Siku ya kutokunywa pombe Duniani kitaifa inafanyika Dodoma

Kurzweil

JF-Expert Member
May 25, 2011
6,622
8,397
MTANDAO wa wadau unaopambana na unywaji pombe kupita kiasi (TAAnet), leo unaadhimisha siku ya kutokunywa pombe duniani ambayo kwa mara ya kwanza inafanyika kitaifa mkoani Dodoma

Taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Wanahabari Wanawake nchini (Tamwa), Edda Sanga, ilisema maadhimisho hayo yatakayoongozwa na kaulimbiu ya mwaka huu ya "Maendeleo ya Viwanda yataletwa na Udhibiti wa Unywaji Pombe kupita kiasi", yataanza kwa maandamano yatakayopokelewa na Mkuu wa Mkoa huo Dk. Bilinith Mahenge, kwenye viwanja vya Chuo cha Biblia.

Kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani (WHO), watu zaidi ya milioni tatu wamefariki kutokana na matumizi mabaya ya pombe mwaka 2016. Zaidi ya robo tatu ya vifo hivyo vilikuwa ni vya wanaume. Kwa ujumla, matumizi mabaya ya pombe husababisha zaidi ya asilimia tano ya mzigo wa magonjwa duniani.

“Matumizi ya pombe na athari zake ni tatizo linalozidi kukua nchini na linapaswa kudhibitiwa haraka iwezekanavyo. Ongezeko hili la unywaji pombe katika jamii ya Watanzania, TAAnet inazikumbusha taasisi husika pamoja na serikali kuangalia kwa haraka namna ya kudhibiti tabia hiyo ili kunusuru maisha ya vijana yanayoendelea kuharibika kila siku.

“Kama wadau wa kupambana na madhara ya unywaji pombe, tungependa kuona watunga sera wanalitafutia tatizo hili ufumbuzi kwa kuwa na ubunifu ambao utaokoa maisha, kama vile kutokomeza unywaji pombe kupindukia,” ilisema taarifa hiyo.

Tanzania ni miongoni mwa nchi ambazo bado haina sera/muongozo wa pombe ikilingalinishwa na nchi jirani kama Kenya, Malawi huku Uganda ikiwa njiani kumalizia mkakati wa sera yao ya pombe.

Taarifa hiyo ilisema TAAnet inapendekeza kupitiwa kwa sheria na kuweka masharti kuhusiana na matangazo, uuzaji na udhamini wa pombe pamoja na kuonyeshwa kwa onyo la athari za pombe kwenye matangazo ya vilevi ili kupunguza matumizi yake kwa jamii.

“TAAnet inaamini kwamba, endapo kutakuwa na sera ya kudhibiti matumizi mabaya ya pombe, wanaume watawajibika zaidi na kuacha matumizi yaliyopitiliza ya vileo, yanayochangia unyanyasaji wa kijinsia, na badala yake kuchangia ustawi wa familia na kukuza maendeleo kwenye jamii na katika Taifa kwa ujumla.”

Kupunguza matumizi mabaya ya pombe kutasaidia kufikia malengo kadhaa yanayohusiana na afya ya Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDG), ikiwa ni pamoja na afya ya uzazi na watoto, magonjwa ya kuambukiza, magonjwa yasiyoambukizwa na magonjwa ya akili, majeraha na sumu.

Chanzo: ITV
 
mkuu naomba uniulizie na sisi walevi tafrija yetu inafanyika lini na itakua wap kitaifa.nawasilisha
 
Ubaya na wema ni mapacha , kunywa sana mpaka kuchanganyikiwa ni ubaya kwani ni kipoteza nguvu kazi lakini TRA na viwanda vya bia vinapeta . Huenda kuna kaformula kuwa lazima mtu aumie ili mafanikio yapatikane . Mf . Waafrika tunanyonywa ili mzungu aendelee !!kisingizio "dini" ikipigwa shavu moja mgeuzie na shavu jingine ! You see !!!
 
Back
Top Bottom