Urafiki limekua ni jambo la hovyo sana siku hizi
'
Japokua dhana yenyewe ya urafiki sikubaliani nayo kabisa sina jinsi zaidi ya kukubali kuwa na marafiki kwa kuwa naishi dunia hihii ya watu wanaokubaliana na dhana hii
'
Tofauti na urafiki kuna kujuana,kujuana kuna karibu maana sawa na urafiki kwani huwezi kumfanyia jambo fulani mtu unaemjua
'
Kujuana au kufahamiana kwa mfano rahisi ni hapa JF.Wapo wasiojuana au wasiofahamiana kwa maana ya hawajawahi kuonana,au hana "umaarufu" wa kufanya watu wakujue hapa
'
Nikizungumzia mahusiano hayo yanayokaribia kufanana,nitazungumzia tafsiri mbovu na binafsi nisiyoipenda ambayo watu wanakua nayo hapa na mitaani tunamoishi
'
Urafiki na kujuana au kufahamiana watu wanaelewa kama kutokumkosoa au kutompinga mtu ambae una mahusiano ya aina hiyo
'
Hii ni tafsiri ya hovyo sana na siitaki.Unapounga mkono kila ninachosema hata kama ni jambo la hovyo nitajifunzaje?
'
Kama unaona nimepotoka mtu wa kwanza kuniambia ni wewe kama huwezi sitaki tujuane au urafiki na wewe
'
Kukukosoa ni kukufahamisha mtazamo tofauti na wako na wala sio ugomvi,kama hutaki kukosolewa tusijuane,kama hutaki kuniambia mtazamo wako ambao ni tofauti na wangu sitaki urafiki na wewe wala usinijue
'
Kutofautiana ni ishara ya kukua!