SIKU YA UKIMWI DUNIANI (Tunakumbushana)

Noor

Senior Member
Feb 5, 2012
146
225
Ndugu zangu,

Nimeona si vibaya kuwakumbusha tunapoenda kwenye siku ya Ukimwi duniani hapo kesho tujaribu kuangalia kwa mapana baadhi ya mambo na kujitafakari kwa mapana kama tuko kwenye njia salama ama la.

Nafarijika kusikia na kutambua kwetu kuwa janga la UKIMWI linahitaji elimu kwa jamii yote ili kufanikisha mapambano dhidi yake. Na nafarijika pia kusikia aghalabu siku hizi vitendo vya unyanyapaa vinapungua kwa kiasi kikubwa. Ndugu zetu walioathirika wasitengwe au kunyanyaswa.

Ningependa sote tujiulize tena maswali magumu bila aibu na tuchukue hatua bila ajizi. Je, tangu mwaka huu uanze tumeshiriki kiasi gani kuzuia kuenea kwa UKIMWI? Je, wewe umekwisharekebisha mwenendo wako na kuacha tabia zinazochangia kuenea kwa UKIMWI? Je, kwenye mazingira unayoishi (sehemu ya kazi au vyuoni) pamekuwa na mwamko mpya wa kupambana na UKIMWI? Wewe unashiriki vipi?

Kila mmoja atafakari kwa dhati moyoni mwake na achukue hatua. Tusaidiane kwa kila hali kuweza kujikinga, na kwa walioathirika tayari kuwatendea haki bila ubaguzi. Kila sehemu iwe na utaratibu wa kukumbushana mara kwa mara juu ya UKIMWI, na mkakati mahususi wa kuzuia kuenea kwa virusi vya UKIMWI.
Nawatakia afya njema na mchango mwema kwenye jamii yetu inayotuzunguka ili tuutokomeze UKIMWI na kuifanya Tanzania na Dunia nzima kwa ujumla kua ni sehemu yenye mafanikio yanayotokana na afya njema.
Mungu Ibariki Tanzania
Mungu Ibariki Afrika.
abdulnoor3@gmail.com
 
Prisoner 46664

JF-Expert Member
Dec 18, 2010
1,945
1,225
Baada ya kufuatilia kwa umakini maendeleo ya afya ya Magic Johnson kwa miaka 20 sasa, na kugundua kuwa mtu anaweza kupata watoto wasio na VVU wengi atakavyo..nimefikia hitimisho kuwa ukimwi si tishio tena
 
Zamaulid

JF-Expert Member
May 25, 2009
17,769
2,000
Baada ya kufuatilia kwa umakini maendeleo ya afya ya Magic Johnson kwa miaka 20 sasa, na kugundua kuwa mtu anaweza kupata watoto wasio na VVU wengi atakavyo..nimefikia hitimisho kuwa ukimwi si tishio tena
mkuu ina mgharimu kiasi gani kumaintain hiyo afya,je mtanzania wa kawaida atamudu!!!nadhani hii kitu bado ni tishio!!
 
PhD

JF-Expert Member
Jul 15, 2009
3,961
2,000
Baada ya kufuatilia kwa umakini maendeleo ya afya ya Magic Johnson kwa miaka 20 sasa, na kugundua kuwa mtu anaweza kupata watoto wasio na VVU wengi atakavyo..nimefikia hitimisho kuwa ukimwi si tishio tena
HIV / AIDS ni biashara na ajira sio janga inakuzwa tu, magonjwa yanayowamaliza watanzania kwa sasa ni malaria kwa watoto , afya ya mama wajawazito wakati wa kujifungua na magonjwa ya kansa yanaua sana kwa sasa. HIV inaua lakini sio kama hayo niliotaja ukiongeza na kisukari na presha.
 
Tikerra

JF-Expert Member
Sep 3, 2008
1,704
0
Ndugu zangu,

Nimeona si vibaya kuwakumbusha tunapoenda kwenye siku ya Ukimwi duniani hapo kesho tujaribu kuangalia kwa mapana baadhi ya mambo na kujitafakari kwa mapana kama tuko kwenye njia salama ama la.

Nafarijika kusikia na kutambua kwetu kuwa janga la UKIMWI linahitaji elimu kwa jamii yote ili kufanikisha mapambano dhidi yake. Na nafarijika pia kusikia aghalabu siku hizi vitendo vya unyanyapaa vinapungua kwa kiasi kikubwa. Ndugu zetu walioathirika wasitengwe au kunyanyaswa.

Ningependa sote tujiulize tena maswali magumu bila aibu na tuchukue hatua bila ajizi. Je, tangu mwaka huu uanze tumeshiriki kiasi gani kuzuia kuenea kwa UKIMWI? Je, wewe umekwisharekebisha mwenendo wako na kuacha tabia zinazochangia kuenea kwa UKIMWI? Je, kwenye mazingira unayoishi (sehemu ya kazi au vyuoni) pamekuwa na mwamko mpya wa kupambana na UKIMWI? Wewe unashiriki vipi?

Kila mmoja atafakari kwa dhati moyoni mwake na achukue hatua. Tusaidiane kwa kila hali kuweza kujikinga, na kwa walioathirika tayari kuwatendea haki bila ubaguzi. Kila sehemu iwe na utaratibu wa kukumbushana mara kwa mara juu ya UKIMWI, na mkakati mahususi wa kuzuia kuenea kwa virusi vya UKIMWI.
Nawatakia afya njema na mchango mwema kwenye jamii yetu inayotuzunguka ili tuutokomeze UKIMWI na kuifanya Tanzania na Dunia nzima kwa ujumla kua ni sehemu yenye mafanikio yanayotokana na afya njema.
Mungu Ibariki Tanzania
Mungu Ibariki Afrika.
abdulnoor3@gmail.com
Siku ya mikono,vidole,viwiko,nywele,macho nk.Tusubiri siku ya U-Cameron(Ushoga) duniani.Hawa jamaa wanatuona sisi mataahira sana,na hatujui kinachoendelea.
 
shumbe

Member
Nov 13, 2012
28
20
siku hii ni muhimu sana kwetu kwani na hakika kuwa kilamoja wetu ameisha poteza ndugu, rafiki na jamaa kwa janga hili. HIvyo ni vyema tuwakumbuke ndugu zetu na kujifunza kutoka kwao.

Kinga ni bora kiliko tiba.
Watanzania wenzangu tuwena mazoea ya kuwa tunatumia kondom kwende tendo la ndoa kwani tumeshindwa kuwa waaminifu:thumbup:
 
ngoshwe

JF-Expert Member
Mar 31, 2009
4,133
1,250
Matangazo ya moja kwa moja (LIVE) ya siku ya Ukimwi Duniani yanayoazimishwa tokea Mkoani Lindi Uwanja wa ILILU kupitia TBC - 1 yameanza kwa kupooza kinoma, watangazaji wa TBC inaonekana hawakujipanga kabisa.

BI Mwanahawa Lugongo ambae anaendesha matangazo hayo ni kama amekurupushwa tu...matukio yanaenda kiholela tu.. sauti zina katika katika hovyoo.. mtangazanji ni kama vile hana ratiba, Mkuu wa Kaya anazunguka zunguka tu vibadani bila maelezo yoyote kuhusu mule apitapo..Watanzania wangependa kujua anazungukia nini..hakuna maelezo....maandalizi duni kabisa.

Kwengine matangazo yanaendelea, kwingine waigizaji (Comedians) wanaburudisha watu, sauti zinaingiliana bila msingi nk..

Aibu MKURUGENZI CLEMENT MSHANA, KAZI IMEKUSHINDA.....
 
CHUAKACHARA

JF-Expert Member
Jun 3, 2011
12,369
2,000
Matanagazo ya siku ya Ukimwi Duniani yanayoazimishwa tokea Mkoani Lindi kupitia TBC - 1 yamepooza kinoma, watangazaji wa TBC inaonekana hawakujipanga kabisa. BI Mwanahawa Lugongo ambae anaendesha matangazo hayo ni kama amekurupushwa...matukio yanaenda kiholela tu.. sauti zinakatika katika hovyoo..

Aibu MKURUGEZNI CLEMENT MSHANA
.
Ukurugenzi gani huyu ataufanya wa maana. Kujikomba kwa CCM.
 
Bilionea Asigwa

JF-Expert Member
Sep 21, 2011
16,358
2,000
Kituo cha taifa cha TELEVISHENI ni kama hakipo japo naamini wanaongoza kwa uwa na bajeti kubwa kuliko vituo vingine vya habari..........
 
TandaleOne

JF-Expert Member
Sep 4, 2010
1,622
1,250
Katika Maazimisho ya siku ya ukimwi ambayo yanafanyika kitaifa Mkoani Lindi, wanaCCM wa Mkoa huo wamepamba maazimisho hayo kwa shughuli mbalimbali za Chama walizoziandaa katika kufanya Maazimisho hayo kufana, walijigawa katika Makundi kulingana na Jumuiya za Chama hicho ambapo jumuiya ya vijana walifanya maonyesho ya gwaride la chipukizi wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi. Pia jumuiya zingine walijipanga vema katika maandamano ya kumpokea na kumsindikiza Mheshimiwa Rais kitendo ambacho Mheshimiwa Rais kilimvutia na kukisifia, lakini pia vikundi vya sanaa na uhamasishaji.

Pia katika matukio mengine vijana wa CUF ambao walijipanga kubeba mabango yenye ujumbe wa kukashfu viongozi wa CCM wa mkoa huo walishindwa kufanikiwa azma yao hiyo baada ya kujikuta kuwa miongoni mwao wanawaunga Mkono viongozi wa CCM na hivyo kufanya mabango hayo kutotumika.
 
Greenwhich

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
1,337
1,195
Ni sahihi kabisa.Hiyo ni sherehe ya wana CCM.Wanafurahia mafanikio.Kama wanavyofunika kwenye misiba ya watu maarufu.
 
zumbemkuu

JF-Expert Member
Sep 11, 2010
10,066
2,000
Katika Maazimisho ya siku ya ukimwi ambayo yanafanyika kitaifa Mkoani Lindi, wanaCCM wa Mkoa huo wamepamba maazimisho hayo kwa shughuli mbalimbali za Chama walizoziandaa katika kufanya Maazimisho hayo kufana, walijigawa katika Makundi kulingana na Jumuiya za Chama hicho ambapo jumuiya ya vijana walifanya maonyesho ya gwaride la chipukizi wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi. Pia jumuiya zingine walijipanga vema katika maandamano ya kumpokea na kumsindikiza Mheshimiwa Rais kitendo ambacho Mheshimiwa Rais kilimvutia na kukisifia, lakini pia vikundi vya sanaa na uhamasishaji.

Pia katika matukio mengine vijana wa CUF ambao walijipanga kubeba mabango yenye ujumbe wa kukashfu viongozi wa CCM wa mkoa huo walishindwa kufanikiwa azma yao hiyo baada ya kujikuta kuwa miongoni mwao wanawaunga Mkono viongozi wa CCM na hivyo kufanya mabango hayo kutotumika.
CCM wengi ni waathirika...
 
shumbe

Member
Nov 13, 2012
28
20
@ Ngoshwe Hivi hadi leo haujajua kuwa WaTZ tuna tatizo la uvivu na kutokujiandaa mapema kabla ya siku ya tukio.
Hiyo ni aibu yetu sote hapo hao jamaa wanafikiria ten percent zao tu hapo akili haifanyi kazi.
 
sony wega

JF-Expert Member
Jun 18, 2012
234
0
Huyo mtangazaji bi mwadawa ni mwenyekiti wa ccm huku mtaani kwetu mbagala kwa mponda hamna kitu hapo bara bara za mtaa zinamshinda na maji vile vie wanauza maeneo ya shule na kujisahau kuwa ile shule ya mianzini inatakiwa iwe na darasa la tatu darasa halijajengwa na hela wamekula wakishikiana na diwani wake alikuwa na nyuma kimeo na hana gari ila baada ya kukwaa uenyekiti basi mama ana rav 4 na nyumba imekarabatiwa na vile vile akae akijua kuwa 2014 harudi kwani yule mjumbe wake wa ccm mchongea aliemfukuza keshajivua gamba na yuko cdm na harakati zimeeanza na mwenyekiti wetu ni lawrence mvungi kupitia cdm kata ya mponda charambe mbagala
 
kibogo

JF-Expert Member
Apr 1, 2012
9,722
2,000
Katika Maazimisho ya siku ya ukimwi ambayo yanafanyika kitaifa Mkoani Lindi, wanaCCM wa Mkoa huo wamepamba maazimisho hayo kwa shughuli mbalimbali za Chama walizoziandaa katika kufanya Maazimisho hayo kufana, walijigawa katika Makundi kulingana na Jumuiya za Chama hicho ambapo jumuiya ya vijana walifanya maonyesho ya gwaride la chipukizi wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi. Pia jumuiya zingine walijipanga vema katika maandamano ya kumpokea na kumsindikiza Mheshimiwa Rais kitendo ambacho Mheshimiwa Rais kilimvutia na kukisifia, lakini pia vikundi vya sanaa na uhamasishaji.

Pia katika matukio mengine vijana wa CUF ambao walijipanga kubeba mabango yenye ujumbe wa kukashfu viongozi wa CCM wa mkoa huo walishindwa kufanikiwa azma yao hiyo baada ya kujikuta kuwa miongoni mwao wanawaunga Mkono viongozi wa CCM na hivyo kufanya mabango hayo kutotumika.
Hapo ndipo ninapokuja kuishangaa hii nchi, Siku ya Ukimwi duniani haiitaji vyama kujionyesha ndani ya sherehe hiyo unapofanya hivyo inanyima uhuru wa watu wengine kujitokeza kuadhimisha sherehe hiyo, kilichotakiwa hapo ni watu wote kuvaa nguo zinazoendana na tukio lenyewe unapovaa nguo ya kijani, nyeusi na njano haileti maana zaidi ya kuleta maudhi kwa wasioipenda CCM. na nafikiri hicho kimechangia kudhorota kwa sherehe hiyo
 
Top Bottom