Sikubaliani kamwe na hili la "Bado tunakopesheka"

Sasa hiyo mikopo inafanya kazi gani maana Kama treni alisema anatumia hela za ndani na bajeti ikapita kwa mbwembwe kuwa hela za tra , zile hell feki ndio zitatumika kujenga.

Barbara nyingi bado zajenga kwa hisani ya Japan na watu wa marekani

Tofauti na hapo hakuna kingine kipya chenye uhitaji wa hela nyingi

Tukiangalia hilo ongezeko la 16pc ndani ya mwaka mmoja ni ukweli kuwa tunadanganywa na serikali yetu kuhusiana na makusanyo ya tra

Ndege zimekamatwa muda sasa Kama hela ingekuwepo Nina hakika wangelipwa kwa ngebe sana

Aliwadanganya wajinga wengi kua tanzania ni donor country kwa kusahau maneno yake akaja kukiri kuwa tajiri lazima akope

Hapo hajui kuwa tajiri mkopo wake unaweza kuwa wa OD au LC ya miezi 3 ambayo servicing ni ndogo

Mikopo hi twaikopa kwa dollar na tsh inshuka thamani hivyo tutajikuta twalipa madafu mengi sana

Kuna vitu vilivyokula hela za nchi ila hatuambiwi bajeti ilitokea wapi na sh ngapi zilitumika
Makinikia saga
 
Mshana jr. Naona umeanzisha kongamano kiaina. Inaonyesha kuna wengi wa aina yako wanalitakia mema Taifa letu lakini wanaogopa kujitokeza hivi. Nini kifanyike?
Hakuna cha kufanyika kwa sababu huna pa kuongelea,hakuna wa kukusikiliza wala kukujali
 
NAOMBA NIKOSOE KWA WELEDI
Mkopo una pande mbili hasi na chanya.... Mkopo hasi ni ule unaotumika mambo yanaposhindikana kabisa... Mkopo chanya ni ule mkopo unaokopa kufanyia jambo la maendeleo.. Lakini vyovyote iwavyo mkopo ni utumwa
Jambo lingine kwenye mkopo ni hili.... Unakopa wapi, unamkopa nani, kwa masharti yapi, kwa muda gani na kwa riba kiasi gani... Kuna mikopo ina masharti magumu na riba kubwa.
Kwenye mikopo pia kuna makubaliano, je familia inajua? Je mmeshauriana na kukubaliana? Hiki ni kigezo muhimu pia... Zaidi usipende kujifananisha na wengine , ati kwakuwa tu mimi nimekopa tena mkopo mrefu basi na wewe uniige... Hujui nguvu yangu ya kulipa ikoje...
Kama nchi naweza kusema tumekengeuka kwenye hili la mikopo na hii misaada, kwakuwa tumekuwa wakurupukaji mno na hatutendi kwa weledi.... Ni kweli kabisa wenzetu wana mikopo mirefu lakini ina faida kubwa na riba yao pengine ni ndogo sana... Halafu WAMESHAURIANA NA KUKUBALIANA.... Nimeshtushwa na kusononeka moyoni kwamba barabara ya uhuru ilijengwa kwa mkopo na tumechukua zaidi ya miaka 40 kuumaliza kulipia.... Hapa mkopeshaji Kala riba ma faida ya kufuru....
Mchina alijikongoja kwa miguu yake mpaka akasimama... Leo ndio mkopeshaji mkubwa wa mataifa mengi akiwamo mmarekani.. Kwahiyo si kweli kwamba usipokopa hutaendelea
Mimi nasema (I stand to be correct) tuondokane na haya mawazo ya kukopakopa.... Hatutafika popote... Tuwe na mawazo mapya ya kuja kuwa taifa linalokopesha kuliko hii ideology ya kusema bado tunakopesheka...!!! TUJIFUNZE KUJITEGEMEA na kama ni kukopa tukope kidogo sana tena kwa makubaliano halafu tukope kwenye taasisi zenye masharti nafuu na riba ndogo
Tusimuige Mjapani hatujui mikopo yake masharti yake yakoje... Lakini tuangalie Mjep yuko wapi.. Tusijilinganishe kabisa na yeye kwakuwa pamoja na kukopa sana almost alisimia 200 ya pato lake la taifa... Lakini ni mmojawapo wa nchi zinazoongoza kutoa misaada Tanzania na mikopo ya masharti nafuu.... Tuwe na tafakuri kwenye hili... Wenzetu wametuzidi sana... Isije kuwa wanakopa kwa riba ndogo sana halafu mkopo huohuo wanatukopesha sisi kwa riba ya juu halafu anakula commission... Mjapani sio mpumbavu atoe chakula chake ampe mgeni
Tusimuige mmarekani, huyo ndio kabisaaa sio level yetu... Hivi tunajua federal reserve kwenye dhahabu ni kiasi gani? Ukipata takwimu zake utatamani ujinyonge... Mmarekani hagusi vyake kabisa... Angalia mafuta anayo lakini hachimbi kila siku anahangaika na mafuta ya waarabu
a16c7de8e74b1adba03a131cf6f46f22.jpg

Mmarekani anakopa kwa akili, angalia mauzo yake ya silaha kwa mwaka duniani... Anakopa BILIONI kumi .. Anatengeza silaha anaziuza kwa BILIONI 20... Huyo sio mwenzako.. USIJIFANANISHE NAYE KABISA...
Tusidumazwe na hizi akili za kukopakopa na misemo ya kujifariji kwamba usipodaiwa huaminiki... Huheshimiki.. Uchumi wetu unajikongoja.. Tusiongeze matatizo ya madeni ya mikopo tena hii ya kukopa mia tano riba mia nne....

Tuwe na tafakuri

Deni La Marekani ni sh ngapi. Ok tuache hayo. Unakosoa kwa nia gani ya kama kawaida yako kumpinga Rais. Unataka kutuambia Rais kama JPM na Sio Taasisi imekopa. Je umeangalia nia ya mkopo. Huwa ajenda zenu mkianza kuandika mnakuwa kwanza na chuki zile za Sisi kina mama au unakuwa na nia tu ya kusubiri kukosoa tena JF ili wanabavicha mpate uwanja Wa kutoa prejudices zenu. Lini umesifia. Katika Nchi za africa zenye wezi wengi jitahidini kupima nia ya viongozi wenu .mnakaa hapa mnasahau historia mpo tu na ajenda zenu zenye majibu kwanza. Eti mnajadili hapa hamjadili mnapiga Majungu. Mana mna majibu yenu. So sad so stupid so disheartening.
 
Wenzetu wanakopa na kukopesheka kwakuwa wana hakiba kubwa sana ya dhahabu wamechimbia chini ya vaults za siri kwenye bank zao... Wanajua thamani yake.. Na hii dhahabu kwa sehemu kubwa inatoka Afrika .. Wakishatuibia vito vyetu kwa mlango wa nyuma kisha wanakuja mlango wa mbele kwa kujifanya kutoa misaada na mikopo yenye masharti (nafuu!?) Halafu tunakenua meno na kuwasifu sana tunawaita WADAU WA MAENDELEO...
da24056b9da7dd54954c731c83a740bb.jpg
Hizi nchi zina utajiri mkubwa ukiondoa dhahabu tu company zao zina generate pesa nyingi sana niliona article moja kama kampuni ya apple ingekuwa ni nchi basi ingekuwa na 42 duniani sasa hiyo ni moja tu ya kampuni.
 
Sasa hiyo mikopo inafanya kazi gani maana Kama treni alisema anatumia hela za ndani na bajeti ikapita kwa mbwembwe kuwa hela za tra , zile hell feki ndio zitatumika kujenga.

Barbara nyingi bado zajenga kwa hisani ya Japan na watu wa marekani

Tofauti na hapo hakuna kingine kipya chenye uhitaji wa hela nyingi

Tukiangalia hilo ongezeko la 16pc ndani ya mwaka mmoja ni ukweli kuwa tunadanganywa na serikali yetu kuhusiana na makusanyo ya tra

Ndege zimekamatwa muda sasa Kama hela ingekuwepo Nina hakika wangelipwa kwa ngebe sana

Aliwadanganya wajinga wengi kua tanzania ni donor country kwa kusahau maneno yake akaja kukiri kuwa tajiri lazima akope

Hapo hajui kuwa tajiri mkopo wake unaweza kuwa wa OD au LC ya miezi 3 ambayo servicing ni ndogo

Mikopo hi twaikopa kwa dollar na tsh inshuka thamani hivyo tutajikuta twalipa madafu mengi sana

Kuna vitu vilivyokula hela za nchi ila hatuambiwi bajeti ilitokea wapi na sh ngapi zilitumika
Makinikia saga
Halafu kuhusu ndege si investment mimi ningeomba kwa sababu zilikuwa pesa za mikopo waje na data Air Tz tumepata pesa kiasi hichi na matumizi kiasi hichi ilitujuwe kama tunatengeneza faida au hasara ila kama tunatumia ndege kama mtaji wa kisiasa tuna hasara maana kila speech nasikia tumenunua ndege utasema ni Airbus 380 kumbe vindege hata watu binafsi wanamiliki.
 
Deni La Marekani ni sh ngapi. Ok tuache hayo. Unakosoa kwa nia gani ya kama kawaida yako kumpinga Rais. Unataka kutuambia Rais kama JPM na Sio Taasisi imekopa. Je umeangalia nia ya mkopo. Huwa ajenda zenu mkianza kuandika mnakuwa kwanza na chuki zile za Sisi kina mama au unakuwa na nia tu ya kusubiri kukosoa tena JF ili wanabavicha mpate uwanja Wa kutoa prejudices zenu. Lini umesifia. Katika Nchi za africa zenye wezi wengi jitahidini kupima nia ya viongozi wenu .mnakaa hapa mnasahau historia mpo tu na ajenda zenu zenye majibu kwanza. Eti mnajadili hapa hamjadili mnapiga Majungu. Mana mna majibu yenu. So sad so stupid so disheartening.
Kama GT nakuona wewe hopeless kabisa,badala ya kujibu hoja na kutoa solutions unaleta majungu na malawama ya kijinga.Mbaya zaidi unaingiza mambo ya vyama katika huu mjadala wa kitaifa.Kwa akili zako unafikiri Hazina wanaweza kukopa fedha bila rais ku Approve?.Yaani leo wizara wakurupuke tu kukopa bila kupeleka proposal kwa rais?..
Halafu mlivyo na craps,mambo mazuri yakifanyika hamsemi ni taasisi,mnamsifia rais moja kwa moja.Ila haya magumu mnamtoa na kusema oooh ni taasisi imekopa,hiyo taasisi ipo chini ya Duka la Mangi au?.Em kuweni serius bana.
 
Kwasasa hatuna jinsi zaidi tu ya kushauri kwa weledi, bila dhihaka, bila chuki bila kubeza
Mungu akutie nguvu kwa hili. Pia waandishi wa habari wasio woga ni watu muhimu sana ktk kufikisha ujumbe. Nikupe mfano. Kipindi cha vita ya wahujumu uchumi (chini ya Hayati Sokoine)kati ya 1982-1983 kuna swali aliulizwa Mwl. Nyerere kwenye interview likapelekea kusitisha operation ile. Kama sijakosea aliulizwa swali moja la kimantiki na mwandishi mmoja maarufu aliitwa Peter Enahoro wa gazeti la Afrca Now. Maswali "Je,mnapokamata pesa na mali za wafanyabiashara na kuzitaifisha ni halali?" Mwl akauliza kwa nini unaniuliza vile? Akamjibu,ni vyema wakatendewa haki! AkamuulizaMwl,hivi katika mfumo wako wa siasa ya ujamaa,ni kiasi gani cha pesa kisheria mfanyabiashara anatakiwa kukimiliki ili asiitwe mhujumu uchumi? Akaendelea,je kama nchi huru,hamuoni ni kosa, kumhukumu mtu kwa kosa ambalo hamjaliwekea sheria yoyote? Kiujumla maswali hayo,yalimfanya Mwl abadili uelekeo na akamjibu yule mwandishi "I wish you could be a good critic by starting there, and I agree with you that we made a mistake"

Sent from my H8501 using JamiiForums mobile app
 
Aliyeshauri tuchukue huu mkopo na bila hata kulishirikisha bunge sijui aliwaza nini... Na aliyekubali pia mkopo wa riba kama hii naamini hajushauriwa vema... Unajua wapiga dili wako kila mahali na kwenye kila viwango vya maisha... Nina wasiwasi huu mkopo uliingiliwa na madalali na inawezekana kabisa ndio walijenga hoja zenye ushawishi mkubwa mpaka ndugu zetu wakalainika na kukubali
nakuelewa sana mkuu
 
Mimi sina shida na mikopo. Maana as a matter of fact, Tanzania hatuna uchumi wa kuweza kusustain huge infrastructure development kama barabara, reli, ndege nk. Swali tunakopa kufanya nini? na accountability iko vipi?

Mshana make no mistake, huko nyuma tumekopa hela nyingi sana but we got nothing to show for it. Nyingi wamekula wajanja. Now kama JPM anakopa na hela tunaiona inakokwenda, basi mimi sina shida kabisa. Maana hata wajukuu na vizazi vyetu vitalipa tuu. In fact baada ya vita ya pili ya dunia Europe ilikopa hela nyingi sana. Lakini unaona walichokifanya.

Tusiwe na mawazo kwamba tukikopa maendeleo ni kwa ajili ya kizazi chetu. Hapana. Anachokifanya JPM..watakaofaidi ni vizazi baada ya miaka 50! Mimi na wewe hatutakuwepo!
 
Deni La Marekani ni sh ngapi. Ok tuache hayo. Unakosoa kwa nia gani ya kama kawaida yako kumpinga Rais. Unataka kutuambia Rais kama JPM na Sio Taasisi imekopa. Je umeangalia nia ya mkopo. Huwa ajenda zenu mkianza kuandika mnakuwa kwanza na chuki zile za Sisi kina mama au unakuwa na nia tu ya kusubiri kukosoa tena JF ili wanabavicha mpate uwanja Wa kutoa prejudices zenu. Lini umesifia. Katika Nchi za africa zenye wezi wengi jitahidini kupima nia ya viongozi wenu .mnakaa hapa mnasahau historia mpo tu na ajenda zenu zenye majibu kwanza. Eti mnajadili hapa hamjadili mnapiga Majungu. Mana mna majibu yenu. So sad so stupid so disheartening.
kwa kauli yako hii nawe unaonekana umepanic
 
mshana jr hivi hawezi kuundwa kamati tukamalizana na huyu mtu.au analindwa na wataalam kutoka Nigeria.wanganga ilikuwa zamani naona haya mateso hayavumiliki
 
Ndio mlipe kodi otherwise tutawabebesha mzigo mzito kizazi kijacho maana siye tunakufa makesho tu
 
Hivi nchi hii tutaacha ujinga lini? Maana tuna midhahabu situichimbe nasiye iwekwe reserve tu
 
Mungu akutie nguvu kwa hili. Pia waandishi wa habari wasio woga ni watu muhimu sana ktk kufikisha ujumbe. Nikupe mfano. Kipindi cha vita ya wahujumu uchumi (chini ya Hayati Sokoine)kati ya 1982-1983 kuna swali aliulizwa Mwl. Nyerere kwenye interview likapelekea kusitisha operation ile. Kama sijakosea aliulizwa swali moja la kimantiki na mwandishi mmoja maarufu aliitwa Peter Enahoro wa gazeti la Afrca Now. Maswali "Je,mnapokamata pesa na mali za wafanyabiashara na kuzitaifisha ni halali?" Mwl akauliza kwa nini unaniuliza vile? Akamjibu,ni vyema wakatendewa haki! AkamuulizaMwl,hivi katika mfumo wako wa siasa ya ujamaa,ni kiasi gani cha pesa kisheria mfanyabiashara anatakiwa kukimiliki ili asiitwe mhujumu uchumi? Akaendelea,je kama nchi huru,hamuoni ni kosa, kumhukumu mtu kwa kosa ambalo hamjaliwekea sheria yoyote? Kiujumla maswali hayo,yalimfanya Mwl abadili uelekeo na akamjibu yule mwandishi "I wish you could be a good critic by starting there, and I agree with you that we made a mistake"

Sent from my H8501 using JamiiForums mobile app

Mkuu wengi tumeikatia tamaa nchi yetu kwa sababu ya figisu figisu za watawala. As a matter of fact, tulikuwa tumefika pabaya. WaTanzania kama binadamu wengine tuna deni kwa vizazi vyetu vijavyo. Mfano tukijenga reli, you can be sure kwamba barabara zitadumu miaka na miaka. Kwa hiyo hizo billions za maintenance tutazielekeza kwingine.

Mimi nasema tukope tuu-kwa uangalifu. Lakini tuweke oversight mechanism kujua hela tuliyokopa imekwenda wapi. Tatizo kubwa nchi ya watu masikini kama yetu kila mtu anataka faida aipate there and then. Ni kama shule, unaenda darasani miaka zaidi ya 20 hujaiona faida. Yeti ukienda Arusha mwana apolo wa mererani au mfanya biashara atakuona mjinga kwenda shule kupoteza mda....wakati ungefanya biashara hela ukipata bila kwenda shule. Leo hii aliyesoma miaka 20 ndo mwenye nafuu. Ambaye hakufoji cheti ndo mwenye nafuu. It is life. Shortcut hailipi popote pale.

Nimekaa JF miaka mingi kidogo. Binadamu ndivyo tulivyo.

Nakumbuka Mkapa tulimnanga sana. Tukimuita fisadi (refer kujiuzia mchuchuma et al, kuuza mashrika ya umma..nk). JK ndo usiseme tulimtukana sana kama mtu anayeendekeza rushwa na kutetea marafiki zake-very weak President! Threads zimo humu JF!

Sasa leo tuna JPM bado lawama ziko pale pale......tusipoangalia wengine tutastaafu tukiwa hatujaona lolote jema kwenye nchi yetu! And that will be a loss! to the nation and ourselves.
 
Hongera sana mshana kwa huu uzi ambao ni ukweli mtupu, ila usishangae wenye 'peo finyu au bendera fuata upepo'akaanza kukushambulia kuwa wewe sio mzalendo au mchochezi.
 
Back
Top Bottom