Siku ya kweli aliyokufa Mwl J K Nyerere

Siku ya kweli aliyokufa Mwl J K Nyerere

Ukweli hauwezi funikwa siku zote. Ni kama kuuzuia moshi kwa kawa.

Kama vile kuvuja kwa taarifa za mipango na utekelezaji wa kumwua Nyerere kulivyokuwa, kisha kuibukia 2012 kwa uwazi zaidi. Ndivyo tarehe rasmi ya kufariki inapojulikana.

Nyerere alifariki tarehe 7 Oktoba 1999.

Tarehe nyingine ni danganya toto. Ukweli unasema, huwezi kuwadanganya watu wote kwa nyakati zote. Ndicho serikali iliyoongozwa na B W Mkapa ilichofanya.

Leta chanzo cha hiyo habari mkuu kama sio porojo tu .
 
Aulizwe ben ndo mhusika mkuu,lengo lilikuwa kufanikisha uchimbaji,uwekezaji na kugawana machimbo ya madini kwa wageni ambapo mwalimu alikuwa kama kikwazo kwani alisimamia msimamo wake kuwa muda muafaka haujafika na hayaozi
 
Ngoja tumulize kagasheki ndo alikuwa balozi uingereza wakati nyerere anakufa
 
Wala hilo halisaidii lolote hata kama alifariki siku hiyo hiyo alipolazwa Hospitalini haiwezi kuubadili ukweli kwamba kwasasa ni Marehemu!!!!

Na anatumikia adhabu kwa dhulma na udikteta aliowafanyia watanganyika
 
Kama una taarifa zaidi zimwage hapa sio kuleta habari ambayo haijakamilika.
 
Ukweli hauwezi funikwa siku zote. Ni kama kuuzuia moshi kwa kawa.

Kama vile kuvuja kwa taarifa za mipango na utekelezaji wa kumwua Nyerere kulivyokuwa, kisha kuibukia 2012 kwa uwazi zaidi. Ndivyo tarehe rasmi ya kufariki inapojulikana.

Nyerere alifariki tarehe 7 Oktoba 1999.

Tarehe nyingine ni danganya toto. Ukweli unasema, huwezi kuwadanganya watu wote kwa nyakati zote. Ndicho serikali iliyoongozwa na B W Mkapa ilichofanya.

Mkuu Mwalufunamba,

1. What is your definition of Death?

2. Kwa ushahidi/vielelezo gani unaweza kutupa ili nasisi/namimi niamini kama wewe?

3. Why now? Ni kwanini kwa taarifa yako uwe nayo kwa muda sasa, na uiibue sasa?

4. Tukishajua kuwa kuwa ni tarehe halisi unataka iweje?

5. Mimi naweza kumuangalia Hayati Mwl J.K Nyerere kama Baba wa Taifa, lakini wapo wanaomuangalia pia kama Marehemu Mume na aliyekuwa baba wa familia, Je, wao wanasemaje kuhusu kauli yako?
 
Na anatumikia adhabu kwa dhulma na udikteta aliowafanyia watanganyika

Umejuaje? Wewe ni Malaika Gabriel? Usishangae ukimkuta amekaa mkono wa kuume wa mwumba wake akibadilishana mawaidha na Mtakatifu Petro.
 
Aliyeambiwa auelezee umma uelewe kwa nini Nyerere alienda UK akitembea akarudi maiti,Mzee Nkapaa huko Arumeru alishindwa kujitetea PAMOJA NA UWEZO MKUBWA WA KUJIELEZA!Nyimbo zile za Komba na KWAYA fulani dakika 5 baada ya Mheshimiwa Rais kutangaza habari ya msiba,nyimbo zenye notation nzuri na zilizopangika kimuziki ni kazi iliyochukua siku walau 3 za zoezi la nguvu.Besides,Kingunge alitumwa UK kudhibiti utoaji wa taarifa za ugonjwa wa MWALIMU.Ninyi magwiji wa clinical death na biological death mnakumbuka saa 12 alfajiri siku RAIS ALIPOONA NI VYEMA KUTUJUZA Mwalimu amelala mautini baada ya kushauriwa na KINGUNGE, alfajiri kwenye AMKA NA BBC Makongoro Nyerere alisemaje?
Ni vizuri tutafunguka na kutambua tabia ya viongozi wetu hapa Tanzania ya kudanganya wananchi!Inasaidia kumjua mwongo, mwizi,fisadi,mkware,na watu woote wa aina hiyo lil kuziba mianya usifanywe ***** mara mbili.Kwa mfano ukiwasikia wanasema uchumi unakuwa kwenye majukwaa ya siasa usishangilie tu uulize mbona ukweli siyo huo?
 
October 7 ndio nyerere day,nakumbuka makongoro alipohojiwa na BBC alisema 'Tuambiwe ukweli baba yetu amefariki lakini tunazungushwa'

Dai haki yako mtanzania.
 
Back
Top Bottom