Siku ya Mtoto wa Afrika Viwanja vya JKMYP na nyimbo za Ali Kiba,Diamond na Man Fongo

mwanamwana

JF-Expert Member
Aug 1, 2011
1,229
4,554
Leo nimebahatika kuhudhuria maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika 2016, viwanja vya Jakaya Mrisho Kikwete Youth Park pale mnazi mmoja.

Pamoja na watoto kuonesha vipaji vyao mbalimbali kama kucheza ngoma, Sarakasi nk pia kilichovutia wengi wetu ni burudani kabambe waliyoshusha hawa vijana wetu wa taifa la kesho.

Ilikuwa hivi, Dj alikuwa akipiga nyimbo tofauti tofauti na watoto walipoingia kati Dj alipiga nyimbo nne, moja Ali Kiba, Harmonize,Diamond na Man Fongo.

Nyimbo ya Ali Kiba ukweli haikuwavutia kabisa vijana wetu,walikuwa wanacheza ilimradi wimbo uishe uingie mwingine, ulipopigwa wimbo wa Harmonize ''Bado'' shangwe ikaamka watoto wakachangamka, ukafuata wa Diamond Shangwe ikazidi mara dufu watoto wakicheza kwa maringo maringo kama achezavyo Diamond.

Kasheshe ikaja baada ya kupiga wimbo wa Man Fongo, siujui jina ila anaimba ( Begi kama hili,huwezi nunua....Huna, Chupi kama hii huwezi nunua... hunaa. ) Ebanaeeee vumbi lililotimka pale sijapata kuona, hata watoto walokuwa kwenye jukwaa wakashuka kuja kucheza SINGELI.

Maana ya BANDIKO langu ni kuwa,

- Kiba bado ana safari ndefu, kiukweli hakubaliki kama mashabiki wake hewa wanavyotaka kuaminisha.
- Diamond bado ni kipenzi cha watu, wawe wazee,vijana na watoto. Bado ataendelea kusumbua mpaka akija mshindani wa kweli

- Muziki wa SINGELI sasa umekua, unapendwa, unachzwa sana na vijana na watoto ambao kikweli ndio wanatoa sapoti kubwa kwa wanamuziki. Bravo Man Fongo, nilisubiria goma lako la Hainaga ushemeji, Tunakulagaa ila bahati mbaya mpaka naondoka saa 11 halikuchezwa.

DSC08839.JPG

Watoto wakicheza wimbo wa Man Fongo
 
Tumekupata mkuu, ila nadhani issue ni kwamba hiyo nyimbo ya Alikiba inachezeka?? Maana sitegemei ata km ingekuwa nyimbo ya Diamond Lala salama eti kisa ni Diamond watoto wangecheza, so issue nahisi nyimbo ilikuwa haichezeki

mfano nyimbo nzuri km ya rich mavoko imebaki story, au basi nenda ya mo music japokuwa ilikuwa ni nyimbo ya taifa ila huwez kuiskia ikipigwa club km dj hataki wateja wake wakae, so kila nyimbo zina mahadhi yake na sio zote za kurusha mabega, zingine unafurahia tu rohoni huku unatikisa tu miguu na kichwa
Ni mtazamo wangu tu.
 
True hata mimi wakati nasikilza clouds fm watoto wengi wanaomba nyimbo za domo.
Cijajua reason behind
 
Back
Top Bottom