Siku za Hussein Bashe ndani ya CCM zinahesabika!

Siku za Hussein Bashe ndani ya CCM zinahesabika!

_MG_6086.jpg
Bashe sio mnafiki.
 
Me naona kama wanamchelesha sana, ningekuwa me mwenyekiti ningeshampiga chin siku ming aende kwa wenzake huko ufipa
 
Dah..mzee mda mwingine ni vema kutofautiana na chama ili utete watanzania wengi zaid...kwani Lazima ufie kwenye chama kimoja? Alichokifanya Bashe utakikumbuka apo mbeleni..kwa sasa we tulia tu..Hongera Bashe.
 
Hivi ujinga na upumbavu, hata km unafanywa na chama chetu tuukubali tu kwa sababu ni chama chetu? Huu si uzalendo!!!
 
Hivi CCM wamefirisika ki mawazo kiasi hiki cha kumchukia mtu tu kwa sababu ni
1. Msema kweli ?
2. Ni msomali ?
3. Hajaukandamiza upinzani?!

Mnasahau hata Kinana ni msomali tena Cornell wa jeshi na sasa Secretary General wa CCM .
 
ULAANIWE , ULAANIWE ULAANIWE

Wewe ndiye unastahili kulaani sababu uko kimaslahi, watanzania walio wengi wanahitaji wabunge kwenda kuwasemea na kuwatetea ili nao wapate manufaa. Ilani ya CCM 2015-2020 ndiyo dira ya wabunge wa CCM na kazi yao ni kuibada serikali kuhakikisha Ilani inatekelezwa. Sasa huyo Bashe yeye anatumia Ilani ya chama gani????
Huyo ni msaliti mkubwa, afukuzwe chama maana nia yake ni kuvuruga kabisa CCM kama anavyotumiwa. HAIKUBALIKI NI MUHIMU ARUDISHE KADI
 
Ukweli ni jambo zuri sana kulisema, lakini uzalendo ni kitu bora zaidi kuliko kitu chochote kile.

Hussein Bashe wewe uko ndani ya CCM na ajabu wewe unaongoza kwa kuiponda CCM kuliko hata ambavyo unaviponda vyama vya upinzani. Katika siasa tabia kama hii haikubaliki hata kidogo.

Wana CCM tumekuwa tukikufuatilia kwa karibu sana, na matamko yako, yanaonesha wazi kabisa wewe siyo mzalendo kwa chama chako kilichokulea mpaka kukufikisha hapo ulipofika.

Inawezekana madai yako yakawa na ukweli ama la; lakini namna unavyoyawasilisha na mahali unapoyawasilisha siyo sahihi hata kidogo. Sidhani kama Mwenyekiti ataendelea kukuvumilia. Mimi nikiwa kama mwanachama wa CCM nimekerwa sana na matamshi yako unayoyatoa bungeni. Acha kutafuta cheap publicity!

Bashe wewe ni msaliti, tena inaonekana unatumiwa na CHADEMA sababu ulikuwa swahiba wa Lowassa. You are a traitor! You are a mole and you have to be removed!

Nakushauri Mwenyekiti wangu mpendwa na Rais wetu, ndugu John Pombe Magufuli, muondoe haraka sana huyu kijana ndani ya chama chetu sababu sasa ameshaota MAPEMBE. Bashe ni hatari sana kwa mustakabali wa chama chetu (CCM).

Hakuna chama chochote kile cha siasa hapa Tanzania ambacho kingemvumilia mwanachama kama BASHE! Mifano ipo mingi sana.

Mbaya zaidi anayoyaongea Bashe bungeni hayana faida yoyote ile kwa wananchi wa jimbo lake! Kazi yako Bashe ni kuwawakilisha wapiga kura wa NZEGA na siyo kupigana na CCM na serikali yake!

Mheshimiwa Rais; naomba uunde kamati maalumu ndani ya CCM kwa ajili ya kumchunguza huyu bwana mdogo. Anakoelekea siko kabisa na hatufai tena ndani ya chama chetu.

Mimi nina uhakika wa 90% hata kama tukimfukuza uanachama huyu msaliti BASHE, jimbo la NZEGA bado tutalichukua. Wakati ni sasa!

By Son of Gamba.
Mwenyekiti wako alishakataa ushauri wa kwenye mamitandao.
 
Kumbe uzalendo huwa si kwa nchi ni kwa ajili ya chama! Hahahahaa, sina mbavu

Mkuu, sisi binadamu tuna uwezo wa namna mbili katika kufikiri yaani kufikiri kwa kina (capacity thinking) au uwezo wa kufikiri (ability to think) na kufikiri kwa makini (critical thinking).

Juzi jumapili nilisikiliza kwa makini mahubiri ya askofu Gwajima na pamoja na mahubiri yake yalojaa siasa, pia alizungumza jambo moja la maana sana.

Askofu Gwajima alisema kwamba sisi waafrika tumefungwa uwezo wetu wa kufikiri na kwamba hata akiwepo mtu ambae anaweza kufikiri kwa kina, basi hata wazungu wapo tayati kumchukua ili akaishi nao halafu wafaidike na uwezo wake huyo mtu.

Sasa kufikiri kwa makini mara nyingi kunaenda na uwezo wa kuchambua vigezo voye na kuvipa umuhimu kabla ya kutoa maamuzi au "judgement".

Na ndiyo maana hata ukiwa na nafasi kama Hussein Bashe kwamba wewe ni mbunge, basi ukikosa uwezo huu wa kutambua kwamba kile ukitamkacho mbele ya hadhira bila kujali ni hadhira ya namna gani kina athari gani, basi wewe hufai kuwa kwenye nafasi ulo nayo.
 
Hata kipindi cha kikwete ccm ili kuwa vipandevipande hata kipindi cha kikwete watu walitekwa. Lkn kikwete alisema nchi ameiacha salama na watanzania tulimpongeza kwa kujiridhisha kweli ameiacha salama...tz ina watu wenye matatizo wengi mno sio hayo ya kulialia bunge kwa vitu ambavyo ni vya kudhani kwasababu hawawezi kutoa ushahidi kwa kushikika.....UZANDIKI na HUJUMA ni adui mkubwa sana wa taifa lolote.
 
Ujinga ni kuweka maslahi ya chama mbele badala ya mustakabali wa taifa mbele elimu inayotolewa Tanzania haijawahi kumkomboa mtu kifikra ndo mana mtu kua unapinga CCM ukiwa ndani ya CCM unaonekana either msaliti au mpinzani...
 
Kwahiyo mkuu kwako bora uzalendo wa chama kuliko nchi?
 
Hujui tu, akina Bashe waliokimya ni wengi sana. Ndani ya Chama wengi wamenuuna.
 
***
MTU ANAPOTOA VUMBI CHUMBANI MWAKE ANAFANYA JEMA AU OVU...!
•RAIS KILA SIKU ANAPIGA KELELE KWA KUTAKA NA KUITAFUTA CCM ILIYO SAFI / KWA UJINGA UNAONA BASHE ANAFANYA BAYA..../
Soma post yangu uelewe nilichoandika, acha kukurupuka. Siyo vibaya kukikosoa chama, lakini kuna vikao maalumu vya kufanya hivyo siyo kuropoka bungeni kama Bashe kwa kutafuta sifa kutoka kwa wapinzani.
 
Nchi yetu imeelemewa sana na mzigo wa watu wajinga kweli. Kwanini watu hawataki ukweli usemwe hadharani kama kweli wana nia ya dhati kuifikisha nchi hii mahali walipoahidi?
Yaani tuwe wazalendo kwenye mambo yanayohatarisha umoja wetu uliojengwa kwa gharama kubwa sana kwasababu ya mapenzi ya vyama?
Hivi nyinyi ccm mmerogwa na nani? Sio nyie kwenye ahadi za chama chenu mnatakiwa kusema ukweli daima unafiki uwe mwiki kwenu?
Kama mnawataka watu wasiseme hadharani kwa maslahi ya chama, je mtapata wapi ujasiri wa juwaomba wananchi wa kawaida kufichua maovu wakati hamuamini juu ya ukweli ila unafiki.
Bashe atishiwe maisha ila mumtake aseme hajatishiwa?
 
Back
Top Bottom