Siku ya kwanza kuamkia kwenye nyumba yako, furaha yake usipime!

Biashara sio kwa kila mtu! Mwingine hiyo pesa ataipeperusha asubuhi kabla jogoo hajawika.
Mtu anaweza kujenga nyumba yenye thamani kubwa lakini sio kwamba alikua na hiyo pesa yote kwa mara moja.
Kwa mfano huyu jamaa kajenga kwa miaka mitano, unaweza kukuta alianza kujenga akiwa na milioni moja au mbili.
Akajichanga kidogo kidogo tena akaendeleza hadi kuja kukamilisha. Usimlaumu sana ila wewe unaweza kuweka ushuhuda wako hapa kama ambavyo yeye ametuletea wake wa maamuzi ya kujenga.

kitu nakubaliana nawewe ni kwamba wengi wetu hatuna elimu ya uwekezaji/ Biashara.
Umenena vyema
 
Habari ndugu,

Baada ya kukuru kakara za kupanga nyumba mbalimbali hapa jijini Dar es Salaam kwa miaka 5 hatimae nikafanikiwa kujenga nyumba yangu.

Nilikuwa nasikia tu watu wakisema mjini kuna baba mwenye nyumba, sasa nimejionea mwenyewe jamani nawaambieni furaha na amani yake usipime.

Siku ya kwanza kuhamia kwenye mjengo wangu kila mtu aliamka ana furaha na amani kuanzia mimi, watoto, mke na jamaa zangu.

Ndugu zangu ya Mungu mengi, ashukuriwe aliye juu.
Ni haki kufurahia asikwambie mtu ujenzi unaumiza Sana.
 
Wakuu, ninakuja kwenu kijana ninayetaka kumiliki mjengo!

Nina mil 8! Kiwanja ninacho chanika! Kipo tambarare ardhi ni Mchanga.

Mchanga roli la 15m3, ni 250,000, maji yapo karibu Ni kufunga tape tu.

Nyumba ya sebule, master, jiko, store.. njoo Cha ndani Cha kawaida.

Kwa pesa hiyo naweza kujenga Boma, kuezeka, plaster, na kufunika paa pamoja na milango na madirisha ya grill?
Acha utani hata paa humalizi
 
Back
Top Bottom