Sikubaliani kamwe na hili la "Bado tunakopesheka"


Mshana Jr

Mshana Jr

JF-Expert Member
Joined
Aug 19, 2012
Messages
102,334
Likes
120,754
Points
280
Mshana Jr

Mshana Jr

JF-Expert Member
Joined Aug 19, 2012
102,334 120,754 280
NAOMBA NIKOSOE KWA WELEDI
Mkopo una pande mbili hasi na chanya.... Mkopo hasi ni ule unaotumika mambo yanaposhindikana kabisa.

Mkopo chanya ni ule mkopo unaokopa kufanyia jambo la maendeleo.. Lakini vyovyote iwavyo mkopo ni utumwa Jambo lingine kwenye mkopo ni hili.

Unakopa wapi, unamkopa nani, kwa masharti yapi, kwa muda gani na kwa riba kiasi gani... Kuna mikopo ina masharti magumu na riba kubwa.

Kwenye mikopo pia kuna makubaliano, je familia inajua? Je mmeshauriana na kukubaliana?

Hiki ni kigezo muhimu pia... Zaidi usipende kujifananisha na wengine , ati kwakuwa tu mimi nimekopa tena mkopo mrefu basi na wewe uniige... Hujui nguvu yangu ya kulipa ikoje.

Kama nchi naweza kusema tumekengeuka kwenye hili la mikopo na hii misaada, kwakuwa tumekuwa wakurupukaji mno na hatutendi kwa weledi.

Ni kweli kabisa wenzetu wana mikopo mirefu lakini ina faida kubwa na riba yao pengine ni ndogo sana.

Halafu WAMESHAURIANA NA KUKUBALIANA, Nimeshtushwa na kusononeka moyoni kwamba barabara ya uhuru ilijengwa kwa mkopo na tumechukua zaidi ya miaka 40 kuumaliza kulipia. Hapa mkopeshaji Kala riba ma faida ya kufuru.

Mchina alijikongoja kwa miguu yake mpaka akasimama... Leo ndio mkopeshaji mkubwa wa mataifa mengi akiwamo mmarekani.Kwahiyo si kweli kwamba usipokopa hutaendelea.

Mimi nasema (I stand to be correct) tuondokane na haya mawazo ya kukopakopa.... Hatutafika popote... Tuwe na mawazo mapya ya kuja kuwa taifa linalokopesha kuliko hii ideology ya kusema bado tunakopesheka...!!!

TUJIFUNZE KUJITEGEMEA na kama ni kukopa tukope kidogo sana tena kwa makubaliano halafu tukope kwenye taasisi zenye masharti nafuu na riba ndogo
Tusimuige Mjapani hatujui mikopo yake masharti yake yakoje Lakini tuangalie Mjep yuko wapi.

Tusijilinganishe kabisa na yeye kwakuwa pamoja na kukopa sana almost alisimia 200 ya pato lake la taifa. Lakini ni mmojawapo wa nchi zinazoongoza kutoa misaada Tanzania na mikopo ya masharti nafuu.... Tuwe na tafakuri kwenye hili wenzetu wametuzidi sana.

Isije kuwa wanakopa kwa riba ndogo sana halafu mkopo huohuo wanatukopesha sisi kwa riba ya juu halafu anakula commission. Mjapani sio mpumbavu atoe chakula chake ampe mgeni.

Tusimuige mmarekani, huyo ndio kabisaaa sio level yetu... Hivi tunajua federal reserve kwenye dhahabu ni kiasi gani?

Ukipata takwimu zake utatamani ujinyonge. Mmarekani hagusi vyake kabisa Angalia mafuta anayo lakini hachimbi kila siku anahangaika na mafuta ya waarabu
a16c7de8e74b1adba03a131cf6f46f22.jpg

Mmarekani anakopa kwa akili, angalia mauzo yake ya silaha kwa mwaka duniani.

Anakopa BILIONI kumi .. Anatengeza silaha anaziuza kwa BILIONI 20... Huyo sio mwenzako.. USIJIFANANISHE NAYE KABISA.

Tusidumazwe na hizi akili za kukopakopa na misemo ya kujifariji kwamba usipodaiwa huaminiki... Huheshimiki.

Uchumi wetu unajikongoja. Tusiongeze matatizo ya madeni ya mikopo tena hii ya kukopa mia tano riba mia nne.

Tuwe na tafakuri
 
mwekundu

mwekundu

JF-Expert Member
Joined
Mar 4, 2013
Messages
20,848
Likes
10,022
Points
280
mwekundu

mwekundu

JF-Expert Member
Joined Mar 4, 2013
20,848 10,022 280
Ha ha sisi tunakopa ili tule ,
Halafu watu wanataka wapate credit kwa deni letu wenyewe

"Utasikia tumejenga barabara km ..kadhaa nani kama ccm"

Siku mtanzania akiamka kutoka usingizini vizazi vya watu wa ccm vina tuhuma za kujibu
 
Sibonike

Sibonike

JF-Expert Member
Joined
Dec 23, 2010
Messages
11,704
Likes
6,804
Points
280
Sibonike

Sibonike

JF-Expert Member
Joined Dec 23, 2010
11,704 6,804 280
Ili uwe donor country lazima ukope sana. Teh teh teh.
Kopa mwanangu, kufa kwaja. Kopa kama vile hakuna kesho.
 
Mshana Jr

Mshana Jr

JF-Expert Member
Joined
Aug 19, 2012
Messages
102,334
Likes
120,754
Points
280
Mshana Jr

Mshana Jr

JF-Expert Member
Joined Aug 19, 2012
102,334 120,754 280
Ha ha sisi tunakopa ili tule ,
Halafu watu wanataka wapate credit kwa deni letu wenyewe

"Utasikia tumejenga barabara km ..kadhaa nani kama ccm"

Siku mtanzania akiamka kutoka usingizini vizazi vya watu wa ccm vina tuhuma za kujibu
Wenzetu wanakopa na kukopesheka kwakuwa wana hakiba kubwa sana ya dhahabu wamechimbia chini ya vaults za siri kwenye bank zao... Wanajua thamani yake.. Na hii dhahabu kwa sehemu kubwa inatoka Afrika .. Wakishatuibia vito vyetu kwa mlango wa nyuma kisha wanakuja mlango wa mbele kwa kujifanya kutoa misaada na mikopo yenye masharti (nafuu!?) Halafu tunakenua meno na kuwasifu sana tunawaita WADAU WA MAENDELEO...
da24056b9da7dd54954c731c83a740bb.jpg
 
R

Retired

JF-Expert Member
Joined
Jul 22, 2016
Messages
15,338
Likes
20,469
Points
280
Age
21
R

Retired

JF-Expert Member
Joined Jul 22, 2016
15,338 20,469 280
Ha ha sisi tunakopa ili tule ,
Halafu watu wanataka wapate credit kwa deni letu wenyewe

"Utasikia tumejenga barabara km ..kadhaa nani kama ccm"

Siku mtanzania akiamka kutoka usingizini vizazi vya watu wa ccm vina tuhuma za kujibu
Watanzania hawawezi kuamka, wamelaaniwa. Kama Wahaya, Nshomile jana walikuwa wanamshangilia, wamesahau tetemeko, basi ujue sisi ni mbuzi mbuzi!
 
R

Retired

JF-Expert Member
Joined
Jul 22, 2016
Messages
15,338
Likes
20,469
Points
280
Age
21
R

Retired

JF-Expert Member
Joined Jul 22, 2016
15,338 20,469 280
Wenzetu wanakopa na kukopesheka kwakuwa wana hakiba kubwa sana ya dhahabu wamechimbia chini ya vaults za siri kwenye bank zao... Wanajua thamani yake.. Na hii dhahabu kwa sehemu kubwa inatoka Afrika .. Wakishatuibia vito vyetu kwa mlango wa nyuma kisha wanakuja mlango wa mbele kwa kujifanya kutoa misaada na mikopo yenye masharti (nafuu!?) Halafu tunakenua meno na kuwasifu sana tunawaita WADAU WA MAENDELEO...
da24056b9da7dd54954c731c83a740bb.jpg
nasikia oil reserves za mmarekani ni the biggest duniani! Is this true? (yale ambayo hayajachimbwa)
 
Kididimo

Kididimo

JF-Expert Member
Joined
Sep 20, 2016
Messages
2,276
Likes
1,521
Points
280
Kididimo

Kididimo

JF-Expert Member
Joined Sep 20, 2016
2,276 1,521 280
NAOMBA NIKOSOE KWA WELEDI
Mkopo una pande mbili hasi na chanya.... Mkopo hasi ni ule unaotumika mambo yanaposhindikana kabisa... Mkopo chanya ni ule mkopo unaokopa kufanyia jambo la maendeleo.. Lakini vyovyote iwavyo mkopo ni utumwa
Jambo lingine kwenye mkopo ni hili.... Unakopa wapi, unamkopa nani, kwa masharti yapi, kwa muda gani na kwa riba kiasi gani... Kuna mikopo ina masharti magumu na riba kubwa.
Kwenye mikopo pia kuna makubaliano, je familia inajua? Je mmeshauriana na kukubaliana? Hiki ni kigezo muhimu pia... Zaidi usipende kujifananisha na wengine , ati kwakuwa tu mimi nimekopa tena mkopo mrefu basi na wewe uniige... Hujui nguvu yangu ya kulipa ikoje...
Kama nchi naweza kusema tumekengeuka kwenye hili la mikopo na hii misaada, kwakuwa tumekuwa wakurupukaji mno na hatutendi kwa weledi.... Ni kweli kabisa wenzetu wana mikopo mirefu lakini ina faida kubwa na riba yao pengine ni ndogo sana... Halafu WAMESHAURIANA NA KUKUBALIANA.... Nimeshtushwa na kusononeka moyoni kwamba barabara ya uhuru ilijengwa kwa mkopo na tumechukua zaidi ya miaka 40 kuumaliza kulipia.... Hapa mkopeshaji Kala riba ma faida ya kufuru....
Mchina alijikongoja kwa miguu yake mpaka akasimama... Leo ndio mkopeshaji mkubwa wa mataifa mengi akiwamo mmarekani.. Kwahiyo si kweli kwamba usipokopa hutaendelea
Mimi nasema (I stand to be correct) tuondokane na haya mawazo ya kukopakopa.... Hatutafika popote... Tuwe na mawazo mapya ya kuja kuwa taifa linalokopesha kuliko hii ideology ya kusema bado tunakopesheka...!!! TUJIFUNZE KUJITEGEMEA na kama ni kukopa tukope kidogo sana tena kwa makubaliano halafu tukope kwenye taasisi zenye masharti nafuu na riba ndogo
Tusimuige Mjapani hatujui mikopo yake masharti yake yakoje... Lakini tuangalie Mjep yuko wapi.. Tusijilinganishe kabisa na yeye kwakuwa pamoja na kukopa sana almost alisimia 200 ya pato lake la taifa... Lakini ni mmojawapo wa nchi zinazoongoza kutoa misaada Tanzania na mikopo ya masharti nafuu.... Tuwe na tafakuri kwenye hili... Wenzetu wametuzidi sana... Isije kuwa wanakopa kwa riba ndogo sana halafu mkopo huohuo wanatukopesha sisi kwa riba ya juu halafu anakula commission... Mjapani sio mpumbavu atoe chakula chake ampe mgeni
Tusimuige mmarekani, huyo ndio kabisaaa sio level yetu... Hivi tunajua federal reserve kwenye dhahabu ni kiasi gani? Ukipata takwimu zake utatamani ujinyonge... Mmarekani hagusi vyake kabisa... Angalia mafuta anayo lakini hachimbi kila siku anahangaika na mafuta ya waarabu
a16c7de8e74b1adba03a131cf6f46f22.jpg

Mmarekani anakopa kwa akili, angalia mauzo yake ya silaha kwa mwaka duniani... Anakopa BILIONI kumi .. Anatengeza silaha anaziuza kwa BILIONI 20... Huyo sio mwenzako.. USIJIFANANISHE NAYE KABISA...
Tusidumazwe na hizi akili za kukopakopa na misemo ya kujifariji kwamba usipodaiwa huaminiki... Huheshimiki.. Uchumi wetu unajikongoja.. Tusiongeze matatizo ya madeni ya mikopo tena hii ya kukopa mia tano riba mia nne....

Tuwe na tafakuri
Mshana jr. Naona umeanzisha kongamano kiaina. Inaonyesha kuna wengi wa aina yako wanalitakia mema Taifa letu lakini wanaogopa kujitokeza hivi. Nini kifanyike?
 
M

MENGELENI KWETU

JF-Expert Member
Joined
Oct 23, 2013
Messages
7,636
Likes
16,883
Points
280
M

MENGELENI KWETU

JF-Expert Member
Joined Oct 23, 2013
7,636 16,883 280
Tanzania tunakopa bila akili..

Kila nikikumbuka ule mkopo tuliokopa kwenye Bank ya Uswiss wa USD MIL 500 ambao tutalipa USD MIL 900 na ni mkopo wa muda mfupi..

Kuna akili gani hapo imetumika na wataalamu wa fedha??

More worse serikalini hakuna discipline ya matumizi.
 
Mshana Jr

Mshana Jr

JF-Expert Member
Joined
Aug 19, 2012
Messages
102,334
Likes
120,754
Points
280
Mshana Jr

Mshana Jr

JF-Expert Member
Joined Aug 19, 2012
102,334 120,754 280
Mshana jr. Naona umeanzisha kongamano kiaina. Inaonyesha kuna wengi wa aina yako wanalitakia mema Taifa letu lakini wanaogopa kujitokeza hivi. Nini kifanyike?
Kwasasa hatuna jinsi zaidi tu ya kushauri kwa weledi, bila dhihaka, bila chuki bila kubeza
 
Mshana Jr

Mshana Jr

JF-Expert Member
Joined
Aug 19, 2012
Messages
102,334
Likes
120,754
Points
280
Mshana Jr

Mshana Jr

JF-Expert Member
Joined Aug 19, 2012
102,334 120,754 280
Tanzania tunakopa bila akili..

Kila nikikumbuka ule mkopo tuliokopa kwenye Bank ya Uswiss wa USD MIL 500 ambao tutalipa USD MIL 900 na ni mkopo wa muda mfupi..

Kuna akili gani hapo imetumika na wataalamu wa fedha??

More worse serikalini hakuna discipline ya matumizi.
Aliyeshauri tuchukue huu mkopo na bila hata kulishirikisha bunge sijui aliwaza nini... Na aliyekubali pia mkopo wa riba kama hii naamini hajushauriwa vema... Unajua wapiga dili wako kila mahali na kwenye kila viwango vya maisha... Nina wasiwasi huu mkopo uliingiliwa na madalali na inawezekana kabisa ndio walijenga hoja zenye ushawishi mkubwa mpaka ndugu zetu wakalainika na kukubali
 

Forum statistics

Threads 1,238,981
Members 476,289
Posts 29,338,895