Nilikuwa na uhusiano na mpenzi wangu kwa muda wa miaka 2 lakini niliachana nae baada ya kugundua ananisaliti baada ya yeye kukiri kunisaliti kiukweli niliumia sana ila niliamua kumwacha maana alionyesha kuendelea na jamaa ingawa baada ya miezi 2 waliachana.Katika uhusiano wetu nilishamvisha pete ya uchumba na kwao walikuwa wananifahamu,kibaya wakati tunaachana nilimtumia meseji nikimwambia yeye ni malaya na hii ilitokana na hasira za kuumizwa na kiukweli najifahamu sio mtu wa matusi.Alichofanya ni kumwonyesha mama yake na ndugu zake kuwa ameachana na mimi kutokana na mimi kumtukana kila siku na kwao nikaonekana sio mstarabu,mama yake alinilaumu na hakuamini lolote nililomwambia.Tangu siku hiyo sikumtafuta na yeye hajanitafuta na sasa ni miezi 3 imepita hatujawasiliana na mimi sioni kama ni ustarabu lakini sitaki kumtafuta maana ataona najishusha sana kwake ila kibaya namkumbuka sana,naombeni ushauri wenu maana nishamzoea sana