Siku za kujifungua zimepitiliza, msaada.

tumaini obedi

JF-Expert Member
Jun 17, 2013
340
190
habari wa ndugu,

mke wangu ana ujauzito , ambao makisio ya kujifungua yalikuwa mwezi wa tatu tarehe 14,
hata hivyo taarifa zakiliniki zilitushitua pale walipo sema kuwa katoto ni kadogo sana na kanaonekana kama vile ni ka wiki 28,,,,hii ni taarifa ya kama wiki mbili zilipita.

baada ya hapo tulipiga moyo konde na kuamua kwenda kwa dakitari wa akina mama [ specialist]
Doctor alituhoji maswali mengi, baadhi aliuza tarehe ya mwisho ya hedhi ilikuwa lini?, tukamwambia tarehe 6/6/2016,,,,je?, mtoto anacheza jibu ndio, .....baada ya hapo akalala mama kitandani akamuwekia kakifaa hivi, kama kabomba halafu akashika na tumbo, akasema mbona tumbo ndogo?, halafu na mtoto kama vile hajaingia kwenye nyonga...tusituka tena .

baada ya hapo , akatuandikia vipimo 2, utral sound kuangalia mtoto yuko je?, na kingine cha kupima mapigo ya moyo wa mtoto....

matokeo, mtoto hana tatizo na ana kilo 3.2kg na anapumua vizuri lakini akasema placenta imeanza kuchoka.......tukaandikiwa tarehe ya kurudi yaani leo [ 9 / 3/4 / 17,] jioni saa 12, ili alazwe na awekewe dilipu za uchungu wa kujifungua.

USHAURI NINAOMBA....mama anaoneka mwenye nguvu , je? tunaweza subiri mpaka mama apate
uchungu wa kawaida wa kujifungua?.
make tunaongopa huenda kama atawekewa dilipu na asifunguke njia .kifuatacho kinaweza kuwa operation......ujauzito mpaka sasa una zaidi ya wiki 43

naombeni ushauri wenu

up to dates..................heshima kwenu [ amejifungua tayari

asanteni.ndugu wana JF ......ninayofuraha iliyopita kikomo, kuwataarifu hatimaye wife amejifungua,,,,jioni ya leo saa...9.30 mchana.
salama kbs.......mimba hii ilikuwa ya aina yake, ukilinganisha na mimba zilizopita ,

kwanza kbs tulianza kupata wasiwasi tangu mimba ina miezi mitano,,,,,na tulienda kwa daktari , make, mama alikuwa hahisi kitu chote tumboni mwake,,,,,,,,,,,,,,dk alitwambia mtoto ni mzima na hana shd yoyote...baada vipimo.

leo ,,,pindi anajifungua ,,,,,,Nesi aliyemsaidia amemwambia inaonekana mimba ilikimbilia kifuani.......amepata shd kweli kweli....baada ya kuonekana dilip za uchungu zinataka kugonga mwamba, mpaka wakaamua ,kurazimishai kuvuja chupa.

amejifungua kwa njia ya kawaida kabisa...........japo kwa pinde.....na mushuru Mungu sana sana....................kuazia mimba ya tano nasikia ipo shughuri.

wana JF, binafsi sitawasahau hata kidogo, ambavyo mumenipa ushauri nn?,,,kifanyike nawashuru sana......na sikujua kama JF kuna masaada wa kiasi hiki.....make mara nyingi mimi huwa naishia kule JAMII FORUMS SIASA.....lakini dahaaaaa...asanteni sana.

mimi na mwenzangu, mpango wetu ulikuwa watoto wanne ,sasa tunao...wanatosha kbs.

tunaye mvulana wa miaka ......17, wa kwanza huyu.
wapili mvulana wa miaka........13,
watatu alizaliwa mwaka 2011 naye alikuwa mvulana alifariki,,,,alizaliwa akiwa na tatizo la moyo ,na upumuaji haukuwa muzuri.

wanne ni mvulana ana anakaribia maiaka mitano.

NA HUYU WA LEO [ 13/4/17.......ambaye ni wakike.
.......namushukuru Mungu sana.......pasaka nitaila vizuri.

asanteni.'
 
Pole sana mkuu.. Yani mtoto mwenye kilo 3.2 na wiki 43. Nendeni hospitalit na mungu atawasaidia..
 
Kanisabla walokole na kama yuko hospital chukua nguo yoyote ipeleke ikaombewe then ukampelekee aivae,,kama kitenge au kanga
 
Poleni Sana
Sina ujuzi WA masuala hayo Ya uzazi, ningewashauri vizuri tu maana unahitaji msaada mkubwa sana
Mungu awalinde....!!
Na wataalamu waje wakushauri yaliyo mema....!!
 
habari wa ndugu,

mke wangu ana ujauzito , ambao makisio ya kujifungua yalikuwa mwezi wa tatu tarehe 14,
hata hivyo taarifa zakiliniki zilitushitua pale walipo sema kuwa katoto ni kadogo sana na kanaonekana kama vile ni ka wiki 28,,,,hii ni taarifa ya kama wiki mbili zilipita.

baada ya hapo tulipiga moyo konde na kuamua kwenda kwa dakitari wa akina mama [ specialist]
Doctor alituhoji maswali mengi, baadhi aliuza tarehe ya mwisho ya hedhi ilikuwa lini?, tukamwambia tarehe 6/6/2016,,,,je?, mtoto anacheza jibu ndio, .....baada ya hapo akalala mama kitandani akamuwekia kakifaa hivi, kama kabomba halafu akashika na tumbo, akasema mbona tumbo ndogo?, halafu na mtoto kama vile hajaingia kwenye nyonga...tusituka tena .

baada ya hapo , akatuandikia vipimo 2, utral sound kuangalia mtoto yuko je?, na kingine cha kupima mapigo ya moyo wa mtoto....

matokeo, mtoto hana tatizo na ana kilo 3.2kg na anapumua vizuri lakini akasema placenta imeanza kuchoka.......tukaandikiwa tarehe ya kurudi yaani leo [ 9 / 3/4 / 17,] jioni saa 12, ili alazwe na awekewe dilipu za uchungu wa kujifungua.

USHAURI NINAOMBA....mama anaoneka mwenye nguvu , je? tunaweza subiri mpaka mama apate
uchungu wa kawaida wa kujifungua?.
make tunaongopa huenda kama atawekewa dilipu na asifunguke njia .kifuatacho kinaweza kuwa operation......ujauzito mpaka sasa una zaidi ya wiki 43

naombeni ushauri wenu
asanteni.
Pole mkuu kwa taharuki hiyo. Kwa kawaida haitakiwi kuvuka wiki arubaini na mbili. Ushauri asiwekewe maji ya uchungu bali fanyeni arrangement ya operation. Kama placenta inaonekana ineanza kuchoka sidhani kama ni salama kuendelea kusubiri.. Kitu kikubwa kabisa mzidishe maombi Mungu ni mwema ataweka mkono wake.
 
Mda wake wa kukaa tumboni ukiisha atatoka tu ila mjiandae na chupa za kumuongezea damu mama issue yako si ngeni kabisa
 
kwa umri huo wa mimba nashauri afanyiwe operation straight kwa kua placenta kuchoka ni dalili mbaya kwa kua halitaweza kuhimili kupeleka oxygen kwa mtoto uchungu ukianza
 
Kg 3.2 cyo ndogo sana kulingana na umri wa mimba japo kikawaida alitakiwa afikie angalau 3.5
Ultrasound huwa inaonyesha umri wa mtoto interm of weeks ( gestational age) je ilionyesha umri gani
Kwani kuna cases nyingi za wamama kusahahu tarehe ya mwisho ya hedh (last normal mestrual period)
 
Mkuu msingoje aanze kupata uchungu wa kawaida na kama mmeshaambiwa placenta imeanza kuchoka,chakufanya ni kwenda hospital na option nzur ya huyo mama kujifungua ni kwa c/section ili kuepuka complications ambazo zinaweza kujitokeza kama placenta kuanza kujiengua
 
asante...c/section ..ndio nn?
 
Kg 3.2 cyo ndogo sana kulingana na umri wa mimba japo kikawaida alitakiwa afikie angalau 3.5
Ultrasound huwa inaonyesha umri wa mtoto interm of weeks ( gestational age) je ilionyesha umri gani
Kwani kuna cases nyingi za wamama kusahahu tarehe ya mwisho ya hedh (last normal mestrual period)
sidhani kama kutakuwa kusahau make hii ni ya tano....tunao uzofu,,,,,labda siju , make kidogo waligusia na umri [ana miaka 35],,, na mimba za nyuma hazina shd kbs,,,,,nilisahau kuuliza utral sound imeditekiti wiki ng?......nilikuwa ninampango wa kurudi niulize na hilo,,,,,, asante
 
asante
Pole mkuu kwa taharuki hiyo. Kwa kawaida haitakiwi kuvuka wiki arubaini na mbili. Ushauri asiwekewe maji ya uchungu bali fanyeni arrangement ya operation. Kama placenta inaonekana ineanza kuchoka sidhani kama ni salama kuendelea kusubiri.. Kitu kikubwa kabisa mzidishe maombi Mungu ni mwema ataweka mkono wake.
.
 
Kaka shituka,,mpeleke akaombewe any church la kiroho plz,,tena inuka now

Acha kumpotosha!

Kuna Wakati mwingine unataka kumfanyia Operation Mama Mjamzito unampa form kusaini anakataa mpaka ampigie Mchungaji amuulize ambae hayupo eneo la tukio wala Hana utaalam wowote wa Fani hiyo.

Zikizid Wiki 40 na bado Hakuna dalili za uchungu Mpeleke hospital na kuna uwezekano akawekewa vidonge vya uchungu kule chini
 
Pole mkuu ,ombeni sana mtafunguliwa,pia muwe karibu na hospitali kwa msaada wa kitaalamu...mtoto atazaliwa salama muondoe hofu..Mungu awabariki.
 
Back
Top Bottom