Siku ya nne bila maji Kibamba, Dar (Juni 9, 2019)

MR.NOMA

JF-Expert Member
Feb 1, 2014
338
502
Wakuu Kwema!!?

Pamoja na Tangazo linalosambaa la DAWASCO kuwa kulikuwa na itilaf kwenye mitambo ya maji huko RUVU, Sasa hii ni Tanzania pekee wananchi wamekosa huduma ya maji kwa siku nne mfululizo, huku mtaani wamama wanahaha kwelikweli, wengine wamelazimika kuuziwa maji yasiyo salama ya visima.

Ila Watendaji wakuu wa DAWASCo wapo tu kwenye nafsi zao mpaka Sasa, Waziri yupo tu,Naibu wake nk.

Hii ni Tanzania pekee,naamini ingekuwa kwingine wangesha jitumbua wenyewe.Kama Kiongozi unachukua karibu wiki nzima kutatua Changamoto ili wananchi wapate maji haraka kwa kuwa ni hitaji la muhimu.

======

UPDATES;10 Juni 2019

Maji yameshaanza kurejea.
IMG_20190610_212423_536.jpg
 
Hii ni fursa iliyo uchi kwa vijana sasa hasa graduate ambao ndio wamejaa kitaa, kama mkokoteni wako kama huna azima, jaza madumu ata matano kwenye visima yanakopatikana, ingia nayo kitaa kwa hali ya maji ilivyo ngumu utayauza buku buku kwa kila dumu kirahisi kabisa, ukianza saa 12 asubui kuyasambaza kwa wateja mpk jion saa kumi na mbili utakuwa umetengeneza mkwanja mrefu tu, ukifanya hvyo mpk yatakaporudi utakuwa umetengeneza mtaji wa kutosha kuanza kabiashara kako ka kishkaji kakuanzia maisha. Kamateni fursa vijana,.
 
Kumbuka utayachota kwa 250 kwa kila dumu kwa sasa, ukiuza buku faida mia saba na hamsini, kama unadumu sita tayari kwa trip moja una 4500,ukienda trip 20*4500=90,000.acha kushangaa hyo ni elfu tisini kwa siku.
 
Trip 20??

Duh!
Yaa mbona ni easily tu mkuu, kumbuka ukishaleta trip moja, orders za akina mama kidawa ndio zinaanza, mara huku niletee dumu mbili kaka, mama asha nae hku chukua kabisa hela yko nataka dum tatu, so kwa mwendo huo trip 20 ni fasta tu
 
Pole sana Mr Noma hiyo ni bonge ya noma....hizo ndio characteristics za ulimwengu wa dunia ya tatu.....usitegemee sana serekali chimba kisima chako....
 
Aisee mpaka Mbezi yamekata. Nimebakiza robo ndoo na huku kwetu hawa jamaa wa mikokoteni sijawahi hata kuwaona. Hili ni janga
 
Yaa mbona ni easily tu mkuu, kumbuka ukishaleta trip moja, orders za akina mama kidawa ndio zinaanza, mara huku niletee dumu mbili kaka, mama asha nae hku chukua kabisa hela yko nataka dum tatu, so kwa mwendo huo trip 20 ni fasta tu

Ni kweli mkuu ila ni ngumu sana labda ingekuwa kwa gari ila sio mkokoteni

Hizo trip 20 go and return ni mara 40 ujue
 
Ni kweli mkuu ila ni ngumu sana labda ingekuwa kwa gari ila sio mkokoteni

Hizo trip 20 go and return ni mara 40 ujue
Sure bt namaanisha ukienda then ukirudi hyo ni trp moja, that is what i mean, sijui nimepatia!!!! Maana hii elimu yangu ya darasa la saba inafanya hii lugha inichukie.
 
Sure bt namaanisha ukienda then ukirudi hyo ni trp moja, that is what i mean, sijui nimepatia!!!! Maana hii elimu yangu ya darasa la saba inafanya hii lugha inichukie.

Hahahahh ila anakuwa ameenda na kurudi mara nyingi

Lakini itakuwa ni rahisi kama umeiandika kiurahisi hivyo
 
Wakuu Kwema!!? pamoja na Tangazo linalosambaa la DAWASCO kuwa kulikuwa na itilaf kwenye mitambo ya maji huko RUVU, Sasa hii ni Tanzania pekee wananchi wamekosa huduma ya maji kwa siku nne mfululizo, huku mtaani wamama wanahaha kwelikweli, wengine wamelazimika kuuziwa maji yasiyo salama ya visima, ila Watendaji wakuu wa DAWASCo wapo tu kwenye nafsi zao mpaka Sasa, Waziri yupo tu,Naibu wake nk.Hii ni Tanzania pekee,naamini ingekuwa kwingine wangesha jitumbua wenyewe.Kama Kiongozi unachukua karibu wiki nzima kutatua Changamoto ili wananchi wapate maji haraka kwa kuwa ni hitaji la muhimu.

Samahani mkuu John Mnyika ndio mbunge wenu?
 
Back
Top Bottom