Siku ya nne bila maji Kibamba, Dar (Juni 9, 2019)

Ndugu zangu wanaJF nawasalimia.

Ninasikitika kusema kuwa leo Jumapili, Juni 09, 2019 ni siku ya nne maji hayatoki maeneo yote ya Kibamba.

Na cha kusikitisha zaidi ni kuwa mamlaka husika zipo kimya na hakuna taarifa zozote kuhusiana na tatizo hili.

Naomba tueleweshwe nini hatma ya tatizo hili toka kwa mamlaka husika..
Hongereni sana.Ila chimbeni visima kama wenzeni wa kitunda kivule mbagala kigamboni,Chanika na gongo la mboto maana hao sijahi sikia wakilia maji
 
Bora yenu hata mnahayo mabomba wengine kwetu hatuyajui kabisa siku yakifika itakuwa sherehe lkn nanyi wadau mnaolalamika maji inatakiwa mjenge mazoea ya kuweka akiba kubwa ya maji tafuteni sm tank kiangazi hiki kimeanza muda mwingine inaweza tokea wiki nzima au mbili kabisa maji yasitoke hawa wahusika kukiwa na mvua maji yanatoka saa 24 subiri kiangazi sasa
 
Hongereni sana.Ila chimbeni visima kama wenzeni wa kitunda kivule mbagala kigamboni,Chanika na gongo la mboto maana hao sijahi sikia wakilia maji
Nashukuru kaka kwa ushauri mzuri. Lakini siku zote huwa kuna permanent solution na immediate solution. Sisi tunaulizia immediate solution. Ni sawa na kukuta mtu amegongwa na gari kisha unaanza kuulizia chanzo cha ajali ili ajali hiyo isitokee tena wakati majeruhi bado kalala chini anavuja damu.. Ila ushauri wako ni nzuri ntaufanyia kazi..
 
Habarini wanajamvi.
Wahusika wa usambazaji maji, DAWASCO kuna tatizo gani?. Mbona maji Msewe hayatoki wiki zinakatika now. Maisha yamekuwa magumu kweli embu tufikirieni kidogo.
 
Back
Top Bottom