siku ya majonzi

19don

JF-Expert Member
May 13, 2011
672
205
ilikuwa siku kama ya leo nikiwa njiani kutokea mjini , nikapokea simu kutoka nyumbani
home; dady kuna majambazi wanapiga risasi huku tunazisikia
mimi; ingieni ndani upesi hamuwezi kujua wataelekea wapi
baada ya dk 10
home; sio majambazi ni mabomu dady
mimi; tokeni ndani tafuteni mahari penye kama shimo jificheni msikae ndani

mara; samahani simu unayo piga kwa sasa haipatikani
ooh mungu wangu inamaana familia yangu yote imeteketea na hawa wanajeshi wamefunga njia itakuwaje sasa, anga linazidi kubadilika rangi , na idadi ya watu wanao kimbia wanazi kuongeza

hii ni siku ambayo mume alimsahau mume , watoto walilala uwanja wa taifa bil blanket wa godoro na msaada walio pewa ni maji na biskuti

ni siku ambayo wagonjwa na wazee walirudi katika ujana na kukimbia hadi sehemu mbalimbali za dar bila kupumzika

JE NDUGU ZANGU WA GONGO LA MBOTO MMEISAHAU SIKU HII TULIWAPOTEZA BAADHI YA NDUGU ZETU ?
JE MMESAHAU TULIOUNGULIWA NYUMBA

RIP NDUGU WOTE WALIO POTEZA MAISHA SIKU YA LEO
NI MWAKA MMOJA KAMILI TOKA SIKU ILE YA MAJONZI 26/FEB/2011
_51312030_cherehani.jpg
 
19don,
Umenifanya nianze kulia kwa kuimbuka siku hii, si kwamba nilifiwa na mmoja wa familia yangu la hasha bali tukio lenyewe lilivyokuwa pamoja na kupotelewa na watz wenzangu na kusababisha watoto kuwa yatima, kusababisha vilema vya maisha kwa watz, uharibifu wa mali nk. nk kwa ajili ya uzembe wa jeshi letu. nimeshindwa kuendelea.
 
Sitokuja kusahau siku hiyo katika maisha yangu.Niligongwa na gari na kuvunjika mguu.Nimekaa mwaka bila kwenda kazini.Niliumia saaana.Nashukuru Mungu kiasi naendelea vizuri.Cha kushangaza ni serikali kutotulipa FIDIA mpaka leo.Watu tulioumia serikali imetususa.PESA iliyochangwa na taasisi mbalimbali imeenda wapi?
 
Aisee hiyo siku sitaki kuikukmbuka ni uzembe wa rais kikwete na wala si jeshi watanzania wenzangu, alipewa barua asign ya kuhamisha zile silaha lakini hakuweza kusign mpaka watanzania wakapoteza maisha, omg !!!! laana na ziwakumbe sana sana. pinda juzi kaua watu wengi sana kwa domo lake omg !!! laana ziwakute
 
Mbona hujamalizia kama familia yako uliikuta kwenye hali nzuri?
 
Fanya editing ya heading so that it can reflect what you want to convene..
 
Ni miongoni mwa matukio yanayopoteza maisha ya watz wengi na bado watu wanafanya masihara.
Ukiambiwa serikali inauwa watu unaambiwa ufute kauli, wallahi sifuti, wauwaji hawa. Yote ili mdudu dowans apite. Laana yao milele, na wataweweseka hadi makaburini.

Vp familia yako uliikuta?
 
ilikuwa siku kama ya leo nikiwa njiani kutokea mjini , nikapokea simu kutoka nyumbani
home; dady kuna majambazi wanapiga risasi huku tunazisikia
mimi; ingieni ndani upesi hamuwezi kujua wataelekea wapi
baada ya dk 10
home; sio majambazi ni mabomu dady
mimi; tokeni ndani tafuteni mahari penye kama shimo jificheni msikae ndani

mara; samahani simu unayo piga kwa sasa haipatikani
ooh mungu wangu inamaana familia yangu yote imeteketea na hawa wanajeshi wamefunga njia itakuwaje sasa, anga linazidi kubadilika rangi , na idadi ya watu wanao kimbia wanazi kuongeza

hii ni siku ambayo mume alimsahau mume , watoto walilala uwanja wa taifa bil blanket wa godoro na msaada walio pewa ni maji na biskuti

ni siku ambayo wagonjwa na wazee walirudi katika ujana na kukimbia hadi sehemu mbalimbali za dar bila kupumzika

JE NDUGU ZANGU WA GONGO LA MBOTO MMEISAHAU SIKU HII TULIWAPOTEZA BAADHI YA NDUGU ZETU ?
JE MMESAHAU TULIOUNGULIWA NYUMBA

RIP NDUGU WOTE WALIO POTEZA MAISHA SIKU YA LEO
NI MWAKA MMOJA KAMILI TOKA SIKU ILE YA MAJONZI 26/FEB/2011
_51312030_cherehani.jpg

INAUMA NA INASIKITISHA SANA!
Halafu Serikali hii ya ajabu isiyojali watu, JK kaenda kutembelea anacheka, akaenda hospitali anaongea na walioumia na kupoteza ndugu akicheka!
Pinda anayo makazi yake huko G'mboto, na majirani zake wengi walijeruhiwa au kupoteza ndugu, lakina hatutaamini kuwa hadi leo hawajalipwa fidia, ana fedha nyingine zimeliwa na maafisa wa Serikali? Je Ofisi ya Pinda idara ya MAAFA sio yenye kamati yake inayosimamia maafa? Amefanya nini?

Halafu, Serikali pia ikatoa kauli kuwa, "Wananchi ndio walivamia, na kujenga karibu na kambi maana kambi ilianza zamani kabla watu hawajajenga huko" Je huu ni utu na kuna ukweli hapo? Mbona nyumba nyingi za raia kadhaa wa Segerea, Kipunguni, Tabata Changombe, Mbagala na maeneo mengi yalipigwa na mabomu, je nao walivamia au kujenga karibu na kambi ya Gongolamboto? Hakuna ukweli na hakuna majibu yenye utu hadi leo! Visingizio tuuu!

KAULI YAKINIFU: TUNAKUMBUSHA KUWA KAMBI ZOTE ZA JESHI NA MAGHALA YA SILAHA YAHAMISHIWE MBUGANI, AU NYIKANI, KATIKATI YA NCHI AMBAKO TUNAYO HAZINA KUBWA YA ARDHI, HAINA WATU, NA RAIA HAWAWEZI KUFIKA AU KUATHIRIKA. KAMA HILO LINAWASHINDA SERIKALI, NA HALIWEZI KUFANYA, HII INAZIDI KUDHIHIRISHA JINSI VIONGOZI WANAVYOPUUZA KILIO CHA WANANCHI HADI MAAFA YAWASHTUE, BASI TUNAWASHAURI, WAJENGE NA WAYAFICHE KATIKA MAGHALA MAHANDAKI KAMA KILOMETA 1 AU 2 CHINI YA ARDHI, AU CHINI YA MILIMA! WAMEFANIKIWA HIVYO NDUGU ZETU WAKENYA! NASI PIA TUNASHAURI SERIKALI HII IJIFUNZE KUTENDA NA WAEPUKE KUEGEMEA KTK VISINGIZIO! "KIDONDA KITIBU KINGALI KIPYA"
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom