefu kidogo.....
 
  • Thanks
Reactions: ram
Back
Top Bottom